Karejea upyaaa, wazee chadema na viongozi wakubali kufukia mabonde ya kijana wao

duh mie niliwahi kumuamini sana zito, ila alinichanganya sana, mpaka sasa simuamini kama ni kweli au vipi,
isije kuwa mpango wa ccm unaelekea kukwama so anarudi ili cdm wamuamini tena then majority wakishamuunga mkono , pengine karibia na uchaguzi aanzishe ujinga mwingine.

achukuliwe kwa tahadhari sana tusimuamini kwa kasi
 
Watu walidhani kuwa tulikuwa tukimchukia Zitto kama Zitto, but leo nimerealize kuwa watu wengi tulikuwa tukiyachukia matendo ya Zitto kwa sababu kutokana na umuhimu wake ndani ya chama, alikuwa anaelekea kukibomoa CDM vipande vipande kitu ambacho wengi hatupendi kukiona kwa sasa. Leo hiii kama kweli Zitto ameerudi kwenye mstari, wengi tumefurahi huku tukiwa na imani kuwa sasa CDM inavuta vihunzi vingine ambavyo wapinzania wa ndani na nje ya chama walidhani kuwa hatutaweza. BIG UP BROTHER ZITTO, KEEP IT UP.
 

probably the guy had no choice. aliambiwa afanye hivyo. yeye si wa kwanza, tunakumbuka nyerere alishawahi kumwambia Aboud Jumbe "you have to step down" historia hujirudia. hivi nilazima zitto uwe hapo chadema? unaelimu kwa nini unyanyasike kwa ajili ya dini yako tu? ya kabila laku tu? ya ukanda wako tu? fikiria, chukua hatua.
 
bla bla bla bla bla bla blah

bla bla bla bla bla bla blah

bla bla bla bla bla bla blah

bla bla bla bla bla bla blah

bla bla bla bla bla bla blah

bla bla bla bla bla bla blah
 
Japo kuwa una dhambi nyekundu kama kaa la moto lakini ukitubu zambi roho yako inakuwa nyeupe kama sufi
 
Bado anayo nafasi hata isipokuwa 2015 kuna 2020 ambayo akitulia vyema inaweza kuwa upande wake ila yafaa atulize kichwa.

nikisoma maneno kama haya yaani mwili huwa unisisimka, sidhani kuwa rais wa Tanzania nayo ni nafasi ya kuzengewa zengewa hivi?

hiyo nafasi kwa mzalendo wa nchi hii ni nifasi ya kujitoa kafara, ni nafasi ya kujitoa mhanga tena ni nafasi ya kuhatarisha uhai wake.

Wote waliopitia hapa nchini na kuonja utamu wa nchi hii bado hajaondoa mikono yao humu; mwarabu,mzungu na hata wabantu tuliodhania ni wenzetu walipoonja tu wakatugeuka na kuanza kututafuna live. Sasa mzalendo anayeutaka urais wa nchi hii maana yake anajitangazia vita vya ndani na nje....
 

huyu nae wa wapi tena.nani kakwambia zitto ananyanyaswa chadema.mambo ya kabila,dini na ukanda yametokea wapi tena? Lione kubwa lakini Akili mgando.
 

We na wewe wa wapi,hujamckia zzk jana hotuba yake?aliyekwambia ananyanyaswa nani?,mbona mnapenda kuwawekea watu maneno mdomoni mwao?...haya tafuta thread ya zzk jana alipokuwa kigoma
 
Hakuna anayemchukia Zito CDM. Watu wananampenda Zito lakini baadhi ya vitendo vyake vinawapa mashaka watanzania wengi. Mimi mwenyewe nimekuwa mkosoaji wa Zito humu ndani. Si kwamba simpendi kwasababu ya dini yake wala kabila lake. Kwani dini na ukabila inahusiana vipi na uongozi kwenye chama.
Kitu ambacho Zito inatakiwa ajifunze ni kuwa chama lazima kiongozwe na watu iwe yeye au watu wengine. Hakuna haja kuleta mfarakano kwenye chama eti kwa kuwa hupendi jinsi chama kinavyoongozwa. Cha muhimu ni kutoa mapendekezo ya kurekebisha kwenye vikao vya chama. Si mapendekezo ya kukashifiana manake vyama vinaongozwa na watu ambao wana mitazamo yao na hawawezi kuvumulia kuvunjiwa heshima. Mnapovunjiana heshima viongozi mjue mnaivunjia heshima chama manake mkigawanyika chama kimegawanyika.
Hakuna chama kisichokuwa na matatizo yake. Lazima kuna kuanguka hapa na pale ambayo ikiwa si kuondoka kwenye malengo ya chama ya kukomboa watanzania kwenye utawala mbovu wa ccm watu wanasonga mbele. Kuna makosa ambayo hayawezi kuvumiliwa kwenye chama lakini vingi ambavyo ni msuguano mdogo upo kila sehemu na hayawezi kukosa hata wakishika serikali au sehemu yoyote ya kazi ambako kuna mchanganyiko wa watu wengi.
Masuala kama yale ya Juliana Shonza ni mambo madogo sana ambayo hayawezi kuondoa watu kwenye mstari wa kujenga chama. Issue kwamba nani anapewa nafasi kubwa kusimamia m4c, nani anatembelea majimbo haya ni mambo madogo tu. Hata kazini bosi wako akikuona hauko imara hawezi kumnyima mtu anayemuona anafaa zaidi kuwa supervisor kumsaidia kwa urahisi. Hata kule kujiona unajua kila kitu kunaweza kuwa kikwazo kikubwa kwako kutimiza majukumu yanayokutaka ushirikiane na watu wengine.
Waislamu wanaofikiri wanabaguliwa CDM kwa kuwa hawajaingia huko wamekunywa tu propaganda za watu wasioitakia CDM na nchi nzima kwa ujumla mema. CDM ina hamu ya kuunganisha wananchi wote bila kujali dini au ukabila wa mtu. Lakini watu wa ccm wanajua CDM kuunganisha wananchi wote ni hatari kwao hivyo wanajenga propaganda hizo ili muogope na waendelee kutawala. Bila kujua mnacheza wimbo wao huku mustakabali wa nchi ukuzidi kufunikwa na giza.
 
Habari hii inatia matumaini. Chadema inahitaji kuwa kitu kimoja kuelekea 2015. Wapenda mabadiliko wote watakuwa wamefarijika na habari hii.
 
Kunakipindi hii single Zitto mwenyewe alikuwa anaiimba sana lakini yeye anasema umri umefika na ameaumua sasa kutoil nakurudi nyuma kwa ajili ya chama manake kesha ona hiyo single haiuuzi anajiunga nawenziwe kwenye M4C sasa tuache sisi tujiridhishe kama kweli amerudi
 
Kurudisha majeshi nyuma si kushindwa mapambano.Jamaa anajipanga kwa awamu nyingine ya mpambano.Haaminiki hata kidogo. Hata masalia walimwamini kwamba atakuwa nao kwa hali zote,lakini mwisho wa siku .... Huyu ni opportunist mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…