Karamagi achunguzwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Hiki ni kichekesho. Mtamchunguzaji waziri aliye bado kashikilia wadhifa wake. Anaweza kutumia kuwepo kwake pale wizarani kuvuruga ushahidi

Karamagi achunguzwa
SAKATA LA BUZWAGI

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima

WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni miongoni mwa vigogo wa serikali wanaochunguzwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).
Taarifa za kuchunguzwa kwa Waziri Karamagi aliyesaini mkataba wenye utata wa machimbo ya dhahabu, Buzwagi, zilifichuliwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Philip Marmo.

Bila ya kutaja jina la Waziri Karamagi aliyesaini mkataba huo wa Buzwagi Februari 17, mwaka jana, Marmo aliujumuisha mkataba wa machimbo ya dhahabu katika eneo hilo kuwa miongoni mwa mambo yanayochunguzwa na Takukuru.

Waziri Marmo, alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM) ambaye pamoja na mambo mengine, alitaka kujua dhamira ya serikali katika kukabiliana na tatizo la kukua kwa rushwa, ambalo sasa limesababisha imani ya wananchi kupungua.

Tamko hilo la kwanza kutolewa hadharani na serikali, tangu hoja ya mkataba huo ilipohitimishwa kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa miezi mitano, linaweza kuibua ukinzani mkubwa wa hoja miongoni mwa wadadisi wa mambo.

Aidha, taarifa kwamba mkataba wa Buzwagi unachunguzwa na Takukuru, ni kielelezo kwamba, majibu yaliyotolewa na Waziri Karamagi wakati akijibu hoja binafsi ya Zitto Agosti 14 mwaka jana, kwamba mkataba huo ulikuwa hauna matatizo yoyote, hayakuiridhisha vya kutosha Takukuru au pengine serikali.

Kumbukumbu za 'Hansard' zinaonyesha kuwa, wakati akijibu hoja hiyo ya Zitto Agosti 14, mwaka jana, Karamagi alisema: "Kama nilivyolielezea Bunge lako tukufu wakati nahitimisha hoja ya makadirio ya matumizi ya wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Katika viambatanisho nilivyokupatia sasa hivi, vilevile nimeambatanisha na kauli yangu hii... Kwa kuwa maandalizi yote ya kusaini mkataba yalikamilika nikiwa ziara ndefu nchi za nje, niliona si busara kuhatarisha uwekezaji wa mradi huu, jambo ambalo lingeathiri maslahi ya taifa."

Siku hiyo, Karamagi alikwenda mbali zaidi kuhalalisha mradi huo kwa kusema, uamuzi wa kuingia mkataba huo ulihitajika kufanyika kabla ya Machi 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huo ingepotea.

Dk. Chegeni katika swali lake la jana, lililozaa majibu hayo ya Marmo, alisema suala la rushwa na ufisadi limechukua sura mpya siku za hivi karibuni, na kusababisha manung'uniko kwa jamii licha ya jitihada za kupambana nalo zinazoongozwa na taasisi hiyo nyeti.

Alisema, jitihada hizo hazijatoa dhamira thabiti ya kupigana kikamilifu na tatizo hilo, huku akihoji hatua zilizochukuliwa na serikali kutokana na kashfa za rushwa kubwa zinazohusisha taasisi kama Benki Kuu, mikataba ya madini na nishati.

Aidha, mbunge huyo alitaka kujua idadi ya watu waliofikishwa mbele ya vyombo vya sheria wakihusishwa na rushwa za aina hiyo.

Katika majibu yake, Marmo alisema licha ya baadhi ya wabunge wa upinzani kuibua tuhuma nzito za rushwa wakati wa kikao cha Bunge la bajeti mwaka jana, serikali tayari ilishaanza kuzishughulikia tuhuma hizo, hata kabla hazijatolewa na kambi ya upinzani.

Alizitaja baadhi ya tuhuma nzito ambazo Takukuru inazifanyia kazi kuwa, ni pamoja na mkataba wa ukaguzi wa hesabu za makampuni ya madini kati ya Alex Stewart Assayers na serikali.

Aliutaja mkataba mwingine unaochunguzwa na Takukuru kuwa ni ule wa uchimbaji wa dhahabu katika eneo la Buzwagi mkoani Shinyanga kati ya kampuni ya madini ya Barrick na serikali.

Mkataba mkubwa wa tatu unaochunguzwa na Takukuru, kwa mujibu wa Marmo, ni wa machimbo ya makaa ya mawe na mradi wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

"Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, inafanya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya Benki Kuu. Uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea," alisema na kuongeza kuwa, hadi hivi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kuhusu tuhuma hizo.

Kwa majibu hayo, Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (Chadema), alilazimika kusimama na kusema kuwa, kuna maelfu ya watu ambao leo hii wapo rumande wakisubiri kesi zao, huku upelelezi ukiwa haujakamilika.

"Kama wapo Watanzania ambao wameshafikishwa mahakamani na wapo rumande wakati upelelezi wa kesi zao haujakamilika, kwa nini hawa wakubwa wameachwa wapo nje wanatamalaki?" alihoji mbunge huyo aliyekuwa mstari wa mbele kuitolea kauli kashfa ya ufisadi ndani ya BoT.

Swali hilo la Slaa lilijibiwa na Waziri Marmo aliyesaidiwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Mary Nagu.

Dk. Nagu alisema serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa, upelelezi wa kesi unakamilishwa mapema ili watuhumiwa wasikae muda mrefu mahabusu.
 
PCCB ya Hosea haina uwezo wa kumchunguza Karamagi kule Buzwagi kama swala la wazi la Richmond wameshindwa na leo ukweli umesemwa .Nao ni watuhumiwa wa kupotosha kwa lengo la kufika ukweli .So ni mafisadi JK get another serious man to run PCCB not Hosea .
 
Viongozi wakuu wa PCCB,Polisi,Mahakama,Usalama wa Taifa Magereza,JWTZ n.k hawa huteuliwa na Rais kama walivyo mawaziri,naibu waziri na taasisi nyingine za serikali.Kwa kweli sina hakika kama wana ujasiri wa kuwachunguza,kuhukumu,kukamata hawa wateule wenzao kama wanavyofanya kwa raia.Kwa hiyo hilo la Karamagi kuchunguzwa ni usemi tu wa kisiasa ili wajilidhishe kwa wananchi.Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu..........!?PCCB tafuneni,maana mnayo meno 32
 
PCCB ya Hosea haina uwezo wa kumchunguza Karamagi kule Buzwagi kama swala la wazi la Richmond wameshindwa na leo ukweli umesemwa .Nao ni watuhumiwa wa kupotosha kwa lengo la kufika ukweli .So ni mafisadi JK get another serious man to run PCCB not Hosea .

exactly
 
Back
Top Bottom