Uko sawa kabisa mkuu, sisi jamii ya waafrica hatuna heshima kabisa na miili ya wenzetu waliotangulia mbele ya haki. Sio vizuri kucukua picha za marehemu na kuzisambaza kwenye mablogu, hasa kwa dini ya wenzetu waislamu. Hebu cheki sasa mambo yote hadharani haa watoto wadogo wanajua ni nini kinafanyika. Tuangalia tusijekuwa watumwa wa tekonolojia.
Mimi huwa najiuliza, how comes mtu unachukua mkanda wa video kwenye mazishi, kuanzia marehemu akiwa kwenye jokofu, anavyosafishwa, valishwa na kisha akiwa kwenye jeneza. What for? hivi mtu ukiangalia mkanda kama huu si ndio kujiongezea machungu?
Africa tujirekebishe kwenye hili na kupunguza mbwe mbwe misibani.