Rais Samia afanya ziara ya kushtukiza Kariakoo, Mbagala na Mwananyamala Jijini Dar

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kustukiza katika soko la Kariakoo Dar es Salaam na kuongea na wafanyabisahara wa maeneo hayo

KARIAKOO

Rais Samia Suluhu amewatembelea na kuwasikiliza wanyabiashara wanaofanya biashara ndani ya soko la Kariakoo, baada ya matembezi Rais Samia alizungumza nao wote kwa pamoja.

Rais Samia: Nimeona nije nione mahali ambapo watanzania wengi wanafanya biashara, nimesikia baadhi ya malalamiko kwahiyo nikaona nije nione mlipo na mnavyofanya biashara zenu.

Nimefanya mahojiano na wachache ndani kati yenu lakini yamenipa sura ya soko linavyoendeshwa na sijui kama viongozi wa soko wako hapa.

Katika ziara yangu nimeona Serikali tusaidia kusimamia kufanya tathmini ya uendeshaji wa soko lote kwasababu hali niliyoiona ndani na hata nje kwenye vibanda hairidhishi.

Serikali pia kuanzia wakati mpendwa wetu Magufuli yupo hadi leo, nia yetu ni kusaidia wafanyabiashara wadogo wadogo. Naona usadizi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo haupo ila kuna kutengeneza faida kwa uongozi wa soko au kwa shirika labda.

Jingine, nimeangalia bidhaa zilizomo ndani ni vurugu mechi, huoni bidhaa gani iko wapi, unakuta muuza vyerehani yupo katikati ya muuza madawa ya kilimo na dawa za panya na mambo mengine.

Wakati tunafanya tathmini ya soko, nimuagize na naambiwa waziri wa Tamisemi alitoa hayo maagizo, kusimamisha uongozi uliopo na tuwatake vyombo vya serikali vifanye uchunguzi kwanza halafu tutakuja kutoa maamuzi.

Kwa wakati huu naomba muendelee na biashara zenu kwa salama bila vurugu, serikali iko pamoja nanyi lakini na nyie ndugu zangu, wakati serikali inawabeba, wanasema bebweo hujikaza.

Wakati Serikali inawabeba nanyi jitahidini kufuata sheria zinazowekwa katika maeneo mlipo kwasababu nimeona njia zote zimezingirwa, vibanda kila pahali.

Kwahiyo nitakaa na uongozi wa Jiji nione njia nzuri ya kuwapanga na njia nzuri ya kugawa maeneo ya kufanyia kazi.

 
tunamuomba pia afanye ziara stendi kuu ya mabasi ya Magufuli, maaana hapo pia ndio chanzo cha uchumi wa JiJi na Tz kwa ujumla.

Stendi ya kimataifa ya mabasi ya magufuli ni chanzo kikubwa cha uchumi wa Tanzania endapo tu, kutakuwa na uongozi imara.
tusisubiri watu waibe weee kisha badae aje CAG achunguze halafu ndipo tuchukue hatua, hii sio sawa kwa viongozi tuliowapa dhamana ya kusimamia.

, kwa nn mnasubiri wizi utokee halafu badae ndio tunachukua hatua! kwa nn tusichukue hatua mapema?
waswahili wanasema usipo ziba ufa utajenga ukuta mzima.
 
Back
Top Bottom