Karibu Rubondo Island

May 3, 2019
53
144
KARIBU RUBONDO ISLAND.

Leo 10:15pm, 27/10/2019.

Sasa Watalii kutoka Gatwick London nchini Uingereza, New York nchini Marekani, Mumbai na New Delhi nchini India, Guangzhou nchini China wataweza kusafiri moja kwa moja toka nchini kwao kwa Usafiri wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa kutumia ndege zake aina ya Boeing kwa ajili ya kwenda kutalii kwenye visiwa vya Rubondo na Saanane ambavyo vinapatikana katika Ziwa Victoria.

Ndege hizo pia zitashuka katika majiji ya Arusha na Mwanza kupeleka watalii katika mbuga kubwa kabisa barani Afrika. Mbuga za Serengeti na Ngorongoro na kupanda Mlima Kilimanjaro tokea Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania wakianzia katika mji wa mzuri wa Moshi kuelekea katika vilele vya Mawenzi au Kibo katika Mlima Kilimanjaro.

-Upekee wa mbuga iliyo ndani ya kisiwa cha Rubondo.

Mbuga ya Rubondo inapatikana katika kisiwa kilichopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, ambalo ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani, likiwa na limeenea kwa robo tatu nchini Tanzania,Kisiwa cha Rubondo inapopatikana mbuga ya Rubondo imeundwa na mkusanyiko wa visiwa tisa vidogo vidogo.

Sehemu ya maji ya kisiwa cha Rubondo ni makazi mujarabi kwa samaki aina kumi na tatu na kwa namna ya pekee kisiwa cha Rubondo kina mazingira muafaka ya kuzaliana samaki wakiwemo Sato na Sangara. Sangara huweza kuwa na ukubwa wa hadi kilo 100 na Sato wakubwa wenye kilo 20.

Fukwe za kisiwa cha Rubondo ni miongoni mwa makazi ya wanyama asilia wanaopatikana hapo tu. Wanyama aina ya Pongo na Nzohe. Lakini si wanyama hao tu, bali hifadhi hii ni maskani makuu ya ndege warukao aina mia nne na samaki aina ya pekee kabisa kama Zumbuli, Chechele na Taisamaki.

-Jiografia ya mbuga ya Rubondo.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 457 na iko kaskazini magharibi mwa Tanzania, katika mkoa wa Geita. Pia hifadhi hii -Inafikika kwa ndege za ATCL na ndege binafsi za kukodi kutoka Arusha, Ziwa Manyara, Serengeti na Mwanza. Kwa njia ya barabara kutoka Mwanza-Sengerema-Geita-Nkome kisha kwa boti hadi hifadhini, na kwa meli unaweza kusafiri kwa meli ndogo kutoka Milena na Bukoba vilevile kwa njia ya barabara kutoka wilaya za Biharamulo na Muleba kupitia kijiji cha Mganza.

-Ujirani wa kisiwa Cha Rubondo na visiwa vingine.

Upekee wa kisiwa cha hifadhi ya taifa Rubondo ni huu ukubwa wa kilomita za mraba 457 ambazo kati yake 237 ni nchi kavu na 220 ni maji.

Mbuga hii ya Rubondo ipo jirani na visiwa 11 vya makazi ambavyo ni Mizo, Nyamitundu, Chitende, Katera, Iroba, Chambuzi, Munyila, Makosi na Izilambula.

Kipekee kisiwa cha hifadhi ya taifa Rubondo na Kisiwa cha Saanane ndio visiwa pekee hapa nchini na Afrika vinavyopatikana katika makazi ya maji ya ziwa na visiwa hivi vikubwa vinapatikana katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza,Tanzania.

-Historia ya mbuga ya Rubondo.

Mbuga ya Rubondo ipo kusini magharibi mwa Ziwa Victoria, jijini Mwanza,Tanzania na sasa mbuga ya Rubondo inaunganishwa na mkoa mpya wa Geita.

Wenyeji na wazawa wa eneo la mbuga ya Rubondo ni Wazinza. Wazinza waliokuwa wakiishi katika kisiwa hicho kutoka katika ukoo wa wanyarubondo. Maana ulivyoeleza utadhani wanyarubondo ni kabila.

Historia inatuambia Wazinza kutoka katika ukoo wa Banyarubondo waliishi katika eneo hilo hadi mwaka 1964-1965 serikali ilipolazimika kuwaondoa kwa kuwalipa fidia na kisiwa cha Rubondo kutangazwa pori la akiba mnamo mwaka 1966 na baadae kupandishwa daraja kuwa hifadhi ya taifa mwaka 1977. Sasa mbuga ya Rubondo ambayo ipo kusini magharibi mwa ziwa Victoria.

Nimalizie kwa kutaja uzuri wa misitu minene yenye wanyama wazuri ambapo iliwavuta University College London kuja kufanya utafiri katika mbuga hiyo Mwaka 2012 hadi 2014.Vilima vizuri na mchanga wa Ziwa unaofanana na mchanga wa baharini unaleta kivutio kingine katika mbuga hiyo ambayo ipo katika Ziwa Victoria. Mungu ameibariki sana Tanzania,ni jukumu letu kutumia vyema baraka za Mungu katika nchi hii ya Tanzania.

Karibuni Rubondo Island using park boat from two different locations. One option is the boat from Kasenda, a small village near Muganza in Chato District. The other option is the boat from Nkome in Geita District. Via Mwanza you can board airplane as Rubondo Airstrip can be reached with Auric Air or Coastal Aviation and Air Tanzania.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania, Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki na kumlinda Rais wetu Daktari John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755 078 854.
 
Je kuna tembo na TWIGA hapo Rubondo?

JE kuna sokwe mtu?

Watalii wangapi hufika kwa mwaka?
 
Naomba kujua entrance fee na accommodation kama logde au hostel price kwa mtanzania per day
 
Back
Top Bottom