Kansa mpya imeingia Mtanzania kuwa makini

HT

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,897
414
mimi ni Mtanzania mwenzenu ambaye baada ya kuona mwelekeo wa nchi yetu nimeona ni vema niwakumbushe wana wa Tanzania. Ndugu zangu watanzania, kuna kansa ambayo imetokea, imeota na sasa inaelekea kukomaa. Kansa hii inaangamiza taifa na kutufanya tuwepo hapa tulipo, imeleta majanga ya kiuchumi tuliyo nayo na imetufikisha hapa tulipo. Ndugu zangu Watanzania, tusipoiangalia na kuitibu kansa hii tunaelekea pabaya sana. Tuanelekea ktk rima refu ambalo kutoka kwake ni neema za Mungu tu.

Kansa ninayoiongelea hapa si ufisadi, wimbo ambao unaimbwa sana. Ufisadi ni sawa na maumivu ambayo kama kidonda kipo lazima yawepo. Siongelei ushabiki wa kisiasa, maana kama umepanda mti, lazima matawi yatamea tu. Ninaongelea kupoteza utambulisho wetu, Utanzania wetu na uzalendo wetu.

Ndugu zangu watanzania, ninyi ni mashahidi jinsi ambavyo watu wengi wamepoteza utambulisho wa wao ni akina nani, hawakuishia hapo wakatupa kando uzalendo na kujisahaulisha wanatoka wapi. Kwa sababu hiyo wakawaona watanzania wenzao ni mtaji wa kujinufaisha na wakasahau nchi ya uzalendo wao, hata wakatajirisha nchi nyingine wakipatia umaskini kwao. Laiti wangelijua wao ni watanzania na ya kuwa watanzania wengine ni ndugu zao, wakatunza uzalendo wao: wangeijenga nchi yao.

Ndugu zangu watanzania, tazama wanasiasa na wafuasi wao walivyopotoka. Wamesahau kuwa wao ni watanzania na kuwa hata wanaopingana nao kisisasa ni watanzania pia. Kama wangelikumbuka walau hili wangewachukulia kwa heshima. Ni nani asiyejua kuwa watanzania ni watu wa staha? Lakini kwa kupoteza utambulisho wetu hatueleweki ni watu wa aina gani na taifa gani. Tunaenenda kama watu wasio na taratibu. Tumedharauliwa na mataifa mengine kwa kuwa si wazalendo tena. Mzalendo huilinda nchi yake na ndugu zake. Kwa kukosa hilo tunatumika na wageni dhidi ya ndugu zetu na nchi yetu.

Vijana mashuleni wanasoma ili wachukue chao mapema. Haya ndiyo matunda ya mfumo wa elimu usiojenga uzalendo. Hatuthamini bidhaa zetu tena maana hatuna uzalendo.

Bado hatujafika hatua ambayo hatuwezi rudi tena, bado tunaweza kubadilika. Wapenzi ndugu zangu, turudishe moyo wa uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu. Hebu uamue kufanya kitu kwa ajili ya nchi yako na watu wako. Usiangalie faida utakayopata kwanza, bali angalia neema utakayoleta kwanza. Ndugu zangu watanzania, tutangulize utanzania wetu kwanza kabla ya siasa. Hebu tuijenge nchi yetu kwanza, maana sisi ndio wana wa Tanzania. Si mwamerika wala mwarabu wala mganda hata mkenya atatujengea nchi yetu. Wao wana nchi yao nasi tuna Tanzania yetu

vijana wa Tanzania, tuamke na tuanze kujivunia nchi yetu. Hata kama ina matatizo na tujivunie huku tukitafuta suluhu halisi na sio politics. Anza kujivunia utanzania wako maana hata kama ukibadili uraia kimaandishi na kimaeneo, bado Mungu alikuweka Tanzania na daima utabaki Mtanzania.

Niwatie moyo wanawake na wanaume wa nchi hii, nchi yetu ni tajiri na bado tunaweza kuichukua juu. Mungu tusaidie wana wa Tanzania tuamke na kuipenda nchi nzuri sana uliyotupa, tusimame na kujivunia.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania,
nawapenda wote,
HT
 
mbona umelalamika tu sijaona kipya au kitu sensitive ktk hii thread yako. Umejaza longolongo nyingiiiiiiiiii. hebu jitazame upya then uuweke tena huo uzi
 
HT Kaongea ukweli kbs ila ametupatia kichwa cha thread ikiwa katika hali ya mshituko mkubwa kwa yeyote aliyeipitia na kuisoma. HT! We piga kimya kwani UKOMBOZI hauko mbali hata kidogo Kamanda wangu. Utafurahi!!
 
HT kansa hiyo ni ufisadi. Ingawa wewe unaiita ni kupoteza utambulisho. Watanzania hata hivyo wako macho sasa wakipigana kufa na kupona kuiondoa kansa hii.
 
U,
ufisadi ni zao na sio chanzo. kukiwa na donda maumivu hayakosekani
 
mbona umelalamika tu sijaona kipya au kitu sensitive ktk hii thread yako. Umejaza longolongo nyingiiiiiiiiii. hebu jitazame upya then uuweke tena huo uzi
N,
sijaelewa kama nimetumia lugha ngumu au wewe ni mmoja ya wanaohitaji kufanya U turn!
 
HT Kaongea ukweli kbs ila ametupatia kichwa cha thread ikiwa katika hali ya mshituko mkubwa kwa yeyote aliyeipitia na kuisoma. HT! We piga kimya kwani UKOMBOZI hauko mbali hata kidogo Kamanda wangu. Utafurahi!!
L,
hii kansa inaenea kwa kasi hata kizazi kijacho tumekiambukiza. Tunahitaji kusimama kugeuka na kurudia Utanzania wetu na uzalendo wetu. Ni mara chache leo hii mtu kujivunia utanzania unless Stars wamepita kuelekea hatua nyingine!
 
mimi ni Mtanzania mwenzenu ambaye baada ya kuona mwelekeo wa nchi yetu nimeona ni vema niwakumbushe wana wa Tanzania. Ndugu zangu watanzania, kuna kansa ambayo imetokea, imeota na sasa inaelekea kukomaa. Kansa hii inaangamiza taifa na kutufanya tuwepo hapa tulipo, imeleta majanga ya kiuchumi tuliyo nayo na imetufikisha hapa tulipo. Ndugu zangu Watanzania, tusipoiangalia na kuitibu kansa hii tunaelekea pabaya sana. Tuanelekea ktk rima refu ambalo kutoka kwake ni neema za Mungu tu.

Kansa ninayoiongelea hapa si ufisadi, wimbo ambao unaimbwa sana. Ufisadi ni sawa na maumivu ambayo kama kidonda kipo lazima yawepo. Siongelei ushabiki wa kisiasa, maana kama umepanda mti, lazima matawi yatamea tu. Ninaongelea kupoteza utambulisho wetu, Utanzania wetu na uzalendo wetu.

Ndugu zangu watanzania, ninyi ni mashahidi jinsi ambavyo watu wengi wamepoteza utambulisho wa wao ni akina nani, hawakuishia hapo wakatupa kando uzalendo na kujisahaulisha wanatoka wapi. Kwa sababu hiyo wakawaona watanzania wenzao ni mtaji wa kujinufaisha na wakasahau nchi ya uzalendo wao, hata wakatajirisha nchi nyingine wakipatia umaskini kwao. Laiti wangelijua wao ni watanzania na ya kuwa watanzania wengine ni ndugu zao, wakatunza uzalendo wao: wangeijenga nchi yao.

Ndugu zangu watanzania, tazama wanasiasa na wafuasi wao walivyopotoka. Wamesahau kuwa wao ni watanzania na kuwa hata wanaopingana nao kisisasa ni watanzania pia. Kama wangelikumbuka walau hili wangewachukulia kwa heshima. Ni nani asiyejua kuwa watanzania ni watu wa staha? Lakini kwa kupoteza utambulisho wetu hatueleweki ni watu wa aina gani na taifa gani. Tunaenenda kama watu wasio na taratibu. Tumedharauliwa na mataifa mengine kwa kuwa si wazalendo tena. Mzalendo huilinda nchi yake na ndugu zake. Kwa kukosa hilo tunatumika na wageni dhidi ya ndugu zetu na nchi yetu.

Vijana mashuleni wanasoma ili wachukue chao mapema. Haya ndiyo matunda ya mfumo wa elimu usiojenga uzalendo. Hatuthamini bidhaa zetu tena maana hatuna uzalendo.

Bado hatujafika hatua ambayo hatuwezi rudi tena, bado tunaweza kubadilika. Wapenzi ndugu zangu, turudishe moyo wa uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu. Hebu uamue kufanya kitu kwa ajili ya nchi yako na watu wako. Usiangalie faida utakayopata kwanza, bali angalia neema utakayoleta kwanza. Ndugu zangu watanzania, tutangulize utanzania wetu kwanza kabla ya siasa. Hebu tuijenge nchi yetu kwanza, maana sisi ndio wana wa Tanzania. Si mwamerika wala mwarabu wala mganda hata mkenya atatujengea nchi yetu. Wao wana nchi yao nasi tuna Tanzania yetu

vijana wa Tanzania, tuamke na tuanze kujivunia nchi yetu. Hata kama ina matatizo na tujivunie huku tukitafuta suluhu halisi na sio politics. Anza kujivunia utanzania wako maana hata kama ukibadili uraia kimaandishi na kimaeneo, bado Mungu alikuweka Tanzania na daima utabaki Mtanzania.

Niwatie moyo wanawake na wanaume wa nchi hii, nchi yetu ni tajiri na bado tunaweza kuichukua juu. Mungu tusaidie wana wa Tanzania tuamke na kuipenda nchi nzuri sana uliyotupa, tusimame na kujivunia.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania,
nawapenda wote,
HT

Ulikuwa Masomoni Nje ya nchi na hukuwa connected na Internet? Karibu nyumbani mzazi
 
Utanzania ni UTU!

Utu hauna dini, utu hauna itikidai, utu hauna ukabila, utu ni uadilifu, hauna ukanda, ni umoja, ni ustwi wa familia, jaimi na ni Uzalendo. Utu ndio msingi wa Utaifa wetu. Ulichooni ni sahihi ..Kuporomoka kwa UTU ..Ni kansa! Sasa tuitibu!!!

Pamoja na michango itakayotolewa hapa jinsi ya kuutibu Utu wa mtu na hatimaye kutibika kwa Utanzania gonga hapa! (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/192708-nini-hasa-maana-ya-utu.html)
 
Ulikuwa Masomoni Nje ya nchi na hukuwa connected na Internet? Karibu nyumbani mzazi
hapana ndugu yangu, nilikuwa naangalia sinema nyingi zinazoendelea zilizotokana na kupoteza utanzania wao!

Tuungane ndugu tuipinge kansa hii, tujenge nchi yetu nzuri sana Tanzania!
 
mimi ni Mtanzania mwenzenu ambaye baada ya kuona mwelekeo wa nchi yetu nimeona ni vema niwakumbushe wana wa Tanzania. Ndugu zangu watanzania, kuna kansa ambayo imetokea, imeota na sasa inaelekea kukomaa. Kansa hii inaangamiza taifa na kutufanya tuwepo hapa tulipo, imeleta majanga ya kiuchumi tuliyo nayo na imetufikisha hapa tulipo. Ndugu zangu Watanzania, tusipoiangalia na kuitibu kansa hii tunaelekea pabaya sana. Tuanelekea ktk rima refu ambalo kutoka kwake ni neema za Mungu tu.

Kansa ninayoiongelea hapa si ufisadi, wimbo ambao unaimbwa sana. Ufisadi ni sawa na maumivu ambayo kama kidonda kipo lazima yawepo. Siongelei ushabiki wa kisiasa, maana kama umepanda mti, lazima matawi yatamea tu. Ninaongelea kupoteza utambulisho wetu, Utanzania wetu na uzalendo wetu.

Ndugu zangu watanzania, ninyi ni mashahidi jinsi ambavyo watu wengi wamepoteza utambulisho wa wao ni akina nani, hawakuishia hapo wakatupa kando uzalendo na kujisahaulisha wanatoka wapi. Kwa sababu hiyo wakawaona watanzania wenzao ni mtaji wa kujinufaisha na wakasahau nchi ya uzalendo wao, hata wakatajirisha nchi nyingine wakipatia umaskini kwao. Laiti wangelijua wao ni watanzania na ya kuwa watanzania wengine ni ndugu zao, wakatunza uzalendo wao: wangeijenga nchi yao.

Ndugu zangu watanzania, tazama wanasiasa na wafuasi wao walivyopotoka. Wamesahau kuwa wao ni watanzania na kuwa hata wanaopingana nao kisisasa ni watanzania pia. Kama wangelikumbuka walau hili wangewachukulia kwa heshima. Ni nani asiyejua kuwa watanzania ni watu wa staha? Lakini kwa kupoteza utambulisho wetu hatueleweki ni watu wa aina gani na taifa gani. Tunaenenda kama watu wasio na taratibu. Tumedharauliwa na mataifa mengine kwa kuwa si wazalendo tena. Mzalendo huilinda nchi yake na ndugu zake. Kwa kukosa hilo tunatumika na wageni dhidi ya ndugu zetu na nchi yetu.

Vijana mashuleni wanasoma ili wachukue chao mapema. Haya ndiyo matunda ya mfumo wa elimu usiojenga uzalendo. Hatuthamini bidhaa zetu tena maana hatuna uzalendo.

Bado hatujafika hatua ambayo hatuwezi rudi tena, bado tunaweza kubadilika. Wapenzi ndugu zangu, turudishe moyo wa uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu. Hebu uamue kufanya kitu kwa ajili ya nchi yako na watu wako. Usiangalie faida utakayopata kwanza, bali angalia neema utakayoleta kwanza. Ndugu zangu watanzania, tutangulize utanzania wetu kwanza kabla ya siasa. Hebu tuijenge nchi yetu kwanza, maana sisi ndio wana wa Tanzania. Si mwamerika wala mwarabu wala mganda hata mkenya atatujengea nchi yetu. Wao wana nchi yao nasi tuna Tanzania yetu

vijana wa Tanzania, tuamke na tuanze kujivunia nchi yetu. Hata kama ina matatizo na tujivunie huku tukitafuta suluhu halisi na sio politics. Anza kujivunia utanzania wako maana hata kama ukibadili uraia kimaandishi na kimaeneo, bado Mungu alikuweka Tanzania na daima utabaki Mtanzania.

Niwatie moyo wanawake na wanaume wa nchi hii, nchi yetu ni tajiri na bado tunaweza kuichukua juu. Mungu tusaidie wana wa Tanzania tuamke na kuipenda nchi nzuri sana uliyotupa, tusimame na kujivunia.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania,
nawapenda wote,
HT
Umesema vyema !
 
Kuanzia leo mimi naukana Utanzania. Nakwenda kuchukua uraia wa Somalia. Hii nchi imeshalaaniwa, labda waje Malaika kutoka mbinguni waje watawale. Lakini sio Mtanzania. VIVA JF.
 
Back
Top Bottom