Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Rufaa Morogoro

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,735
22,433
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.

Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.

Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).

Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.
kigwa-2.jpg
 
Hizi ziara za kustukiza katika hospitali na vituo vya Afya na kuanza kushangaa kwamba hospitali haina hiki, haina kile, majengo yamechakaa, sijui kama inaangalia pia upande wa resources. Je sehemu hizo zinazotembelewa zilipata resources za kuwezesha hayo mambo kufanyika?

Pamekuwepo kilio kwamba fedha za budget kwenye wizara mbali mbali kwa mika kadhaa zimekuwa zikipatikana kwa chini ya asilimia 35.

Nafikiri badala ya kuwalaumu viongozi wa taasisi hizo ni vyema pia akatumia muda huu kuona walipokea shilingi ngapi na walifanya nazo nini?
 
Mkuu kabla ya kuvamia mahali
Wamesha fanya utafiti wavamizi wanajuwa kila kitu kuhusu Hospital au office.
Hawakurupuki tu
 
HIVI HAWANA UBUNIFU WA NJIA NYINGINE YA KUWAWAJIBISHA MPAKA ZIARA ZA KUSHTUKIZA? hATA UKISHTUKIZWA NYMBANI LAZIMA MAPUNGUFU YATAONEKANA!
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.

Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.

Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).

Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.View attachment 323873
sijui nani atajitolea kumwambia mkuu raia wenye wagonjwa huwa tunafulishwa shuka za hospitali hapo alipotembelea.
 
Sasa kama zinasimamiwa na TAMISEMI yeye kilichompeleka ni nini ?
 
Wanazogawana.

Mtani kuna mahali sielewi,hivi hospitali hizi pesa hii kubwa inapatikana wapi??Hata kama wanakula siyo nyingi kiasi hicho.BAdo waziri walitakiwa kutafuta mbinu ya hospitali hizi kupata mashine za kisasa
 
Dr. Kigwangala aliwahi kusema kwenye mdahalo mwaka jana kwamba hakuwahi kuona wagonjwa wanaolala chini katika hospitali ya Muhimbili! Kweli Mungu ni mkubwa. Sasa amepelekwa Wizara ya Afya ili ajionee mwenyewe.
 
Back
Top Bottom