Kardinali Pengo: Tumuombee Rais Magufuli

Kardinali Pengo: Tumuombee Rais Magufuli

Ikitokea Mungu akaifuta Afrika kwenye uso wa dunia itakuwa ushindi mkubwa sana duniani.
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Watanzania kuzidi kumuombea Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya. Kardinali Pengo alisema hayo alipokutana na waandishi wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema mambo anayoyafanya sasa Rais Magufuli yana manufaa makubwa kwa Watanzania na kusisitiza kwamba ni viongozi wachache duniani wenye ujasiri wa kufanya hivyo. Kardinali alisema kutokana na kutumbuliwa majipu kwa watu ambao walikuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya Watanzania, kiwango cha ubinafsi kinaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.

Alitoa rai kwa Watanzania kuwaombea viongozi wa nchi ili waimarishwe katika kuleta maendeleo ya taifa. “Tunahitaji kuiombea Serikali na tuiweke mikononi mwa Mwenyezi ili viongozi wake waimarike katika kuleta maendeleo kwa taifa letu,” alisema Kardinali Pengo.

Katika mkutano huo, Kardinali alitangaza Parokia teule sita kuwa Parokia kamili, ikiwemo ya Kijitonyama iliyokuwa ni Kigango cha Parokia ya Mwananyamala, hivyo kufanya parokia za Jimbo Kuu Dar es Salaam kufikia 95.

Mbali na Kijitonyama, nyingine ni Mtakatifu Rita Temboni, Msakuzi, Mbande, Mshikamano na Michungwani iliyoko Kimara. Mapema mwaka jana, alipokutana na Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo alisema anamwomba Mungu amwezeshe kusimika parokia 100 za jimbo lake katika uhai wake. Kwa sasa zipo parokia teule nyingine sita ambapo zikikamilisha mahitaji yote, zinaweza kutangazwa parokia kamili ndani ya mwaka huu.
tumwombee ili atubu
 
Acheni kufukua makaburi..hii kauli aliitoa siku nyingi kabla ya kutenda dhambi
 
Pengo analeta siasa pia, kwa akili chafu za JPM, Kesho kilaini akiponda serikali, anaamini anaweza kulifuta kanisa katoliki.

[HASHTAG]#MagufuliSioMungu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Katubu[/HASHTAG]
 
“Muendelee kuniombea ili cheo changu cha Urais kikajenge umoja wa Tanzania, mniombee ili nisiwe na kiburi kwa kutumia cheo changu cha urais, mniombee niwe mtumishi wenu ndugu zangu watanzania- @MagufuliJP
 
Siongezi neno! Kama kuna mtu namdai nilipe nisepe! Hivi kuna watu binafsi wanafanyaga maombi hayo zaidi ya kkt na rc,maana ipo kwa lazima!
 
Mtu kutekeleza majukumu ya kazi yake kikatiba hahitaji kuombewa. Kwa watu wa dini wanasema unaomba mungu (kama yupo) akusaidie kutatua jambo gumu usiloliweza sasa kama mtu anajua urais ni mgumu hadi ahitaji mambi hakua na haja ya kuuomba.

Hii n8 serikali ya ajabu sana inayohitaji maombi kwa kila inachokifanya, kwa hiyo bila maombi hawezi kutekeleza majukumu yake?

Maombi yataleta viwanda? Maombi yatatoa mil 50 kila kijiji? Maombi yatapeleka meli kila ziwa? Maombi yataleta kilimo cha umwagiliaji wa mibuyu? Maombi yataleta barabara ya njia sita toka chalinze au mambi yataleta elimu bure?

Serikali ya maombi.
Maombi ili mafisadi msimdhuru kipenzi cha watanzania.
 
Watanzania wote bila ya kujali itikadi zetu tumuombee Rais Magufuli kwani anayo nia ya dhati ya kulivusha taifa letu..

Wanaomdhihaki ni mafisadi...
Hatimaye leo Mungu amejibu maombi yetu.

Hujui tu tulikuwa tunaomba nini.
 
Back
Top Bottom