getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Awali napenda kuishukuru serikali kwa kuweka wapelelezi wao kwenye maduka kariakoo.
ili kuwabaini watu wasiotoa risiti za EFD. Na wale wanao ondoka bila risiti baada ya kununua bidhaa zao hili ni jambo jema, Lakini ukwepaji kodi mkubwa karikakoo hauko katika kutokutoa risiti za EFD tu..
ukwepaji unafanyika kwa kutoa risiti yenye thamani pungufu kwa mzigo ulionunuliwa mfano umenunua mzigo wenye thamani ya tsh 600,000 au Tsh 1,000,000 muuzaji atatoa risiti ya tsh 2,00,000 au hata Tsh150,000 ukiuliza anakujibu brother hiyo si ya njiani tu?
Ukikomaa kutaka risiti kamili unakuwa umetengeneza uadui kesho ukija inakuwa ngumu sana kuhudumiwa kwenye duka hilo..!!
Ushauri wangu,
TRA waendelee na hiyo system ya kuvizia kwenye maduka lakini awamu hii wakamate wanunuzi waulize bei ya mizigo waliyonunua kisha waangalie risiti walizo nazo kama zina thamani ya mzigo iliyobebwa.! Wapige thamani ya mzigo na risiti walizo nazo..!
wakifanya hivi kwa mwezi mmoja naamini kila mnunuzi atakuwa makini.
mwisho watu wao wanaowaweka sokoni kariakoo wanatambulika na wafanyabiashara wenye maduka kuwa ni watumishi wa TRA hivyo ni vema ama wakawa wakibadirisha mara kwa mara.
nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app