whizkid
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 357
- 240
Kutokana na yaliyojiri kuhusu kutumbuliwa kwa mkurugenzi wa TANESCO (sababu anazijua mwajiri wake) na kusitishwa kwa bei mpya za umeme kwa mwaka 2017 mpaka serikali itakapopitia kwa kina ripoti ya EWURA (kulingana na barua ya waziri kwenda EWURA), tujikumbushe kanuni zinazotumika katika kupanga bei ya umeme nchini.
NOTE: 5(a) na 5(b) ni kwa manufaa ya mjadala. Kanuni zote zimeambatanishwa kwenye uzi huu.
Pia, ifahamike kuwa, kusitishwa kwa bei mpya iliyopendekezwa na EWURA haimaanishi bei ya umeme haitopanda milele. Ni mchakato ambao upo kisheria na ni jukumu la EWURA kusimamia. Hivyo basi, kwa maoni yangu, iwapo ripoti ya EWURA itaonesha ulazima wa kupandisha bei, serikali kama mmiliki na mdau muhimu wa TANESCO itabidi akubali matokeo au/na akikataa, kuwe na njia mbadala ya kufidia gharama za uendeshaji wa shirika ili bei zisipande.
Mwisho, namtakia kila la kheri "kaimu" mkurugenzi mpya wa TANESCO ambaye naamini yupo tayari kupitia makabrasha ya TANESCO na kuja na mkakati wa kuendesha shirika kwa faida bila kupandisha bei za umeme.