Kanuni za kuishi na watu/binadam Vizuri

Kanuni za kuishi na watu/binadam Vizuri

Sifa nyingine, USIJENGE UKUTA KWENYE KIWANJA KISICHO CHAKO
 
Mtoa mada unamteta Mkuu wangu wa kazi, au tupo office Moja? Mana hizi ID tuzitumiazo usikute tupo kijiwe kimoja.
 
Jifunze kusali/ kuswali
Kwa kumtegemea Mungu . Usisahau kufunga Kwa maombi
Na kutoa fungu la 10, na zaka
Unaweza kuswali alafu ukawa mchawi vile vile au gaidi
 
Safi sana mkuu kwa ujumbe mzur ila no 21. Ulitaka kumaaanisha nini unaweza fafanua
 
tatizo ni hili; unaweza ukawapenda na kuwajali watu wote bila ya kuangalia kipato chao, elimu yao,rika, jinsia zao n.k.......Lakin watu hao hao wakat mwingine hukugeuka na kuwa maadui wako-mfano Yesu.

Na siku zote katika kanuni ya kuishi,,"Binadamu ni wepesi sana wa kukumbuka mabaya {hata kama ni moja} kuliko mema mengi uliyowatendea"
-Mfano Gadafi.

Na ktk ulimwengu huu wa maisha ya vuta nikuvute, kukwaruzana hakukwepeki.So kuvumiliana ndipo kunapopaswa kuchukua mkondo wake.....Japokuwa unaweza kuwavumilia watu kwa madhaifu yao lakin wao wakashindwa kukuvumilia kwa madhaifu yako.
=== ===============

"Ndo walivyo binadamu"
 
Mm hapo hata moja sinaaa.. seriously... na napendwa na watu vibaya mnooo mnooo... nina pesa za uhakika... na nawapa fedha wakiwa na matatizo mfano misiba, harusi, ada kwa majirani, na natoa hela ndefu kidogo eg. harusi laki 5, ada nachanga laki 3, misiba nawapa hata gari..

Ila napendwa sana sanaaaa, na sina hizo sifa hata moja hapo juuu.. in short sina muda na mtu... mm ni kazi tu...!!

Tafuta fedha halali uwe na uwezo mzuri, achana na hayo... utakufa maskini.. ooh
 
Kwa hizi kanuni hata kiongozi wa dini sidhani kama anazitekeleza zote
 
Kwa hizo sifa labda uwe malaika ila sio uliyetoka kwenye tumbo la mwanamke, kuna kipindi niliamua niishi maisha ili nimpende kila mtu kwa kufanya wema na kuchangamkia watu sana ila niliishia kukopwa na wengine kunionesha dharau kwa kudhani najipendekeza na kupigwa majungu. Walishangaa nimebadilika ghafla na kurudi katika ya kawaida ndio nikagundua huwezi kumridhisha kila kiumbe ishi maisha yako aisee hawa raia hawana jema eti.
 
kwa kusumaraizi tunasema...KIKUBWA NI KUWA NA UPENDO (1 Wakorintho 13)
Hakika muhtasari wa yote hayo ni UPENDO. Kwa maana nyingine ni USIWATENDEE WENZAKO YALE USIYOPENDA KUTENDEWA bali Watendee wenzako yale ambayo ungelipenda wakutendee. Haihitaji hata nukuu ya kitabu, Ukweli ni kwamba hii ni kanuni ambayo Mwenyezi MUNGU alikwishatuumbia moyoni mwetu. Kwa ufupi tumezaliwa nayo.
 
Ukiwa hivo jiandae kutendwa kila siku,wewe utakuwa ni mtu wa vilio tu. Cha kufanya ni kuwa 50/50 sometimes yes sometimes no,yaani husomeki wakikuzingua unawazingua wakikuheshimu unawaheshimu.
 
Kanuni yako kuhusu Matusi haikubaliki kwa Wazee wa Bandari. Wana matusi shetani kasingiziwa na ni watu poa mpaka mwisho...
 
Kanuni nyingine: Ukitaka kuishi na watu vizuri

- Ipende Tanzania
- Mpende JPM
- Ipende CCM
- Ipende System yake

Hapo utaishi kwa raha mustarahe.

TZ Baby.
 
KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI.


KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZUR.jpg


Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote

maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana

hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa

wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila

mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri._

1) Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda._
_
2) Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana._

_3) Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika._
_
4) Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu._
_
5) Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe._
_
6) Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga._
_
7) Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya._
_
8) Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu._
_
9) Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo._
_
10) Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa._
_
11) Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda._
_
12) Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu._
_
13) Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu._

_14) Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu._
_
15) Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki._
_
16) Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea._

_17) Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema._

_18) Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo._
_
19) Tunza siri zako na za wengine._
_
20) Usiwe mwepesi wa hasira_
_
21) Kumbuka majina ya watu unaokutana nao._

_22) Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri._
_
23) Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli._
_
24) Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda._
_
25) Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika._
_
26) Jifunze kusamehe makosa ya watu._
_
27) Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha._
_
28) Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako._
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom