Karibu Tujadili Kuhusu Upendo

Jeho

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
5,068
Reaction score
5,559
Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo(1 Kor. 13:13).

Siyo ajali kuwa orodha ya Paulo inayoeleza sifa za kitabia zinazotambulisha tunda la Roho huanza na upendo. Upendo ni sifa kuu kwa Mkiristo kwa vile ni sifa inayoelezea sifa ya tabia ya Mungu. Ni upendo uliomsukuma Mungu kutuumba, kututunza, na kujifunua mwenyewe kwetu, na kutupatia mwanawe ili aje kutukomboa.
Yohana huelezea kinaganaga na kwa maneno rahisi kuwa--"Mungu ni upendo" (1 Yohana 4:16). Kwa sababu upendo ni kiini cha tabia yake, upendo wapaswa kuwa kiini cha tabia yetu pia. Naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake (1 Yohana 4:16).
Kwa masikitiko, neno upendo hutumiwa visivyo siku hizi. Mara nyingi tunasema tunapenda hali ya hewa, tunapendelea chakula fulani tunachokipenda, tunampenda mbwa wetu. Lakini aina hizi za upendo hazikidhi kipimo cha upendo wa kweli wa Mungu(soma 1 Wakorintho 13). Upendo ni kitu tofauti kabisa, kitu fulani kinachoathiri maisha yetu kwa ujumla, mwenendo wetu, na namna tunavyohusiana na wengine. Viambato vya upendo ni kifurushi kimoja, na siyo orodha ya vitu ambavyo tunachagua vile vinavyotuvutia na kupuuza vingine.
Karibuni wanajamvi wote, tujadiri katika UPENDO.

Nakala kwa: Ntuzu Nkwesa Makambo Eiyer tedo juve2012 Blueband Ls man charminglady na wengine wote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Basluma Original Nashukuru sn Kwa Uzi Huu Na Kusema ule ukweli UPENDO ndio kila KITU! Na UPENDO Ni sifa kuu ya MUNGU!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tujiandae kujibu swali hili ambalo wengi walio neutral na mambo ya dini huuliza,kama Mungu ni upendo,kwa nini ameruhusu dhambi na mateso kuwepo?this is the most challenging question ambalo ni lazima ukutane nalo ukiwaambia watu wa leo waliojeruhiwa na maisha kwamba Mungu anawapenda sana.tujibu hili swali tukiendelea na mnakasha huu.
 

Ningeomba mods wauache uzi huu hapa jukwaa hili ili hao wenye kuuliza maswali kama ya hapo juu waje.kule kwenye jukwaa la dini si wengi wenye access nako na hii mada iko huru kwa mtu yeyote kujadili from any perspective,it is both religious and intellectual.
 
Pendaneni pendaneni, kama nilivyowapenda mimi.


With love, nothing is impossible!
 
Pia ningependa kusikia waislam wanafundisha nini kuhusu upendo?@faizafoxy
 
Nakala kwa Mkuu Invisible na moderators wengine.
 
Last edited by a moderator:
Ntuzu hebu niitie huyu dada hapo juu mie nashindwa kuandika ID yake..tupate maoni from different corners provided hatutaleta yale mambo ya kunyoosheana vidole hapa jamani.tuzungumzie upendo basi.
 
Upendo ni nn?na mwenye upendo anakuwaje? Sbb hata ccm wanadai nawao wanaupendo nawakati ni mashetani.
 
Kila mtu anapohisi kuumizwa kuwa ndani ya Mungu angetambua jambo hili kuwa Mungu hawezi kutupitisha katika njia yenye mawe pasipo kutuandalia viatu imara vya kuhumili mawe hayo bila shaka maswali hayo yasingekuwepo. Tatizo ni kwamba, tunapopatwa na matatizo yaliyo magumu kwetu tunahisi kama Mungu ametuacha, kumbe Yesu alituahidi hivi tazama mimi nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahali, kwa maana kwamba, hata katika shida yupo karibu nasi hata yaweza kuwa zaidi ya anavyokuwa karibu katika vipindi vyetu vya raha.
 
Upendo ni nn?na mwenye upendo anakuwaje? Sbb hata ccm wanadai nawao wanaupendo nawakati ni mashetani.
Mwenye upendo anakuwa hivi anampenda jirani yake kama nafsi yake mwenyewe. Nikupe sifa za upendo ili uweze kujua kama hao unaosema kuwa wanadai wanaupendo kama ni kweli au la.
Upendo huvumilia
upendo hufadhili
upendo hauhusudu
upendo hautakabari
upendo haujivuni
upendo haukosi kuwa na adabu
upendo hautafuti mambo yake
upendo hauoni uchungu
upendo hauhesabu mabaya
upendo haufurahii udhalimu
upendo hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hutumaini yote, hustahimili yote; upendo haupungui neno wakati wowote(1Wakorintho 13).
Hivyo kama wana sifa hizo katika upendo wao, basi ni kweli wana upendo wa kweli na sio unafiki.
 
Ntuzu hebu niitie huyu dada hapo juu mie nashindwa kuandika ID yake..tupate maoni from different corners provided hatutaleta yale mambo ya kunyoosheana vidole hapa jamani.tuzungumzie upendo basi.


FaizaFoxy tafadhali naomba uje Huku!

Asante!
 
Last edited by a moderator:
Wakuu mkisoma kitabu CHA Yohana Wa kwanza 4:1-21 mtakuta maneno mazito sn juu ya UPENDO.

KM kuna mtu anaweza kuileta Hiyo sura Hapa kiurahisi ITAKUA Vzr sn tukayapitia HAYO maneno ya MUNGU!
 


Nakubaliana Na maelezo yako Mkuu lkn wakati mwingine MUNGU huwaacha wapitie tabu ili wapate kumjua YEYE KM Ni MUNGU! Kwahiyo MUNGU hapendi mtu aangamie Au apotee Au apate shida Au Taabu lkn SISI Ni sababu ya mapito yote HAYO! SISI ndio chanzo CHA yote HAYO! Kila Jambo liko Na ujira wake KM Ni jema Au baya! Na MUNGU tangu awali YEYE Sio sababu ya mabaya!
 
VIPENGELE VYA UPENDO
Yesu akamwambia, mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanan nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako(Mathayo 22:37-39, soma pia Kumb. 6:5).
Tafsiri za Biblia, kama zilivyo kazi zote za uandishi, hutofautiana katika uchaguzi wa maneno. Kwa mfano Ndege alikuwa mdogo katika tafsiri nyingine inaweza kusomeka, Ndege alikuwa mdogo sana au katika tafsiri nyingine Ndege alikuwa mchanga. Tafsiri zote hizi zitakuwa ni sahihi. Kwa hiyo ili kujifunza tunda la Roho, itasaidia sana kutafsiri maana za maneno kwa kuangalia lugha za awali. Katika kumbukumbu 6:5, neno la Kiebrania lililotumika kwa upendo ni ahabta, ambalo kimsingi humaanisha upendo unaodhihirishwa kupitia nia, akili, na vitendo badala ya upendo unaodhihirishwa kwa hisia na msisimko. Ni upendo wa kiwango cha juu zaidi, kwani humhamasisha mtu kutenda lililo sahihi na adili bila kujali hisia zake. Hivyo, upendo Yesu anaouzungumzia katika Amri Kuu ni wa adili, safi, na aina ya juu kabisa ya upendo wa kujitoa mhanga na ndio ambao kila mtu anaamuriwa kuwa nao kwa Mungu.
Wayahudi tayari walijua kuwa amri kuu ya kwanza ilikuwa ni kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa roho yote, kwa akili zote, na pia kwa nguvu zote, kama anavyoongezea Marko(tazama Marko 12:30). Katika kutaja vipengele vyote vinne vya binadamu, Yesu kimsingi analeta pamoja vile mtu alivyo. Yeye anasema unahitaji kumpenda Mungu kwa nafsi yako yote. Kusudi lake siyo kuchambua maana mojamoja ya kila neno; hata hivyo, itakuwa ni faida kubwa sana kujifunza vipengele hivi vinne.
Kumpenda jirani yako kama nafsi yako humaanisha kuwapenda watu wote kwa moyo wako wote. Upendo unaotajwakatika "amri hii ya pili" ni sawa na ule unaoongelewa katika "amri ya kwanza". Ni upendo katika vitendo, ukihusisha nia na makusudio ya moyo. Kuwapenda jirani zetu kama sisi wenyewe humaanisha kumjali mtu mwingine kama vile ambavyo ungalijijua wewe binafsi.
Ni rahisi kuzungumzia kuwapenda wengine kama nafsi yako; jambo lisilo rahisi ni kuweka suala hilo katika vitendo. Je, ni kwa kiasi unafaulu katika eneo hili? Ni kwa jinsi gani utajifunza som gumu la kuifia nafsi ili uweze kuhudumia mahitaji ya wengine?
 
Kabisa mkuu, na ndio maana anasema mtu anapojaribiwa asiseme anajaribiwa na Mungu, maana mtu hujaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe. Kwa kiasi fulani sisi wenyewe ndiyo chanzo cha kupata matatizo tunayoyapata, japo yapo pia ambayo huja kwa njia iliyo nje yetu mfano kwa Ayubu.
 

Ni swali rahisi lakini gumu kwa akili za binadamu.....
 

Binadamu tu wabinafsi by nature haijalishi unajaribu kuiweka vipi lakini si rahisi kupenda kabla hujajipenda, ukijipenda nakutambua Upendo ambao ni Mungu ndani yako huwezi kuwapenda wengine.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…