Kanuni ya Hisia (Kanuni ya 7 ya Akili na Ulimwengu)

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,218
Uhusiano kati ya Uhalisia Mawazo na Hisia.

Huwezi kuwa na hisia bila kuwa na wazo.
Kauli ni sawa na kusema kuwa hisia hutokea baada ya wazo kuwepo. Ikiwa na maana kuwa wazo hupelekea hisia na hisia haiwezi kuwepo bila wazo kuwepo.



Sheria hii inahusu sana uhusiano uliopo kati ya Wazo na Hisia. Kuwa makini na hili, kuwa huwezi kuwa na hisia bila kuwa na wazo kwanza. Unapoelewa hilo vyema, utaelewa kuwa hata hasira haiwezi kuwepo bila kuwa na wazo la kuudhi akilini. Kwa maana kuwa mawazo ya hasira hupelekea hasira. Pia huwezi kuhuzunika bila kuwa na mawazo ya kuhuzunisha akilini. Huwezi kuwa na hisia za upendo bila kuwa na asilimia kubwa ya mawazo ya upendo akilini. Hivyo utaona kuwa mawazo mengi hupelekea Hisia kuwepo katika upande wenye mawazo mengi. Ni sawa na akili uliilinganisha na anga, kuna mawingu mbalimbali (mawazo), mawingu hayo sio anga (mawazo sio akili), bali mawingu hayo ni hali ya kupita pita tu na hayapo stable (mawazo huibuka na kupotea akilini, wewe ni mtazamaji wa mawazo yako na sio mwingine, mawazo ya aina mbalimbali ni kama hali mbalimbali, hali ya aina fulani ikikua basi hupelekea hali ya hewa kubadilika badilika).

Uhusiano wa Mawazo, Hisia na Tabia.

Watu wanaofikia kuuelewa ukweli huu hasa kwa kujichunguza hujifunza point ya msingi sana. Hujifunza kuwa makini na mawazo yazungukayo akilini mwake, huyachunguza, na hujichunguza kuangali uhusiano wake na mawazo yako na kuchunguza aina ya mawazo yanayomtawala.

Hebu tujaribu kuifanyia majaribio Kanuni hii.

LIMAO: Hebu vuta picha unaonja limao. Nini kinatokea baada ya hapo? Utaona kuwa wazo hilo limechangamsha mdomo, mate yakatokea au ukasisimka ilimi kama vile hali ile inavyokukuta wakati ukilila. Lakini hamna limao bali ni wazo tu na kuweka fikra yako katika picha hiyo na effect yake inatendeka mwilini.

Weka picha akilini mwako ya mtu ambaye amekukosea. FIkiria kwa muda sababu au mabaya anayokufanyia uone ni mbaya. Unapata hisia gani? Je unaihisi hasira? Mapigo ya moyo yamebadilika? Kuna wakati unaweza kuwaza kitu fulani au hali au mtu na kupelekea kupata hisia fulani labda ni hasira, furaha n.k

Hasira. Hasira ni aina ya hisia ambayo wengi tunaifahamu vyema kuwa ina adhari kubwa sana kwa anayeibeba. Hasira inaweza kuongeza mapigo ya moyo kwenda kasi, adrenalini kutengenezwa, na vyote hivyo vinaanza katika viwazo vinavyotawala kwanza na hatimaye huweka hisia.

Watabiri.Wapo watu mbalimbali walioelewa ukweli huu na wakajifunza kuwa watabiri. Siri kubwa wanayobeba katika kutabiri na kumsoma mtu ni kuwa akili, mawazo yako na ufahamu wako upo katika hali ya energy/umeme. Mtu mwenye kujifunza kufahamu energy ya wenziye anaweza kuelekeza ufahamu wake kutambua ufahamu wako kwa kusoma subconscious mind yako vyema. Wote hawa hutambua kuwa reality yako haiumbwi nje bali inaumbwa ndani yako inaumbwa ndani. Na kama inaumbwa ndani basi reality yako ya ndani ilivyo hivi sasa ndio reality yako ya nje ijayo. Ukiweza kusoma reality ya ndani unaweza kufahamu reality ijayo ambayo ndio reality ya nje.




Hivyo kwa kutoa ujumbe mzuri kuhusiana na hilo, tunapaswa kuweka akilini kuwa hisia yako haina nguvu kama mawazo yako. Hatuhitaji kuweka akili kwenye hisia bali kuijua hisia imeanzaje tunapaswa kuangalia asilimia kubwa ya mawazo yetu imetawaliwa na upande gani.


Asante

@blessing-baraka @UNDENIABLE @KikulachoChako @aretaskimario @Patrickn @Noah.. @Ms.Lincoln @IGWE @aretaskimario @crunkstaa @Matola @it is me


 
Mkuu nimepitwa na sheria kama mbili hivi (ya 5 & 6) lkn bado tunaenda sawa.

Samahani kama nitakosea lkn naomba niulize kama kuna group lolote whatssap ambalo una deal nalo kutoa Elim hii. Me nimedhamiria kujifaham vizuri ubinaadam wangu.
 
Mkuu nimepitwa na sheria kama mbili hivi (ya 5 & 6) lkn bado tunaenda sawa.

Samahani kama nitakosea lkn naomba niulize kama kuna group lolote whatssap ambalo una deal nalo kutoa Elim hii. Me nimedhamiria kujifaham vizuri ubinaadam wangu.

Habari ndugu yangu. Nashukuru sana kwa kuwa pamoja nami katika kuelekezana.

Sina group lolote na sitegemei kuweka group lolote kwenye Whatsapp. Napendelea kushare online na kila mtu ajifunze. Labda kama ni Blog ndio nilipendelea kuweka ili wengi wachangie na kutoa mawazo yao. Wanaokaribishwa ni wale wote wanaotamani kufahamu maana za maisha kwa ujumla.

Nashukuru sana ndugu yangu. Asante.
 
thumb up kwako mkuu Apollo
nimejifunza na ninaendelea kujifunza mengi kutoka kwako mkuu

. made in mby city.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom