Karibu mwaka mpya wa 2023

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Ndugu zanguni Watanzania, bado muda mfupi kuingia mwaka mpya wa 2023.
Bila shaka kila Mtanzania anaweza kukubaliana na mimi kwamba, huko nyuma sisi kama Watanzania kwa ujumla wetu tukianza na mtu mmoja mmoja hatujawajibika ipasavyo na hali hiyo imeweza kutufikisha hapa tulipo.
Mapendekezo yangu ni kwamba, mwaka 2023 uwe ni mwaka wa kuandika Historia mpya ya Mapinduzi ya Fikra kwa kila Mtanzania.

1. Tukawe ni watu wenye uwezo na ujasiri wa kuwahoji Viongozi wetu pale wanapokwenda kinyume na matarajio ya Nchi.

2. Tukawe ni watu wenye uwezo na ujasiri wa kuwachukulia hatua kali Viongozi wetu wanaposhindwa kutimiza matarajio yetu.

Sina maana kwamba tukalete vurugu, hapana, lakini inapobidi kuwahoji Viongozi wetu, basi tukafanye hivyo kwa nia njema ya kuliponya Taifa letu.
Maswali yafuatayo yanapaswa kuulizwa kwa Viongozi wetu wa ngazi mbalimbali, wakiwemo Wabunge na Madiwani.

(1) Kwa nini huduma za jamii(Elimu, Afya, Umeme, Maji, Miundombinu) ni duni wakati Tanzania ina utajiri wa rasilimali za kila aina?

(2)Kwa nini Maisha ya Watanzania ni duni katikati ya utajiri wa Nchi wa kiasi hicho?

Maswali haya ni mfano tu, kila mmoja anaweza kuongeza au kubadilisha maswali kulingana na changamoto za eneo analoishi.

Zamani nilidhani kuhoji Viongozi ni wajibu wa vyama vya siasa tu, lakini nimegundua kuwa huu ni wajibu wa Watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Mungu atupe ujasiri, hekima, akili, nguvu na maarifa ili tuweze kufanya Reformation katika Nchi hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom