Mkuu Jove, hicho kinakuwa ni kipindi ambacho ni kama kuamka kutoka uzingizini. Yaani kunakuwa na mwamko wa kitaifa au hata kimataifa. Kwa mara ya kwanza kilitokea Ulaya kwenye karne ya 14 ambapo Wazungu ni kama waliamka na kuanza kukuza SANA mambo ya fasihi na utamaduni. Yaani ni kuamka kwa maana ya kuinuka, kupiga hatua na kusonga mbele kwa ari kubwa.