Kanuni 3 zinazotawala ulimwengu wa roho

Kanuni 3 zinazotawala ulimwengu wa roho

Daraja2

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
285
Reaction score
346
Watu wema wanapolala usiku na kupitiwa na usingizi mzito,roho zao hufanya "khiyana" kwa kutoroka na kuacha viwili-wili vyao kusafiri umbali mrefu sana kwenda katika ulimwengu wa roho.
Roho hizo zinapofika katika ulimwengu wa roho kabla hazijatua chini(ardhini) huvalishwa viwili-wili kama vya huku duniani.Kiwili-wili hicho maalum kinauwezo mkubwa sana wa kuhimili hali ya hewa ya huko kwa kutembea chini(ardhini), kuruka juu na kusafiri angani.Kiwili-wili hicho kinafanana sana na cha huku duniani lakini si cha huku duniani.
Ulimwengu wa roho ni kisiwa Fulani ambacho hakipo juu(mbinguni),chini(ardhini) wala angani(yaani kati ya mbingu na ardhi) huku duniani Bali kipo sehemu maalum iliyojificha.Kisiwa hicho kina ardhi yake na anga yake pia.

Kuna kanuni kuu 3 zinazoongoza ulimwengu wa roho kwa watu wake yaani "watu-roho".
1.Ukitaka kuruka juu na kutembea angani sharti mbebane jinsi mbili tofauti,yaani mmoja kumbeba mwenzake mgongoni kama mama anavyombeba mtoto wake mchanga huku duniani.
-------Ninaposema "jinsi" ni tofauti ya kimaumbile kibaiolojia kati ya mwanamke na mwanaume.
2."mwanamke-roho" mwenye umri sawa na "mwanaume-roho" anaweza kuruka na kumwendesha "mwanaume-roho" wa umri wake angani.Jambo hili litawezekana tu mpaka mwanaume-roho husika atoe idhini(ruhusa).
------Ninaposema umri sawa ni kwamba ,kama mwanaume-roho ana umri wa miaka 21 lazima mwanamke-roho pia awe na umri wa miaka 21na si vinginevyo.
3."Mwanaume-roho" mwenye umri mdogo ndiye anayeruka na kumwendesha "mwanamke-roho" aliyemzidi umri.Katika ulimwengu wa roho "mwanaume-roho" ndiye kiongozi mkuu.

ZOEZI/HOME -WORK
1.Taja tofauti 3 kati ya dunia na ulimwengu wa roho.
2.Roho ipi ya kwanza kuingia ulimwengu wa roho(me/ke)?
3.Ni watu wa rika lipi zaidi wanaopatikana katika ulimwengu wa roho? taja umri wao.
4.Je "watu-roho" wanaweza kuvunja kanuni zinazotawala ulimwengu wa roho? Kama ndiyo/hapana toa Maelezo.
5.Taja sifa/tofauti 6 kati ya "mtu-roho" na "mtu-dunia".
6.Je "watu-roho" wanaweza kuja duniani.kama ndiyo/hapana toa Maelezo.
7.Je roho za viumbe wengine zinaweza kuingia kwenye ulimwengu wa roho?
8.Taja sifa/tofauti 5 kati ya "mwanamke-roho" na "mwanamke-dunia".

--------Ahsanteni kwa kuwa pamoja na tutaonana majaliwa!
4



Sent from my HUAWEI Y360-U82 using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa somo mkuu liko poa sana ila muda uliolitoa daaah nashindwa kulala naogopa roho isije nitoroka ikasepa
 
Unazungumza habari ya astral projection. Roho ya mtu huweza kutoka na kuacha mwili lakini lazima roho nyingine kama ya jini ichukue nafasi la sivyo mwili unakufa. Hii inafanyika lakini nitoe onyo kuwa ni kitu kibaya na cha hatari sana! Kama hakifanyiki kwa mapenzi na maongozi ya Roho Mtakatifu kitendo hiki ni ushirikina na kina hatari kubwa kwa afanyaye. Tafadhali usijaribu.
 
JF sio sehemu ya kutoa Homework mkuu...i hate homework
 
hii mada kama vile ni nzuri lakini imekosa mvuto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom