Kardinali Pengo: Tumuombee Rais Magufuli

Kardinali Pengo: Tumuombee Rais Magufuli

Sisi wenyewe tuna matatizo kibao tunaomba wenyewe sasa tutaanzanze kumwombea mwingine wakati wenyewe tunapigika? Kila mtu aombe mwenyewe. Kwani yeye hakupata mafundisho na kupata kipaimara?
 
Tumuombee labda aweje. Tu be honest kama nikiamua kumuombea nitamuombea kwa mungu ampende zaidi ili ikiwezekana amchukue. Ila sina muda wa kumuombea mtu kama uyo wakati hata mimi nabidi nijiombee.
 
Hakuna sababu ya kutafiti kwa nini waumini na sadaka siku hizi vimepungua sana kanisani. Hata mahudhurio kwenye jumuia yamebaki ya kina mama na watoto.
 
hahahah.Yaani niache kumuombea Lisu .
yaani niache kumuombea mke wangu na mwanangu nimuombee nani?
 
Nilijua kasema leo ningemshushia tusi lenye upako
 
Tuanze kukuombea wewe kari dili nali ili upunguze bei ya sadaka na michango ya kwenye jumuiya inaongeza uccm ccm rohoni
 
Mtu kutekeleza majukumu ya kazi yake kikatiba hahitaji kuombewa. Kwa watu wa dini wanasema unaomba mungu (kama yupo) akusaidie kutatua jambo gumu usiloliweza sasa kama mtu anajua urais ni mgumu hadi ahitaji mambi hakua na haja ya kuuomba.

Hii n8 serikali ya ajabu sana inayohitaji maombi kwa kila inachokifanya, kwa hiyo bila maombi hawezi kutekeleza majukumu yake?

Maombi yataleta viwanda? Maombi yatatoa mil 50 kila kijiji? Maombi yatapeleka meli kila ziwa? Maombi yataleta kilimo cha umwagiliaji wa mibuyu? Maombi yataleta barabara ya njia sita toka chalinze au mambi yataleta elimu bure?

Serikali ya maombi.
Asante kwa maoni yako.
Sie tunamuombea kila siku
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Watanzania kuzidi kumuombea Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya. Kardinali Pengo alisema hayo alipokutana na waandishi wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema mambo anayoyafanya sasa Rais Magufuli yana manufaa makubwa kwa Watanzania na kusisitiza kwamba ni viongozi wachache duniani wenye ujasiri wa kufanya hivyo. Kardinali alisema kutokana na kutumbuliwa majipu kwa watu ambao walikuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya Watanzania, kiwango cha ubinafsi kinaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.

Alitoa rai kwa Watanzania kuwaombea viongozi wa nchi ili waimarishwe katika kuleta maendeleo ya taifa. “Tunahitaji kuiombea Serikali na tuiweke mikononi mwa Mwenyezi ili viongozi wake waimarike katika kuleta maendeleo kwa taifa letu,” alisema Kardinali Pengo.

Katika mkutano huo, Kardinali alitangaza Parokia teule sita kuwa Parokia kamili, ikiwemo ya Kijitonyama iliyokuwa ni Kigango cha Parokia ya Mwananyamala, hivyo kufanya parokia za Jimbo Kuu Dar es Salaam kufikia 95.

Mbali na Kijitonyama, nyingine ni Mtakatifu Rita Temboni, Msakuzi, Mbande, Mshikamano na Michungwani iliyoko Kimara. Mapema mwaka jana, alipokutana na Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo alisema anamwomba Mungu amwezeshe kusimika parokia 100 za jimbo lake katika uhai wake. Kwa sasa zipo parokia teule nyingine sita ambapo zikikamilisha mahitaji yote, zinaweza kutangazwa parokia kamili ndani ya mwaka huu.
Pengo aache unafiki, Mimi no mkatoliki lakini huyu askofu amepungukiwa tunu ya kinabii ya kukemea maovu. Mbona hakemei ugaidi wa kiserikali, ukiukwaji wa haki za kiraia nk.
 
duh kauli ya huyu kiongozi wa dini ile yenye majina mengi ya watakatifu lina ukakasi sana.iko siku naye watu wasiojulikana watampitia.Sijamsikia akisema tumwombee Lissu apone haraka arudi kwenye majukumu yake
Acha zako mbona unaombea vitu vibaya wenzako.
Akitembelewa na wasiojulikana utapata faida gani?
 
Tafuteni kitabu cha how the church and government got the same bed hakika unafiki huu wa viongozi wetu wa didi umezidi,hv mbona wakati wa awamu ya nne ya mtoto wa mjini matamko yalikuwa mengi? Je matamko hayo kwa sasa yamepotelea wapi? Au kwa sababu ni wakwao? Hapa bila shaka pengo litaendelea wigo wa mapengo?
Achana na fikra potofu
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Watanzania kuzidi kumuombea Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya. Kardinali Pengo alisema hayo alipokutana na waandishi wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema mambo anayoyafanya sasa Rais Magufuli yana manufaa makubwa kwa Watanzania na kusisitiza kwamba ni viongozi wachache duniani wenye ujasiri wa kufanya hivyo. Kardinali alisema kutokana na kutumbuliwa majipu kwa watu ambao walikuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya Watanzania, kiwango cha ubinafsi kinaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.

Alitoa rai kwa Watanzania kuwaombea viongozi wa nchi ili waimarishwe katika kuleta maendeleo ya taifa. “Tunahitaji kuiombea Serikali na tuiweke mikononi mwa Mwenyezi ili viongozi wake waimarike katika kuleta maendeleo kwa taifa letu,” alisema Kardinali Pengo.

Katika mkutano huo, Kardinali alitangaza Parokia teule sita kuwa Parokia kamili, ikiwemo ya Kijitonyama iliyokuwa ni Kigango cha Parokia ya Mwananyamala, hivyo kufanya parokia za Jimbo Kuu Dar es Salaam kufikia 95.

Mbali na Kijitonyama, nyingine ni Mtakatifu Rita Temboni, Msakuzi, Mbande, Mshikamano na Michungwani iliyoko Kimara. Mapema mwaka jana, alipokutana na Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo alisema anamwomba Mungu amwezeshe kusimika parokia 100 za jimbo lake katika uhai wake. Kwa sasa zipo parokia teule nyingine sita ambapo zikikamilisha mahitaji yote, zinaweza kutangazwa parokia kamili ndani ya mwaka huu.
unafiki mtupu
 
Genocide ya Rwanda 1994 viongozi wa dini tena hii hii walihusika kwa maneno yao ya unafiki..
 
Back
Top Bottom