Kariakoo hawataki kutoa risiti kamili

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,585
14,045
TRA njoni kariakoo mjionee wenyewe namna wafanyabiashara wanavyokuwa wasumbufu kutoa risiti kwa wateja wao. Unanunua bidhaa za 1 milioni wanatoa risiti ya ya laki mbili. Ukikomaa kudai risiti kamili sawa na pesa ulizowapa wanarudisha bidhaa walizokuuzia. Utabisha hapooooeeee mpaka ama unachukua risiti pungufu ya electronic au unaacha bidhaa zote ulizonunua na kurejeshewa hela zako. Nadhani hali sio shwali. Nilipotaka kujua kwanini hivyo wanasema waagiza mizigo nje ya nchi nao hawatoi risiti kwao pia. Nina uhakika kuwa watumishi tu ndio wanaolipa kodi halisi nchi hii.
 
Acha kuwachomea wenzio jombaaaa!
Biashara yenywe ngumu kweli sasa hivi!
Nahitaji huduma ziwepo hospitali, maji, barabara, nk. unaosema ww ni u..pu.u.z sawa na upuuu....z mwingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom