Kariakoo tuwaache wachina watufundishe biashara

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,247
Reaction score
16,169
Watu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu na waendelee kutoa huduma mbaya kwa wateja

TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu Moja vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.

Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.

Unapochangamana na mchina au mgeni tumia hiyo fursa kuuliza na kujifunza badala ya kumchukia na kulalamika na kukodoa macho kodo eti aondoke ili wewe uendelee na uvivu wako na lugha mbaya yako kwa wateja; koma kabisa.

Kondacta wa daladala anawasokomeza watu kwenye daladala huku akiwaambia kama hutaki piga chini, daladala halijai kama ndoo ya maji huku akipita katikati yao kuwapanga na kukusanya nauli na nguo zake chafu. Vipi kama akija kondacta mchina na madaladala yake akaja na level seat akiwa amevalia suluali nyeusi na shati jeupe la mikono mirefu na tai yake shingoni?
 
Watu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wakiwa na wadogo wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu.

TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.

Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.
Ni kwel hii dunia ni ya ushindani acha tupigane spana na wachina watufundishe biashara
 
Ni kwel bhana mbongo analidhika sana, my ex yf pind mjamzto tukaenda kununua vitenge maandaliz ya kujifungulia.
Kuna duka tuliingia mdada anachat amekaa tena anajibu inshort, hata kumsikia gud hamna.
Nikaludia kumuulza koz ckuckia gud 'umesem sh ngap dada?" akawa kimya.
Hatukuendlea kuchagua na mke wang tukahama duka jirani c pesa ya kwetu bhana afu analeta nyodo kweny tonge
 
Watu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu na waendelee kutoa huduma mbaya kwa wateja

TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu Moja vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.

Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.
Kariakoo wafanyabiashara wakubwa sio wachina ni wazawa ila tu mnadanganyana tu humu. Wachina wamezidi tu kidogo wafanyabiashara wa kati wa kawaida ila hakuna wachina level za Kina Gsm, Metl, Bakhresa na wengineo kwa sasa. Bado biashara kubwa kubwa ni za watanzania. Ushamba wetu tu kuwatukuza.
 
Ni kwel bhana mbongo analidhika sana, my ex yf pind mjamzto tukaenda kununua vitenge maandaliz ya kujifungulia.
Kuna duka tuliingia mdada anachat amekaa tena anajibu inshort, hata kumsikia gud hamna.
Nikaludia kumuulza koz ckuckia gud 'umesem sh ngap dada?" akawa kimya.
Hatukuendlea kuchagua na mke wang tukahama duka jirani c pesa ya kwetu bhana afu analeta nyodo kweny tonge
Wacha washindane na wageni watajifunza maana ya mteja na namna ya kuuzia watu bidhaa. Kama mchina anachoma mahindi vizuri bila ya kuyababua na moto, akayanyunyizia tangawizi na vanilla na kunikaribisha kwa bashasha na heshima kwanini aambiwe aondoke ili auze mswahili anaechoma kwa kuyaungaza huku anachat bila kujali mteja wake? Kwanini mhindi ukifika dukani kwake anakwambia karibu dugu yangu anunue kitu giniani bhana!!
 
Watu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu na waendelee kutoa huduma mbaya kwa wateja

TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu Moja vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.

Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.
Nakubali kwa kweli maana Wakinga na Wapemba wamezidi ushirikina na hawana ubunifu wowote zaidi ya kufuga majini na kurogana tu.
 
Umitashumta kaletwa HUSSEIN BOLT kubabake
Umitashumta hiyohiyo mbona wakinga wanatoboa?, kule kwetu Tanga ukitumwa dukani lazima uende na shilingi Moja ya kugongea dirisha la dukani kumuita muuzaji aje akuuzie, maana hakai dukani lazima aitwe na mteja. Unagonga na kuita duuukaniiii, maduka wanafungua saa 3 asubuhi na kufunga saa 2 usiku.
 
Wachina washikilie hapo hapo
TRA kusanyeni kodi yenu mengine tuachieni sisi wateja tuchague nani anihudumie. Ukweli tumechoka kununua bidhaa zenye mavumbi kutoka kwa wauzaji walionuna na wasiomjali mnunuzi. Wazawa hawatoi risiti, Bei kubwa na wanakwepa kodi pia. Tuwaache washindane kama vile akina Ibrahim Bacca, Job, Mzize, Kapombe, Shabalala na suleman mwalimu wanavyoshindana kupata namba katikati ya wachezaji wageni.
 
Nakubali kwa kweli maana Wakinga na Wapemba wamezidi ushirikina na hawana ubunifu wowote zaidi ya kufuga majini na kurogana tu.
Hiyo sio kweli, nenda kamchunguze mkinga uone anaamka saa ngapi kufungua biashara na anafunga saa ngapi na anawahudumiaje wateja wake. Chunguza matumizi yake na anakula nini na kiasi gani kwa siku. Mchunguze uone kama ana roho nzuri ya kusaidia ndugu zake na kunywa pombe na starehe nyingine za wanawake, chunguza kama anafiwa uone kama anafiwa na kuhudhuria misiba Kila siku, nenda kaone namna anavyoongea na mteja wake na usafi wa bidhaa yake, hakuna uchawi kaka anajilipua TU na kufuata misingi ya biashara. Wewe Kila siku uko kipalang'anda kuzika mjomba mara kaka yake mdogo mkazamjomba mara rafiki yake wa utotoni mdogo wake bibi Yako.

Biashara ni mapato na matumizi
 
huo muda wa kumchunguza mkinga we uliupataje?.
 
Back
Top Bottom