Kansa yaendelea kuwa tishio Tanzania. Kilimanjaro na Dar Es Salaam yaongoza kuwa na wagonjwa wengi zaidi

Kansa yaendelea kuwa tishio Tanzania. Kilimanjaro na Dar Es Salaam yaongoza kuwa na wagonjwa wengi zaidi

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Idadi ya wagonjwa wa saratani nchini Tanzania imeripotiwa kuongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.
Ripoti mpya inaonyesha kuwa jumla ya wagonjwa 16,516 walirekodiwa kati ya mwaka 2019 hadi 2023.

Kwa wanaume saratani ya tezi dume ndio inayoongoza, wakati kwa wanawake saratani ya shingo ya kizazi inaendelea kuwa juu.

Taarifa hizi zinatoka kwenye Ripoti ya Usajili wa Saratani Tanzania 2019 hadi 2023 iliyotolewa na Wizara ya Afya. Ripoti hiyo inatoa tathmini ya miaka mitano kwa kutumia takwimu kutoka vituo vitano vya usajili wa saratani vya Dodoma Kilimanjaro Dar es Salaam Mbeya na Mwanza.

Ripoti inaonyesha kuwa mkoa wa Kilimanjaro umeongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi 6,161 ambao ni asilimia 37 ya kesi zote nchini.

Dar es Salaam ilifuata kwa kesi 3,521 ambayo ni asilimia 21 Dodoma 2,999 asilimia 18 Mwanza 2,220 asilimia 13 na Mbeya 1,615 asilimia 9

Source: The CItizen

Akizungumzia takwimu hizo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Jairy Khanga amesema sio kwamba mkoa wake una wagonjwa wengi lakini ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali umeimarisha huduma za saratani na kuchangia upatikanaji mkubwa wa takwimu.

===========================


The number of cancer cases in Tanzania is on the rise as more people adopt lifestyles that increase the risk of non-communicable diseases.

A new report shows that the country recorded a total of 16,516 cancer cases between 2019 and 2023.

Prostate cancer remains the most common type among men, while cervical cancer leads among women, highlighting a growing national cancer burden that calls for increased awareness, early detection, and improved access to treatment services.

The findings come from the Tanzania Cancer Registry Report 2019–2023, published by the Ministry of Health. The report offers a five-year analysis of cancer across the country, based on data collected from five Population-Based Cancer Registries (PBCRs) in Dodoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mbeya, and Mwanza.

The report reveals that Kilimanjaro Region recorded the highest number of cancer cases, with 6,161 cases (37.3 percent) of all reported cases nationwide.

It was followed by Dar es Salaam with 3,521 cases (21.3 percent), Dodoma with 2,999 cases (18.2 percent), Mwanza with 2,220 cases (13.4 percent), and Mbeya with 1,615 cases (9.8 percent).

Commenting on the figures, Kilimanjaro Regional Medical Officer, Dr Jairy Khanga, said there is no specific reason why Kilimanjaro leads in cancer cases but credited the results to significant investments and partnerships that have strengthened cancer services in the region.

Source: The Citizen
 
Akizungumzia takwimu hizo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Jairy Khanga amesema sio kwamba mkoa wake una wagonjwa wengi lakini ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali umeimarisha huduma za saratani na kuchangia upatikanaji mkubwa wa takwimu
Yes hii ndio point yenyewe. Ukiona una wagonjwa wengi ujue umepima wengi pia!!
 
Back
Top Bottom