Kariakoo siyo waaminifu kwenye biashara ya simu

Kariakoo siyo waaminifu kwenye biashara ya simu

Ukinunua simu ya samsung kariakoo kwanza wapige biti kali cha pili ipeleke samsung waicheki then mkihakikisha ni og ndio mlipane
...................Na kwanini uhangaike kununua kwa mtu mwenye uko na shaka naye kisha tena uipeleke Samsung wakaihakikishe wakati wenyewe Samsung wanazo simu wanazouza?
 
Kuna Jamaa alinunua sumsung feki mtaa wa aggrey , phone memory ilionyesha 64 Gb , kwenda nayo home na kuichunguza fresh phone memory hamna kitu mpaka uweke external memory . ilikuja kumfia.
 
Kkoo ukitaka simu OG nunua
TECNO,ITEL,INFINIX,OPPA,VIVO n.k

Ukigusa SAMSUNG, IPHONE,SONY,NOKIA andika maumivu
Kuna siku nimekaribia kulizwa mchana mchana. Hot9 inauzwa 280 ila jamaa anauza 200, A20 ni 300+ jamaa anauza 220. Ni kutokuwa na pesa mkononi kulinisaidia sana otherwise ningeuziwa famba
 
Nilinunua samsung s6 mhhhhhh nilipofika home nikaichunguza nikajua nimepigwa nikaiuza siku hio hio sasa hv niko na vivo no stress warranty miaka 2 sijajutuia kuhamia vivo
 
Hata wahindi ni wezi hapo kariakoo, niliwahi kununua tablet hapo kariakoo duka la muhindi alinipa nikaikagua fresh ile anairudisha kwenye box kumbe ipo mbovu imetegeshwa chini ya droo then nikaomba risiti akaiandika wakati nahesabu pesa tablet ikabadilishwa nikatoka nje nikahakiki jina la duka kama linaendana na jina la kwenye risiti nilivyoridhika nikasepa, nafika home chomeka charge kuanzia saa mbili hadi saa kumi chrge hata asilimia moja hakuna na ukibadili charger ni hivyohvyo.

Dah nikasema nikienda polisi gharama zitaongezeka na pia kesho yake nilitakiwa kusafiri kwenda kusimamia mavuno ya mashamba yangu ya viazi huko njombe, so nikaongea na bodaboda mmoja hv mrefu mweusi kama wakurya nikampa mchongo ajifanye askari amkazie muhindi arudishe pesa, jamaa akashauri twende stationery tuprint risiti nyingine then bei tuzidishe mara mbili kwa makubaliano kwamba pesa itayozidi tugawane pasu nikasema fresh, time print risit mpya tukafika dukani kwa muhindi ndo wapo ktk mishe za kufunga jamaa akajitambulisha kwamba ni askar na mm ni mteja nilinunua tablet na nimeuziwa tablet feki kwa hyo funga duka tuelekee kituoni.

Muhindi akaomba tumuoneshe tablet tukampa chomeka kwenye charge haipeleki wakapiga simu mwenzao akaja ongea kihindi hapo mwisho wakaomba watupe nyingine tukagoma tukawaambia war u Di she pesa wakakubali wakasema niwape risiti waliyoiandikia wakachukua na kuhesabu pesa chapchap bila kujua kwamba ile bei original wahuni tulishadouble nikamwambia umenipa pesa nusu, akasema ndio tulioiandika kwenye risiti, yule askari akaomba risiti akasema mteja yuko sahihi mlipeni pesa yote, mhindi kuangalia risti kitu kpo doubled na askar npo naye ilibidi awe mpole akajua sasa kaingia choo cha chekechea, alitoa mpunga bila kubisha then tukasepa, tukaifuata bodaboda tuliipak pale msimbazi petrol station jamaa akala chake na mm nikaenda zangu mwenge kujipongeza naka drostidy ka bariiidii.
 
Nakazia Tena watanzania acheni ujinga.


Ukienda kariakoo nenda kwa ajili ya kununua Tecno, Itel, Infinix, oppo, vivo n.k

Ila ukijichanganya kununua Samsung, iPhone, Sony, Nokia n.k lazima upigwe. Narudia tena lazima upigwe. Otherwise ukanunue simu kwa wahindi au waarabu. Wabantu Wenzetu ni takataka hawana uaminifu kabisa.


Kazi yetu tumeshamaliza kuwapa tahadhari tusisikie vilio tena humu ndani.



Usimuamini mtanzania mweusi (mbantu) akuuzoe simu pale kariakoo utalia. Wahindi hata akikuuzia simu feki ni waoga Sana kwenda polisi au ukimtishia suala la uhamiaji anaogopa. Ila hawa wabantu Wenzetu utajua.


Nendeni mkanunue vitu kwa wahindi.


Tumemaliza.
Mkuu hata hizo akina tecno & infinix feki zimejaa kibao pale mtaa wa Aggrey ukiingia kichwa kichwa napo unapigwa vizuri tuu. Nimezishuhudia tecno & infinix fake pale mtaa wa Aggrey kwa macho yangu nikabaki nacheka tuu.

Sasa sijui hizi mamlaka zetu za ukaguzi wa ubora wa bidhaa zinafanya kazi gani au wakisha kula kodi yao tuu ndo basi. Polisi nako watakuzingusha mpk ukome na watakuita mzembe.
 
Wakuu habarini za asubuhi.

Katika biashara uaminifu ni kitu kikubwa sana kwenye biashara bila uaminifu hata wateja watakukimbia.

Watanzania hasa wafanyabiashara wa kariakoo hasa hawa wanauza simu wengi ni matepeli na wezi kibao, kuna hawa wanaotengeneza simu na kuuza simu wengi ni wezi na matepeli.

Biashara ya simu inalipa sana na mtu anatumia gharama kubwa kununua simu nzuri akiamini hapa nimepata simu kumbe wizi na utapeli mtupu.

Wafanyabiashara wa kariakoo mbadilike tutafikishana pabaya maana tukiwapeleka polisi huko nako ni danadana ,sasa endeleeni kutuibia na mtambue kuna njia nyingine tunaweza kutumia na hata hiyo biashara usikitamani tena na mwisho ikawa vibaya kwako.

Wanaumizwa ni watanzania ,na sisi sote ni watanzania.

Kuanzia leo nawashauri wanunuzi wa simu ya kutumia kwa matumizi yako binafsi kanunue simu kwa wahindi au nenda mlimani city hawa wabongo ni wapumbavu tu.

Nimemaliza.



Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Pole sana aisee, mi sijawahi kuuziwa simu fake Kariakoo. Ni bora kabla hujalipa ukaomba IMEI number ukaitest kny website ya imei.info
 
Kikukweli inaboa
Na rafk yangu nmesoma nae msing ni fund simu pale nilmpelekea Galaxy j7 anibdlshie kioo akadai kioo kizur (0rg) n Tshs 100,000

Nkampa lak moja aka fix kioo (Samsung wenyew iko kioo wanauza 135000/-

Bwana wew jamaa akalalamika ajabakiw hata na mia kumbe ni utapeli tuu nimetumia simu miez 3 kioo kimepga mistar na giza hakionyeshi (nazn alinunua Cha 25000 au 35000)

Dah asee nmefata namkazia Bado anasem kioo chenyew na anatak kuniuzia kioo kngen 70,000 nikateman nae

Kinachonikera nilmpelekea yey nkzan atakuw mwaminfu
Mkuu nikuuzie kioo cha J7 original kabisa sio kipya ila ni simu ambayo nilikuwa naitumia nimenunua nyingine. Ni original mkataba kabisa
 
Back
Top Bottom