masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
kwa muda mrefu sasa Kanisa La Moravian Tanzania (KMT), limekuwa katika mgogoro usioisha.
Kiini cha mgogoro huu ni ugomvi wa madaraka na mapato ndani ya kanisa hili kongwe.
Kanisa la Moravian asili yake ni Nyanda za Juu Kusini ambako lili chanua na kusambaa hadi Mikoa ya Tabora na hata sehemu za Katvi , Iringa na hata Mpanda.
Kinachotusikitisha waumini wa kanisa hili ni huu ugomvi ambao kiini chake ni fedha.
Tukumbuke kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea Pasaka,kipindi alichosulubiwa Mwokozi wetu Yesu Kristo,
ni fedha vile vile zilizo msaliti Bwana Yesu.
Hili somo nafikiri halijatua vema kwa wachungaji wetu ndani ya kanisa hili kongwe, fedha , asili ya tamaa ya kimwili ndio inalisambaratisha kanisa hili.
Pamoja na tamaa za fedha, kitu kinachojitokeza ni uvivu wa wote wanaohusika.
Mtu, uwe mchungaji au m-deacon, kama unslaumiwa kwa ajili ya tamaa zako ni heri tu kujiuzuru ili kanisa lisonge mbele kwa amani.
Lakini kwa sababu ya uvivu na tamaa sijasikia yeyote amejiuzuru,
Tukumbuke kuwa kujiuzuru ni kujitolea kwa kiwango cha chini kabisa ukilinganisha na Bwana wetu Yesu Kristo alivyotoa uhai wake kwa ajili ya dhambi zetu.
Kwa haya yanyoendelea katika Kanisa La Moravian Tanzania, waumini tusali sana ili virusi vya mwovu shetani viweze kudhibitiwa na Roho Mtakatifu.
cc Bujibuji , Baba V

Last edited by a moderator: