Kanuni za kuishi na watu/binadam Vizuri

Kanuni za kuishi na watu/binadam Vizuri

ushauri mzuri sana naunafaa kwa watu usiokaabao kwa muda mwingi kama wateja ,majirani ,wapita njia na watu tunaokutanao njiani lakini kwa wafanyakazi wenzetu huko makizini ni ngumu sana
 
KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI.


View attachment 438959

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote

maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana

hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa

wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila

mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri._

1) Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda._
_
2) Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana._

_3) Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika._
_
4) Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu._
_
5) Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe._
_
6) Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga._
_
7) Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya._
_
8) Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu._
_
9) Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo._
_
10) Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa._
_
11) Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda._
_
12) Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu._
_
13) Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu._

_14) Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu._
_
15) Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki._
_
16) Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea._

_17) Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema._

_18) Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo._
_
19) Tunza siri zako na za wengine._
_
20) Usiwe mwepesi wa hasira_
_
21) Kumbuka majina ya watu unaokutana nao._

_22) Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri._
_
23) Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli._
_
24) Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda._
_
25) Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika._
_
26) Jifunze kusamehe makosa ya watu._
_
27) Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha._
_
28) Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako._
Mi ninazo 32 na zote nazitimiza.....
 
Mh. Mzizi leo naona umeamua kututibu saikolojia zetu. Asantesana. Wengine hua wavivu ukimwambia ndimu2 mdalasini uliosagwa na habatsoda anaona kama vile kapewa hesabu za logarithm. Ila hii ni kusoma na kusave changes tu na kuapply. Asante mkuu
 
Maneno mazuri, kwakweli Mungu atusaidie tu.

Hivi ukitimiza hayo si umekuwa malaika[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] nawaza tu.
Sikuzote personality inakua shaped kwa kufunzwa au kuachwa uendeleze ujinga. Mfano kuna familia wao kutukana ni msamiati wa kawaida sana so mtoto atakayelelewa hapo usitaraji atakuwa muungwana kwenye maongezi.

Lkn angalia pia ww unayedhani unafanya vzr hvyo vigezo alivyorusha Bwn. Mzizi utagundua kuwa ulilelewa hvyo na ukashauriwa vzr na wale uliowaamini wengine hata kuombewa mmeombewa.

Hivyo tusikimbilie tu kusema hvyo ni vigezo vya malaika tunakwepa wajibu kinamna.
 
Pamoja na kwamba mazingira aliyokulia mtu yanachangia kwa kiasi kikubwa...unaweza kujifunza haya mambo ukubwani ukakata tamaa kabisa!!!

Watu wakatumia sifa hizo kama udhaifu wako kukufanya daraja!!
Hekima ya kuishi na watu ndyo kuu kuliko yote kama una mambo hayo ukakosa hekima hakika hauwezi kumantain.
 
Pamoja na kwamba mazingira aliyokulia mtu yanachangia kwa kiasi kikubwa...unaweza kujifunza haya mambo ukubwani ukakata tamaa kabisa!!!

Watu wakatumia sifa hizo kama udhaifu wako kukufanya daraja!!
Hekima ya kuishi na watu ndyo kuu kuliko yote kama una mambo hayo ukakosa hekima hakika hauwezi kumantain.
kweli kabisa
 
tatizo ni hili; unaweza ukawapenda na kuwajali watu wote bila ya kuangalia kipato chao, elimu yao,rika, jinsia zao n.k.......Lakin watu hao hao wakat mwingine hukugeuka na kuwa maadui wako-mfano Yesu.

Na siku zote katika kanuni ya kuishi,,"Binadamu ni wepesi sana wa kukumbuka mabaya {hata kama ni moja} kuliko mema mengi uliyowatendea"
-Mfano Gadafi.

Na ktk ulimwengu huu wa maisha ya vuta nikuvute, kukwaruzana hakukwepeki.So kuvumiliana ndipo kunapopaswa kuchukua mkondo wake.....Japokuwa unaweza kuwavumilia watu kwa madhaifu yao lakin wao wakashindwa kukuvumilia kwa madhaifu yako.
=== ===============

"Ndo walivyo binadamu"
Noted
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom