Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya kidato cha 6

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Leo baraza la mitihani la Tanzania NECTA limeyatoa matokeo ya kidato cha sita, kwa uzoefu wangu nimeona ni vyema tuanzishe uzi huu maalumu ili tushauriane, tueleweshane, tuambiane nini cha kufanya na namna ya kuchagua vyuo.

Ikumbukwe TCU wametoa vigezo vipya kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu.

Karibuni....
 
KE_PCM_ECE point 13,sijui watamchagua au ndio tumftafutie genge la nyanya maana pesa ya diploma hamna?
 
Nimeona kuna thread nyingi zimefunguliwa kila mtu akiulizia kuhusu kujiunga na chuoo na watu wamekuwa na Matokeo tofauti tofauti!!!

Kwa utaratibu ulio tolewa hivi karibu na tume ya vyuo vikuu ni kuwa CUTT POINT minimum ni 4.0 SASA BASI KATIKA MATOKEO YAKO AU YA NDUGU YAKO HAKIKISHA KUWA ANA (D,D)! NAKUENDELEA

Kama atakuwa ana D moja kushuka chini huyo chuo kikuu hataweza kwenda bila kujari combination alio isomaaa!!!

Na watu hao wengi wapo kwenye Division Three (3) ya point 15. Na wengine point 14! Usihangaike kuomba chuo kama huna D 2 na kuendelea!

Kwa watu wa Diploma ni GPA ya 3.5 kinyume cha hapo ni usisumbuke kuomba chuo kikuu

Huo ndio uelewa wangu kulingana na utaratibu wa chuo ulivyo kwa sasa!!!

Kama kuna mwenye nyongeza karibu
 
Yaani TCU hawataki kuona E kati ya masomo 2 yanayohesabiwa point hata kama ana AEE chuo atakisikia kwa wenzake.
Asante mkuu ingawa nimeona tarifa kwenye gazeti la "HABARI LEO" la leo zikikanushwa hizo tarifa na Mr Mkaku kuwa sio zakweli ngoja niendelee kuvuta subira.
 
kwa matokeo haya ya kidato cha sita basi tutalijie vyuo vingi vikikosa wanafunzi na kubadili matumizi au vikifungwa kabisa hasa, mfano wanafunzi wengi walisoma sayansi wengi wana div.three ya ya 15 so vyuo kama SUA, BUGANDO, KCMC, IMTU, n.k vitakosa wanafunzi, na hatimaye vitafungwa na hatimaye watafugia kuku, serikali ijaribu kuliangalia hili kwa kina sana na mapana yake wasiangalie sana Arama alizopata mtu bali wa focus kwenye uwezo wa mtu.
 
Asante mkuu ingawa nimeona tarifa kwenye gazeti la "HABARI LEO" la leo zikikanushwa hizo tarifa na Mr Mkaku kuwa sio zakweli ngoja niendelee kuvuta subira.
Fungua mwenyewe website ya TCU ujisomee simu na data unazo kwa nini usifungue website ya TCU ukasoma hilo tangazo?
 
Wakuu shikamoo,
Mimi ni mtahiniwa wa ACSEE 2016, naomba mnisaidie grades zilizotumika kwenye upangaji matokeo yetu wakati wa usahishaji make mimi kama mimi zinanichanganya..msaada tafadhali
 
kwa matokeo haya ya kidato cha sita basi tutalijie vyuo vingi vikikosa wanafunzi na kubadili matumizi au vikifungwa kabisa hasa, mfano wanafunzi wengi walisoma sayansi wengi wana div.three ya ya 15 so vyuo kama SUA, BUGANDO, KCMC, IMTU, n.k vitakosa wanafunzi, na hatimaye vitafungwa na hatimaye watafugia kuku, serikali ijaribu kuliangalia hili kwa kina sana na mapana yake wasiangalie sana Arama alizopata mtu bali wa focus kwenye uwezo wa mtu.
Sasa uwezo wa mtu unaupima Je?
 
Back
Top Bottom