KARIBU TANGANYIKA Bye Bye CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KARIBU TANGANYIKA Bye Bye CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jul 10, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huu ni wakati wa kuiondoa CCM madarakani kwa kutumia mwigo wa Katiba mpya ,Katiba mpya inamuelekeo wa kuwepo serikali tatu ,mawazo yalio mengi kutoka Zanzibar ni kuwepo kwa serikali tatu au kurudishwa kwa serikali ya Tanganyika.

  Hili litakuwa pigo takatifu kwa serikali iliyopo ya Muungano na zaidi ni pigo kwa Chama tawala ambacho kimehodhi kila kitu na zaidi ambalo ni hatari mali na utajiri wa Tanganyika ambao ni mkubwa kuliko wa Zanzibar haumnufaishi mwananchi wa kawaida kutokana na ufisadi unaofanyika ukiongozwa na WaTanganyika wanaopata nafasi za uongozi ndani ya serikali ya Muungano.

  WaTanganyika hamna budi kumuunga mkono Mheshimiwa Tundu Lissu katika kuwakilisha maoni yenu juu ya kuitaka na kuirudisha serikali ya Tanganyika ,wakti ni huu na Chadema imeonyesha njia na kumulika ni wapi Watanganyika nao watajiondoa katika jinamizi hili liitwalo MUUNGANO ,kusema ukweli dudu hili Muungano sio linawakandamiza waZanzibari tu bali hata WaTanganyika kwani wao ni zaidi kwa maana ni wengi kiidadi. Hivyo uchumi ambao mafisadi wanauteka ni mkubwa sana wakitumia kivuli cha Muungano.

  Kuweni makini na ondokaneni na dhana hizi za kero za Muungano sijui mafuta ,madini ,gas na vinginevyo haya ni machanga ya macho tunayopigwa nayo wala hakuna linalofanyika ,ona hili mafuta hayaja anza kufukuliwa tayari wachache wanamiliki accounts kwa kutumia mafuta na gas.

  Kuwanasa wezi hawa ni kuirudisha Tanganyika na sidhani kama itakuwa rahisi kwani hawapo tayari ila mkishikamana kwa umoja basi Tanganyika itarudi na hizi kero itakuwa ndio mwisho wake.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hv kero za muungano si zilishughulikiwa na ccm na cuf!
  hazijaisha?, basi hivi vyama ni dhaifu!
   
 3. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Let Zanzibar GO
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kero za Muungano ni mtego usioteguka ,ni walaji au tuwaite mafisadi ambao wamekuwa wakitumia huo msamiati lakini hakuna ukweli ndani yake ,ni changa la macho ,sio ccm wala cuf ,viongozi walioko ndani ya Muungano ndio wanaofaidika na kero hizo ,mimi na wewe na wengine ni wapanga foleni tu.

  Dawa ya kero ni kurudi kwa Tanganyika bila ya hivyo sote ,si WaTanganyika si WaZanzibari tutakuwa na kuendelezwa kuwa watumwa ndani ya nchi yetu ,mfano lima karafuu vuna kauze serikalini ,lima pamba vuna kauze serikalini ,lima kolosho vuna kauze serikalini ,wananunua kwa bei waitakayo wao na kama hukupeleka kuwauzia ,watakushitaki ! Je hujafanywa mtumwa ndani ya nchi yako ?

  AMkeni kurudi kwa Tanganyika ni lazima kama kufa otherwise ,tutapigwa virungu na kuogeshwa kwa maji ya washawasha milele na milele , kuyaondoa haya ni lazima CCM na muungano wake waondoke.
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Haya ndio mawazo tunayoyataka.

  Mungu akubariki.
   
 6. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar ikiondoka, Tanganyika itasajiliwa upya UN?? Tunakuwa Taifa lililopata Uhuru? Kutoka kwa koloni lipi??
   
 7. A

  Awo JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 792
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Kikwete = Gorbachev! Nyerere alisema "mtapata Gorbachev wenu hapa na atavunja muungano..." Yametimia.
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmh! leo Mwiba kawa mchongoma....ahsante kwa kufunguka.
  Hata hivyo ccm wanaing'ang'ania Zanzibar kwa faida ya kura za urais ambazo wakazi wa huko
  umpigia kura rais wa bara....ila wakazi wa bara haturuhusiwi kumpigia kura rais wa visiwani.
  Je umenielewa? za mbayuwayu changanya na zako
   
Loading...