Kanisa la ufufuo na uzima linaandaa rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa la ufufuo na uzima linaandaa rais?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpingauonevu, Mar 12, 2012.

 1. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Wapendwa mimi bado ninabumbuwazi na hili kanisa la kurudisha misukule. kwanza walipoanzisha hiyo program yao ya kuita wanasiasa wakawaita kambi ya Sitta na mwakiembe. Sera zilizopelekwa hapo ni sumu na ufisadi. Wa mwisho kutembelea hapo ni Nape Nnauye. Maswali ninayojiuliza
  1. Mungu anaweza kudhihakiwa kwa kiasi hiki? kama kanisa linamuandaa rais Na waislam nao wakamuandaa na wapagani hii nchi itatawalika?
  2. Busara za viongozi huwa ni wale walioko ccm tu? yaani CDM, CUF au NCCR hawana viongozi wenye hekima?
  3.kwa kuifahamu biblia, Mungu huwa hachagui mtu maarufu na mwenye uwezo (alimchagua daudi kuwa mfalme akiwa mdogo, alimchagua mariam maskini kati ya mabikira waliokuwa maarufu) - sasa leo kumchagua mtu maarufu kunaendana na andiko?
  4.Kwa sababu hawa mitume na manabii wanaopenda sifa huwa hawapendani (kwa sababu wote ni wapenda sifa kama baba yao lusifa)(anayempenda Mungu humpenda jirani yake) - inamaana Kakobe na Mwingira nao wanarais wao? (angalau kakobe aliaibika baada ya mrema kuchina)
  5. Je? hao wakina sitta (kumbuka sitta ameoa wanawake wawili) wanaishi kulingana na maadili ya kanisa?
  6. au ndio kuwajibu EL na RA kwamba wao wakienda lutherlan na Roman wao wanaenda kwa wapentekoste?
  Wapendwa naomba mnisaidie kushangaa!
   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Drug Dealers tu hao! Achana nao!

   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280

  mambo mengine usiyaweke maanani. Hiyo siyo institution, ni mtu na ujanja wake. There is no way anaweza aka-influence uchaguzi wa Rais. I can dare to say ni kundi la shetani linatafuta survival kwa migongo ya tulio na shida na shida zetu hazina majawabu. We are seeking solutions in super natural powers!!!!
   
 4. kiagata

  kiagata Senior Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  kuandaa Rais siyo rahisi,makanisa fulani walimwekea mikono Mh.Mrema kuwa ni chaguo la MUNGU akashindwa na Mchungaji KABKOBE alimwekea fulani kuwa Rais akashindwa.Sasa waache waombeane,wachaguane kabla ya uchaguzi mwisho wata prove fairure.
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hata mie nashangaa kanisa limeanza juzi tu hata miaka 8 halina lakini kikawa nikikundi cha wanasiasa fulani . Kwa mara ya mwisho nimemuona Sitta kwenye Lori akienda kuoga Baharini na wafuasi wa kanisa hilo
   
 6. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Umenigusa hapo inamaana alienda kubaatizwa tena! hahahah labda wamempa jina jipya!
   
 7. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuliangalia upya swala la uhuru wa kuabudu. (pamoja na kuwa ni haki ya kikatiba). Tujiulize KWA NINI SIKU HIZI NDIO WANAIBUKA WATU WANAOJIITA WAPONYAJI? KWA NINI ZAMANI HAWAKUWEPO? Hawa watu wanatafuta ajira kwa kucheza na akili za watu, wanawaibia kwa njia ya udanganyifuna kuwaharibia kabisa maisha yao. Hawa siku hizi wanajiita maaskofu na manabii (wanajipa wenyewe uaskofu na unabii), Uaskofu ni cheo unachopewa na kiongozi mkuu wa dhehebu na kwa kufuatautaratibu/mchakato maalumu, unabii unapewa na mwenyezimungu mwenyewe.
   
 8. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  halafu hawa jamaa hawalipi kodi kabisa na serikali haifanyii ukaguzi mahesabu ya mashirika ya kidini hivyo kuwafanya hawa jamaa wakwasi vibaya sana!
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye namba 3; umaarufu unaupimaje?, je; Mungu anapima umaarufu wa mtu kwa vigezo gani?, unajuaje kuwa Daudi na Bikira maria hawakuwa maarufu.
   
Loading...