Karibu Tujuzane mbinu za kuwa pilot

Karibu Tujuzane mbinu za kuwa pilot

Mtu mbalimbali

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
887
Reaction score
1,633
Habari za muda wanajukwaa, poleni na majukumu

Tanzania tumekuwa na uhaba wa wafanyakazi wengi wazawa katika fani ya aviation na pilot kwa ujumla kutokana na changamoto mbalimbali hasa za kiuchumi katika familia zetu.

Mimi ni kijana wa miaka 20

Nina matarajio ya kuwa rubani na imekuwa ndoto yangu tangu nilipokuwa mdogo lakini ninakumbana na matatizo fulani hasa ya kifedha ambayo huwa yananikatisha tamaa ya kufikia malengo yangu hivyo naomba kuuliza kama naweza kupata sponsorship au scholarship kutoka ndani au hata nje ya nchi kwa masomo ya shule ya urubani ambapo nitapata ujuzi wangu kuhusu usafiri wa anga

Ni imani yangu na natumain naweza kupata msaada kupitia Jamii forums
Kwa namna moja au nyingine ili niweze kufikia malengo yangu kwa hivyo mwenye ujuzi wowote juu ya aviation tafadhali naomba anipe muongozo wa namna ya kupata ufadhili wa kusoma katika flight schools.
asante
the-office-boeing-737-800-83753109%20(1).jpg
 
Hakika umechagua fani nzuri na huwa haina changamoto kwenye kupata vyuo Ila kipengele ni kimoja tu,unatokea kwenye familia gani kiuwezo?. Hii fani inahitaji uwezo mkubwa wa kifedha. Million 5 hadi 250 zitatumika kama ada na field hivyo lazima ujitoe mzee.

NB: Kama utapata konekshe ya pilots katika kipengele cha kukusanya masaa ya uongozaji ndege juu gharama zina weza kupungua.
 
Asante mkuu
Familia yangu haipo vizuri sana kiuchumi na ninahofia hicho kinaweza kuwa kikwazo cha kufikia ndoto zangu

Lakini kwa sasa nategemea sana ufadhilii japo nao ni ngumu kupata
Ila nimewasiliana na baadhi ya pilots wakongwe hasa kwa nchi za Marekani na Canada wengi wanasema waliingia kwenye hii career kupitia jeshi
 
Penye nia pana njia. Uwezo mdogo wa familia isiwe chanzo cha kukata tamaa. Watu wengi walitoka familia maskini, lakini nia yao iliwafikisha walipopahitaji.

Kwa bahati nzuri, sasa hivi fani hiyo inafundishwa hapa nchini na baadhi ya vyuo vyetu! Hii nadhani inapunguza hata gharama ya mafunzo ukilinganisha na vyuo vya nje.

Nadhani pia vyuo hivyo (vya hapa nchini) vinafahamiana na taasisi nyingi zinazodhamini wanafunzi (tofauti na HSLB) kwenye course hiyo, maana vinachukua wanafunzi hadi kutoka nchi zingine.

Nakushauri nenda katika moja ya vyuo hivi, ukaulizie suala ka udhamini wa wanafunzi wengine ambao tayari wanasoma course hiyo, huenda ukapata muelekeo mzuri. Kila la heri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri wako nitaufanyia kazi
 
nikifanikiwa nitaleta mrejesho hapa iwe na faida kwa wote wenye nia kama yangu
Kila la kheri nilikuwa ndoto kama zako ....umasikini zilaishia hewani ...pambana jiwekee muda na malengo yako kila is kheri .....
 
Hela yako tu
Dollar 17,000 unapata PPL pale Moswood Terminal 1
Hapo unapigwa Theory, Simulator na Flight Time ya Masaa 50

Japo waweza anza na Theory afu kwenye kusaka Masaa ili upate leseni, ukipata 600,000 unaenda paa Saa lako 1 unatulia

Ukimaliza PPL, Tafuta pesa kapige CPL ambapo huko utahitajika utimize Masaa 250 kwa C208 Caravan

Hayo masaa ndio ghali maana kila saa 1 ni Dollar 200 +- 50

Ukimaliza hapo unapiga APL, baada ya hapo ukipata shirika litakusomesha lenyewe kwa mkataba wa kuwafanyia kazi
 
Habari za muda wanajukwaa, poleni na majukumu

Tanzania tumekuwa na uhaba wa wafanyakazi wengi wazawa katika fani ya aviation na pilot kwa ujumla kutokana na changamoto mbalimbali hasa za kiuchumi katika familia zetu.

Mimi ni kijana wa miaka 20

Nina matarajio ya kuwa rubani na imekuwa ndoto yangu tangu nilipokuwa mdogo lakini ninakumbana na matatizo fulani hasa ya kifedha ambayo huwa yananikatisha tamaa ya kufikia malengo yangu hivyo naomba kuuliza kama naweza kupata sponsorship au scholarship kutoka ndani au hata nje ya nchi kwa masomo ya shule ya urubani ambapo nitapata ujuzi wangu kuhusu usafiri wa anga

Ni imani yangu na natumain naweza kupata msaada kupitia Jamii forums
Kwa namna moja au nyingine ili niweze kufikia malengo yangu kwa hivyo mwenye ujuzi wowote juu ya aviation tafadhali naomba anipe muongozo wa namna ya kupata ufadhili wa kusoma katika flight schools.
asante View attachment 2545763
airport@flymwaa.com or telephone 0715 555 777 Monday thru Friday. You may also like to visit our website at www.flymwaa.com and our video is on YouTube at .
 
Uzi mzuri kijana wangu anasumbua sana analilia urubani kwa SA naskia ni best kwa kozi hii so mwenye info atujuze pls till anamaliza kozi kiasi gani nianze jipanga wakuu yupo std 7 kwa sasa
 
Jf tuna watu wengi sana na wenye taaluma mbalimbali
naamin kupitia huu uzi ,fursa na elimu juu ya urubani zitaonekana
 
Back
Top Bottom