Nimekuwa mfuatiliaji wa tamthilia nyingi zinazorushwa na Azam two.
Nawapongeza sana.
Kwa sasa pamoja na nyinginezo tamthilia iliyopo ni Kara Sevda.
Sielewi mapenzi ya kituruki kwa mwanamke wa ndoa mara kadhaa kumtamkia mumewe kwamba hampendi na hapohapo ana mwanamme mwingine na mume anamjua. Na muda mwingi ni kulialia.
Kwa sisi waswahili kuna mapenzi kama hayo?
Kuna cha kujifunza?