Kanisa lavamiwa: Mapadre wapigwa risasi Iringa

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2010
Posts
230
Reaction score
57
eofrey Nyang'oro, Iringa

MAPADRI wawili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, Jimbo la Iringa, wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kutokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuwajeruhi kwa silaha za jadi na bunduki, baada ya kuvamia nyumba wanazoishi.

Paroko wa Kanisa hilo Angelo Burgio kutoka Italia (60) na msaidizi wake Herman Myala walikumbwa na mkasa huo usiku wa kuamkia jana.

Padri Burgio alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mbili kifuani na kucharangwa mapanga, msaidizi wake Padri Myala alijeruhiwa kwa
mapanga na kuburutwa chini kwenye ardhi.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku moja tangu kuvamiwa kwa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa lililopo eneo la Kihesa mkoani humo, ambapo mlinzi wa kanisa hilo, Batholomea Nzigilwa (65) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Nzigilwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, huku hali yake ikielezwa ikiwa ni mbaya.

Watangaza msamaha Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.

Akizungumza kwa tabu, padri huyo alisema majambazi hao walifika eneo la Kanisa la Kihesa saa tano usiku wakiwa na silaha mbalimbali
za jadi na bunduki.

Alisema baada ya kumshambulia msaidizi wake, walimfyatulia yeye risasi kifuani wakati alipofungua mlango na kutaka kukimbia.

"Mimi baada ya kuwasikia nilifungua mlango kwa lengo la kutaka kukimbia ili nijinusuru, lakini hamadi wakanifyatulia risasi kifuani. Nilianguka chini na walipoingia ndani walichukua fedha taslimu Sh3.5 milioni zilizokuwa chumbani kwangu na kisha kunikata na panga
kichwani, " alisema Burgio.

Hata hivyo, padri huyo alisema, "Sisi tunawasamehe. Mimi na mwenzangu tumewasamehe tangu walipofanikiwa kutushambulia na kukimbia. Tunawaombea msamaha kwa Mungu kwani yeye ndiye anayejua," alisema Padri Burgio.
 
I hate this sasa............. too much,
 
Kikulacho kinguoni.........!, Hivi wale wachungaji waliowapeleka wenzao mahakamani imefikia wapi?
 
MUNGU awatie nguvu na wapone na hata wapone mapema!
 
Mnajuaje kama waumini wa hapo hapo kanisani wamefuata sadaka zao.Maswala ya kuwasingizia waislamu mkome.Majambazi ni hao hao wagalatia wenzenu
Ndugu yangu, kama unawajua 'wahuni' basi na hao watakuwa ni 'wahuni' tu. Wahuni wengine waliovamia, kuharibu na kuiba mali za Kanisa tunajua kesi zao zinaendelea. Ila hata hawa 'wahuni' na wenyewe watadakwa tu siku itakapofika...
 
Nawapa pole watumishi wa Mungu waliojeruhiwa katika matokeo hayo.

Hilo shambulizi halina uhusiano kabisa na tofauti za kidini kati ya wakristo na waislam. inaonekana kana kwamba kuna
kutokuelewana miongoni mwa waumini wakristo wenyewe kwa wenyewe. Hiyo ni hujuma na inabidi waangalie chanzo
ni nini wakifanyie kazi ili maafa zaidi yasitokee!
 
Ukweli utajulikana tu...
 
Wangewaua wote, hao akina bagio ndio waoleta cocein kwa mgongo wa kanisa
 
Pole kwa walopatwa na maswaibu yote...Mungu atawaponya na kupata uzima tena...
 

Naomba ufafanuzi, je hao mapadri wa Parokia ya Isimani iweje wavamiwe eneo la Kihesa?
Waliofanya hivyo ni wahuni na watu wanaotaka hela kwa njia haramu. Watakachokipata itakuwa funzo kwa wengine.
 
Nawapa pole sana waloathiriwa na unyama huo. mungu awajalie afya njema ili warejee majukumu yao. uchunguzi wa kina ufanyike ili kubani watuhumiwa wa mkasa huo.
 
Nafikili Mwandishi kajichanganya..Juzi walivamia Jimboni Kihesa,wakati jana Isimani Parokiani!Padre Angelo ni wa muda mrefu sana...ameishi Isimani toka miaka ya 1970's!amejenga shule,zahanati na kituo kikubwa sana cha watoto Yatima kilichofunguliwa na Kikwete,alikuwa amebakiza mda mchache arudi kwao Agrigento-Italia baada ya kukaa Isimani zaidi ya miaka 35..sherehe za kumuaga zilishafanyika,lakini majambazi nao wamemuaga kwa namna yake
Naomba ufafanuzi, je hao mapadri wa Parokia ya Isimani iweje wavamiwe eneo la Kihesa?
Waliofanya hivyo ni wahuni na watu wanaotaka hela kwa njia haramu. Watakachokipata itakuwa funzo kwa wengine.
 
Wangewaua wote, hao akina bagio ndio waoleta cocein kwa mgongo wa kanisa
Laana hii ikutafune wewe mwenyewe haraka iwezekanavyo hadi hapo hiyo roho ya ibilisi inayoongea ndani mwako itakapokoma!!!!
 
Poleni sana, hebu hakikisheni nitashangaa ikiwa hao majambazi si dini nyingine
 
I hate this sasa............. too much,

Kwa kamanda wa Iringa ingekuwa ni maadamano ya cdm angeweza !! Sina hakiaka kwa hili !!! na ingekuwa ulaya mtu angejiuzulu na kupisha uchunguzi!! lakini kwetu anapata promotion!! kabakiza mwaka kustaafu pengine alirudisha nyuma miaka yake kwa maana kachoka sijui!!
 
Mungu ni muweza ya yote, atawaponya na kurudia katika kazi yao ya utumishi wa bwana. Kwenye taarifa ya ITV ya saa 2 imesema yule mlinzi wa jimboni Iringa hali yake si nzuri amepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…