kanusho la dk.Mengi kwa prof Muhongo.

deecharity

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
893
500
1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.

2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha
kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:

“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”

4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.

5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.

8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.

Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
sasa tumuamini nani? yan anamiliki eneo ata km 1 ahifiki harafu muhongo aseme eneo analomilik ukubwa wa Dar mara 3.

Namshauri prof Muhongo wachukue eneo ilo kama ni kweli harafu tuone kama atalalamika
 
BABU CHONDO

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
858
195
Ameanza kukwepa,hiyo mijihela inayotakiwa kwa uwekezaji isiwe ya kukopa awe nayo bank,achanganye mpaka za radio one
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,550
2,000
Hivi hawa tuliowapa dhamana ya kuzisimamia rasilimali zetu wana nini na wazawa ambao ndo waliowaweka madarakani?
Kwa Muhongo kumshambulia Mengi kwa namna yoyote ile haikubaliki na ni kutokuwa mzalendo.
Hata kama Mengi angemiliki mererani yote kwangu mie ni sahihi kwani ni wa hapa. Anataka kutuambia kuwa wageni ndo wenye ruhusa ya kufanya hivyo?
Kuhusu Mengi kuwa dalali kamwonea kwani wao kutwa wapo safarini kutafuta ten % kwa hao wanaowaita wawekezaji! Sasa kati yake na Mengi nani dalali?
Muhongo ajitafakari upya juu ya utendaji wake na dhana nzima ya kuwapa wazawa fursa ya kumiliki vitalu vya gas otherwise atatuletea ya Boko-haram
Nigeria.
Kwani hajajifunza ya Karamagi kuuza migodi yetu na kuwafukuza wazawa? Au anatekeleza sera ya ccm kuuza kila kitu kwa wageni?
Awe wazi tu nitamwelewa.
 
KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225
1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.

2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha
kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:

"Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu."

4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.

5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.

8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.

Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013

Reginald Mengi ni Nduma kuwili anajifanya CHADEMA huku akifanya kazi ya Kikwete sasa anagombana na Prof Mhogo kwa kuwa naye anataka mali.

Mengi amezuia Vyombo vyake vya habari kuandika habari yoyote inayomhusu Kikwete na Ufisadi kwa kuwa yupo kwenye koti hilo, sasa Mengi huyo huyo anapingana na Prof Mhogo ambaye ni Mteule wa Kikwete huyohuyo anayelindwa na Mengi.
Sasa kama anadhamila ya dhati Mengi aondoe Mkataba na Kikwete.

Prof Mhogo na Mengi wote wanamtumikia Kikwete na CCM
 
Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,089
2,000
Huyu Mengi anadhani kwa sababu watu wanaichukia CCM basi watakubaliana na utetezi wa kipuuzi kama huu. Eti nina eneo la ubia lisilozidi kilomita moja za mraba, kwelii? Anamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,878
2,000
Itabidi nikajifunze vizuri hezabu za kuzidisha, hasa hii tebo mpya ya Dar.
Dar mara moja Dar,
dar mara mbili sijui nini
Dar mara tatu......
 
mamseri

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
704
500
jamani acheni kushabikia vitu hamvijui mi nishafanya kazi kwa mengi pale mererani block D yaani hata hio km moja haina mtu mwenye eneo kubwa kwa mererani n Tanzanite one mi nilisikia nikafikiri labda ana eneo lingine kumbe alimaanisha mererani huyo ni muongo kupindukia
 
M2flan

JF-Expert Member
Jun 27, 2013
414
250
1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.

2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha
kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:

“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”

4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.

5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.

8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.

Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013

Prof.Muhongo jina lake linasadifu wasifu wake
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,253
2,000
Hii sinema bado mbichi Mengi vs Muhongo hv ikitokea tukawapa kamba washindane kuivuta nani ataibuka mshindi ?
 
jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,344
2,000
1. Kwanza anajiita 'Dr' wakati doctorate yake haitambuliki TCU (and therefore Tanzania) tayari hapo anathibitisha kuwa yeye ndio Muongo!
2. Mengi anaongea kisiasa. Alichokuwa anarefer prof Mhongo ni vitalu vya utafutaji madini ambavyo si tu Mengi anamiliki kupitia complex shareholding structures bali tayari ameshauza hisa za baadhi kwa makampuni ya nje.
Kuthibitisha uongo wa mengi cheki hii thread hapa ya mwaka 2010. Kazi yake huyu bwana ni udalali tu sio uwekezaji!

IPP gold strikes deal
"Douglas Lake Minerals Inc. (the "Company" or "Douglas Lake") (OTCBB:DLKM)(FRANKFURT:D60) is very pleased to announce that the Company has recently received approval from its Board of Directors to both enter into and immediately close upon the terms and conditions of a certain Mineral Property Acquisition Agreement (the "Acquisition Agreement"), with IPP Gold Ltd. ("IPP Gold"), to acquire a 100% interest in four prospecting licences (the "PLs"), totaling approximately 800 square kilometres, located in the Handeni District of Tanzania and which are owned or controlled by IPP Gold and its affiliates." 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,478
2,000
Mengi nilitaraji ungejibu kisomi yaani Facts and Figures sasa naona majibu yake yamekaa kisiasa kweli na ilo la Handeni jee.
Tuambie unamiliki maeneo yapi then tusum up ukubwa wa maeneo haYO!
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,684
2,000
Hii sinema bado mbichi Mengi vs Muhongo hv ikitokea tukawapa kamba washindane kuivuta nani ataibuka mshindi ?

Mimi sasa hapo ndipo panaponipa wasiwasi mno, ndiyo maana muda wote natamani hawa watu wapate suluhu na wawe marafiki. Wakiedelea hivi bila muafaka baadaye utakuja kuibuka mziki mtamu hapa nyie wenyewe mtashangaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom