Kanjanja mkware nikatia timu msibani…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,362
aminachifupa9.jpg

Picha haihusiani na habari hii......

Nakumbuka ilikuwa ni mwishoni mwa miaka ya 1990, ndipo tukio hili liponitokea.

Baada ya kupata misukosuko kadhaa hapa jijini Dar, kutokana na mbilinge zangu za kuwania vimwana, nilipata wazo la kubadilisha upepo na kwenda kwa mjomba wangu aliyekuwa akifanya kazi mkoani Tabora. Mjomba alikuwa akiishi eneo moja liitwalo Cheyo, aneo ambalo ni maarufu sana mkoani Tabora kwa sababu wanaoishi eneo hilo ni watu wenye nafasi kidogo, yaani ni kama vile unazungumzia Masaki au Oysterbay kwa hapa Dar. Mjomba alikuwa anaishi na mkewe na watoto wake wawili wa kiume ambao bado walikuwa bado wadogo, wa kwanza akiwa na miaka mitano na wa pili akiwa na miaka mitatu.

Nilipofika mjomba aliniahidi kunifanyia mipango ya kwenda kusoma chuo cha ualimu, lakini kwa kuwa nilikuwa nimechelewa ilinipasa nisubiri hadi mwakani. Hata hivyo nilipata wazo. Kwa kuwa mjomba alikuwa na kamera yake aina ya Yashica aliyoinunua nchini japani alipokwenda kwa mafunzo mafupi, nilimuomba niitumie kwa kupiga picha za mitaani na kujipatia kipato.

Mjomba alinikubalia na nikaanza kazi hiyo mara moja kwa kurandaranda mitaani na baiskeli yake na hiyo Kamera nikipiga picha. Haikuchukua muda nilianza kuwa maarufu pale katika viunga vya cheyo na maeneo ya jirani kwa sababu nilikuwa natoa picha nzuri sana. Umaarufu huo ulinipelekea nianza kubabaikiwa na vidosho, maana ile kujulikana kwamba natokea Dar kulinipa credit ya kuwabadilisha mabinti nitakavyo.

Haikuchukua muda tabia yangu hiyo ya kuchukua vibinti vya shule ikaniletea kisirani ikiwa imebaki mwezi mmoja kujiunga na chuo cha ualimu. Nakumbuka mjomba aliniita na kuniambia kwamba amepata fununu kuwa kuna binti mmoja ambaye baba yake anafanya kazi usalama wa taifa nimempa ujauzito, na hivyo natafutwa na Polisi, aliniambia kwamba muda wowote nitakuja kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kumpa mwanafunzi Mimba.

Taarifa zile hazikuwa nzuri kwangu kwani nilibabaika sana, lakini nilijikaza kiume nisionyeshe hisia hizo za kubabaika kwa mjomba. Nilisimama kidete kukanusha taarifa hizo, lakini mjomba aliniambia kwamba nitakapofikishwa mahakamani ndio ukweli utajulikana, kisha akaondoka kwenda kazini. Huku nyuma shangazi alinishauri nitoroke maana huyo baba wa binti ni mtu wa Musoma, anaweza kunifanyia kitu mbaya.

Ni kweli nilitorokea kwa rafiki yangu na kujificha na siku iliyofuata nilipanda Treni na kurudi Dar na kuepuka kifungo cha kumtia mimba binti wa shule.

Nilipokuwa Dar niliendea na kazi yangu ya kupiga picha baada ya kununua kamera kutokanana fedha nilizojikusanyia nilipokuwa Tabora. Siku zilienda, nikasahau kuhusu tukio hilo na maisha yakaendelea. Katika pilika pilika zangu hizo za kupiga picha, nilipata wazo la kutafuta kitambulisho cha uandishi wa habari ili niweze kujipenyeza kwenye mahoteli makubwa na kupiga picha za matukio mbalimbali ili kujiongezea kipato, wazo hilo nililipata kutoka kwa rafiki yangu mmoja ambaye yeye alikuwa ni mwandishi wa habari na mpiga picha by professional. Alikuwa anatengeza fedha kweli kweli kwa kuhudhuria semina mbalimbali na kujipatia posho achilia mbali kuuza picha.

Ni kweli nilifanikiwa kupata hicho kitambulisho na sasa nikawa najulikana kama mwandishi wa habari, ingawa sikuwa mwandishi wa habari bali mwandishi wa habari feki ambapo hujulikana kwa jina maarufu la Kanjanja.

Ilitokea siku moja ulitokea msiba wa mke wa mzee mmoja ambaye alikuwa ni bosi mkubwa kabisa pale katika wizara fulani. Msiba huo ulivuta watu wengi kutokana na umaarufu wa mzee huyo kiasi cha kutembelewa na viongozi mbalimbali wa serikali. Yule rafiki yangu aliitwa kwa ajili ya kupiga picha, hivyo akaniomba nifuatane naye, ili tuwe wawili. Tulifika pale msibani majira ya mchana na kuanza kupiga picha kila wageni wanapofika hapo msibani ikiwa ni pamoja na matukio mengine madogo madogo.

Nikiwa katika pilika pilika zangu za kupiga picha, nikaitwa na kijana mmoja, nakunieleza kuwa ninaitwa na mzee mmoja aliyekuwa amesimama na binti mmoja. Nilipofika pale nilidhani wanataka kupiga picha, lakini yule mzee aliniambia kwamba hakuniita ili kupigwa picha bali kulikuwa na jambo anataka kuniuliza. Yule binti ambaye awali sikumjua kutokana na kujitanda ushungi alikuwa akiniangalia kwa jicho kali mpaka nikaogopa.

"Samahanin kijana, eti unamjua huyu binti…" yule mzee aliniuliza akinionyesha binti aliyesimama naye.

"Hapana mzee simfahamu kabisa……." Nilimjibu yule mzee lakini yule binti alinikata kalma, "Ina maana leo unajifanya hunijui wewe…….., (alitaja jina langu) wakati uliponipa mimba kule Tabora na kuniharibia masomo na kisha kutorokea Dar ulidhani hatutakutana..? Alisema yule binti wa Kijita huku akiwa amefura kwa hasira na kisha akamgeukia yule mzee na kumwambia, "Mjomba ndiye huyu huyu, na wala si mwingine………."

Nilibabaika kidogo.

Ni kweli, nilipomtazama vizuri yule binti nilimkumbuka sasa, kwani alikuwa amebadilika sana na alikuwa mzuri kweli kweli kutokana na kuoga maji ya Chumvi ya Dar….

"Kijana, huyu binti hana sababu ya kukusingizia, kuwa mkweli tuyamalize haya mambo la sivyo utaozea jela, usicheze na serikali kijana…." Yule mzee aliongea kwa ukali kidogo huku akiwa amenikazi macho…………..

Nikajua sasa mambo yameshaharibika, lakini sikukubali, nilikanusha vikali na kusisitiza kwamba wamenifananisha.

"Naona wewe hutaki suluhu, sasa itabidi tukazungumzie Oystabay Polisi." Alisema yule mzee huku akitoa simu yake ya mkononi ili kupiga simu polisi.

Niliposikia habari ya Oystebay Polisi, nilikurupuka na kutimua mbio zisizo za kawaida, yule mzee aliwaita vijana wake na kuwa amrisha wanikamate lakini wapi, niliwaacha mbali sana, nikawa nime save kutoka kwenye kadhia hiyo.

Baadae nilitafuta wazee na kwenda kuzungumza na yule mzee ambaye alikuwa ni mjomba wa yule binti na kuyamaliza ambapo pia nilipata bahati ya kumuona mwanangu wa kiume. Alikuwa na miaka mitano wakati huo. Nilikuja kugundua kwamba yule binti alijifungua salama kisha akaja Dar kwa mjomba wake na kuendelea na masomo ambapo kipindi hicho waliponibamba alikuwa yuko chuo kikuu akisoma sheria…………..
 
Hahahaaa... Stori tamuuu.. Natamani ingeendelea zaidi..!!

We nawe Neylu vipi..!
Si umeona hapo tuliyamaliza nikiwa na wazee sasa unataka iendelee kivipi....?
 
Last edited by a moderator:
We nawe Neylu vipi..!
Si umeona hapo tuliyamaliza nikiwa na wazee sasa unataka iendelee kivipi....?

Hahahaaa... Iendelee kama vile ulimchukua mtoto ukamlea, au mkaendeleza tena mahusiano na huyo bibie..!! Au ndio ukamtosa jumla.. Au labda ndio mama Ngina wa sasa..! Lol
 
story nzuri na nyenye mafunzo kwenye vichenchede wakuchukua madent hasa wanapo jiona wamekua maarufu
 
Hahahaaa... Iendelee kama vile ulimchukua mtoto ukamlea, au mkaendeleza tena mahusiano na huyo bibie..!! Au ndio ukamtosa jumla.. Au labda ndio mama Ngina wa sasa..! Lol

Mengine nimeweka kwenye mabano.......... LOL
 
Ha ha ha story imekaa uzuri kabisa, ila kama alivyosema mdau ni kama inaendelea vile......... maana umeanza kumsifia tena kuwa amekuwa mrembo kwelikweli baada ya kuoga maji ya chumvi, hapa tunategemea baada ya matangazo tamthilia itaendelea.
 
Ahsante mkuu,mara nyingi natumia simu lakini ninapopata wasaa wa kutumia laptop lazima nifungue jf ili nione notification na hasa tags kutoka kwako. Siku njema
 
hahahahah mama ngina kiboko alikaba koo hilo nusu kufa safi sana safi sana lol hii ulificha wapi toka zamani lol Mtambuzi hahahaah na kazi ya picha ikaishia hapo hapo hahahahahahahahah ila unabahati wewe kama ni mei huchomoki mita na wewe
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nilihisi aunt yako kafanya makeke utorike cse akupenda usomeshwe. Tena nikaanza kunogewa na mtiririko nikijua ndoa ya mkeka lazima ingekuusu! !

Nimependa story bt malizia baasii
 
hahahahah mama ngina kiboko alikaba koo hilo nusu kufa safi sana safi sana lol hii ulificha wapi toka zamani lol Mtambuzi hahahaah na kazi ya picha ikaishia hapo hapo hahahahahahahahah ila unabahati wewe kama ni mei huchomoki mita na wewe

Mama Ngina anajua kuwa mie nilikuwa mkware na ndio maana akanipenda, maana anajua vimwana weshanikinai, na nimeshakuwa kama Fisi aliyeshiba mifupa hata mizoga sitamani.................
 
Kwanza nilihisi aunt yako kafanya makeke utorike cse akupenda usomeshwe. Tena nikaanza kunogewa na mtiririko nikijua ndoa ya mkeka lazima ingekuusu! !

Nipenda story bt malizia basii

Shangazi yangu alikuwa mtu pouwa sana, na ni yeye aliyenisaidia kumaliza hili soo.........
 
Nakukubali sana mtambuzi, na story zako hua zina mafundisho flani, au zinaweza kufanya ukumbuke sehemu, hapa umenikumbusha maeneo ya cheo, national na kiyungi pamoja na ipuli paka kule kanyenye... Tupo pamoja sanaaa karibu nyama choma festival hapa kijitonyama postal
 
Nakukubali sana mtambuzi, na story zako hua zina mafundisho flani, au zinaweza kufanya ukumbuke sehemu, hapa umenikumbusha maeneo ya cheo, national na kiyungi pamoja na ipuli paka kule kanyenye... Tupo pamoja sanaaa karibu nyama choma festival hapa kijitonyama postal

Kumbe mkuu na wewe ni mwenyeji wa kule Tabora aisee..........!
Nilifanya mabalaa kule ile mbaya na niliacha historia, ukifika kule ulizia Mzee wa Yashica wananijua....LOL

Niko home na mama Ngina nawajibika na majukumu ya nyumbani mkuu.................
 
Kumbe mkuu na wewe ni mwenyeji wa kule Tabora aisee..........!
Nilifanya mabalaa kule ile mbaya na niliacha historia, ukifika kule ulizia Mzee wa Yashica wananijua....LOL

Niko home na mama Ngina nawajibika na majukumu ya nyumbani mkuu.................
sawa sawaaa ulikua unasafishia picha maeneo ya diamond au .....? dudu ulikua unamkumbuka.....
 
Story nzuri sana! Ila nahic haijaisha! Au ndo mama Ngina ndo huyo mama yetu uliyemkimbia!
 
Ha ha ha story imekaa uzuri kabisa, ila kama alivyosema mdau ni kama inaendelea vile......... maana umeanza kumsifia tena kuwa amekuwa mrembo kwelikweli baada ya kuoga maji ya chumvi, hapa tunategemea baada ya matangazo tamthilia itaendelea.

Hahaa, Matangazo yameisha. Mtambuzi endelea tafadhari
 
sawa sawaaa ulikua unasafishia picha maeneo ya diamond au .....? dudu ulikua unamkumbuka.....
manoah nishasema mimi nilikuwa mpiga picha bana.....
Huyo Dudu si alishafariki? au taarifa nilizopata hazikuwa sahihi?
 
Last edited by a moderator:
Story nzuri sana! Ila nahic haijaisha! Au ndo mama Ngina ndo huyo mama yetu uliyemkimbia!
Yegoo, mama Ngina ni chombo kipya, yule keshaolewa zamaani ingawa nilitaka kukumbushia akaniwekea mkwara..........
 
Last edited by a moderator:
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom