KARIAKOO: Waziri Nape afanya ziara ya kushtukiza, aagiza duka kufungwa

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669

Waziri Nape Nnauye leo amefanya ziara ya ghafla katika jengo linalodaiwa kudurufu CD la Aguster Kariakoo jijini Dar.

Ameagiza duka hilo kufungwa

13669733_1163592207036299_4097990436294164006_n.jpg

Nape Nauye amefanya ziara katika mitaa inayohusika na uuzaji wa CD/ DVD maeneo ya Kariakoo na kubaini kiwanda bubu cha kudurufu Kazi za wasanii na kuinyima Serikali mapato pamoja na wasanii kukosa haki stahiki.
 
Japo nimeipenda hii lakini najiuliza tu...Kwa nini mpaka afanye yeye?

kwa mtazamo wangu hiyo ni kazi ndogo sana inayotakiwa kufanywa na watu wa chinichini sana. sasa wanalipwa mshahara wa nini.

acha kamishna, hata mkurugenzi hawezi kufukuzana na wadurufu CD, ni kazi za watendaji wa chini, maafisaafisa tu.
 
Sawa.Nguvu hiyo itumike kujenga au kukarabati viwanja vya michezo.
 
Japo nimeipenda hii lakini najiuliza tu...Kwa nini mpaka afanye yeye?

kwa mtazamo wangu hiyo ni kazi ndogo sana inayotakiwa kufanywa na watu wa chinichini sana. sasa wanalipwa mshahara wa nini.

acha kamishna, hata mkurugenzi hawezi kufukuzana na wadurufu CD, ni kazi za watendaji wa chini, maafisaafisa tu.

Nadhani ungejiuliza ni kwa nini hao wa chini hawajafanya mpaka yeye akaenda.
 
Wonders shall never end. Kama kuna ushahidi kwa nini mtuhumiwa asifikishwe kwenye vyombo vya sheria. Je kufungwa kwa hilo duka ndio suluhisho vp kama hiyo mitambo ya kudurufu itahamishiwa duka jingine? Ooh!Sorry nilipitiwa kumbe hii ni serikali ya mwendokasi kufukuza na kufungiwa ndio mtindo wa kisasa mahakamani baadae sana...
 
Huu utoto haujaisha tu?
Inamaana huyo Agusta anauza hizo CD peke yake nchi nzima?
 
Nampongeza Magufuli kwa kututeulia viongozi vijana jijini Dar, yaani kiongozi akizubaa tu anafunikwa na kusahaulika.JJM hapo Kibamba ashasahaulika wadau wanaanza kucheza muziki wa Slowslow
 
Back
Top Bottom