Biashara ya Kimataifa
Mji ulistawi kwenye biashara kati ya pwani la Afrika Mashariki na Bara Arabu, Uhindi na hata Uchina. Kilwa ilikuwa kituo kwa ajili ya majahazi yaliyopita njiani. Miji yote ya Uswahilini ilinunua bidhaa kutoka Waarabu na Wahindi na kuuza pembe za ndovu, ganda la kobe na mazao pamoja na watumwa. Biashara kubwa ya Lamu ilikuwa miti aina ya mkoko yenye ubao usiooza rahisi hasa hauliwi na mchwa hivyo unafaa vizuri kwa ujenzi wa nyumba. Mikoko ilipatikana tele kwenye fungu-visiwa ya Lamu lakini siku hizi imepungua mno hivyo serikali imepiga maarufu kuziuza nje.