Dah! Mkuu Safari_ni_Safari umenikumbusha siku moja niliona kitu kama hiki.
Mwizi alikuwa anakimbizwa mjini Dar maeneo ya Jamhuri, tatizo waliokuwa wanamkimbiza walikuwa hawapigi kelele za mwizi huyo!! Jamaa akakimbia na kuingia ndani ya kituo cha polisi mojakwamoja.
Polisi wakashangaa wakamuuliza vipi mbona unaingia kwa ghafla hivyo? ... yeye akawaomba wamuokoe maana kuna mtu kamuibia sasa kundi la watu wanamkimbiza kimya kimya kwa sababu wanataka kumuua wakati yeye kawaibia tu. Akawa analalamika akawaambia polisi toka lini umeona watu wanafukuza mwizi hawapigi kelele za Mwizi huyo! ... hawa wanataka kuniua!