Kanisa Katoliki Ufilipino latoa waraka kuhusu Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa Katoliki Ufilipino latoa waraka kuhusu Mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paschal Matubi, Mar 21, 2010.

 1. P

  Paschal Matubi Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Chanzo Cha Habari: Gazeti la TUMAINI LETU
  Mmiliki wa Gazeti: Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la D'Salaam
  Toleo: 00302
  Tarehe: MARCH 19, 2010
  Ukurasa: 07


  Wakati wananchi wa Philipines wakijiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wa Serikali nchini huo baadaye mwaka huu, Kanisa Katoliki limetoa waraka wa kichungaji likiwataka waamini na wananchi kwa ujumla kuwa makini na wanasiasa wanaotumia fedha kupata ili kupata uongozi.

  Waraka huo wa kichungaji ulioanza kusambazwa Jumapili liyopita umetolewa na Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Manila Mwadhama Gaudensio Kardinali Rosales na kusainiwa na maaskofu wengine kumi na tano wa nchi hiyo.

  Katika waraka huo, Kardinali Rosale alisema kuwa ni vyema wananchi wakawa na tahadhari kubwa na wanasiasa wanaotumia fedha nyingi wakati wa kampeni kwa kuwa wanasiasa wa namna hiyo hawana lengo zuri kwa wapiga kura wao.

  Aliwataka wananchi kupiga kura kwa uhuru na kuchagua viongozi bila kujali shinikizo la aina yoyote likiwemo la fedha ili kuwapata viongozi wa nchi watakaowajibika na kuwatumikia wapiga kura wao.

  Kardinali Rosale alisema ni vyema kila mpiga kura akasoma kwa makini maelezo binafsi ya wagombea na kuzipima kauli zao badala ya kuangalia kiasi cha fedha kinachotumika katika kampeni.

  Aidha waraka huo wa maaskofu umezitaka mamlaka zinazohusika nchini humo kuhakikisha uchaguzi nchini humo unafanyika kwa misingi ya kuzingatia demokrasia bila kuwepo vitisho.

  Uchaguzi nchini Philipines utafanyika Mei 10 mwaka huu.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mzee unapoandika heading uwe unaweka iliyokamilika, mimi Binafsi nilijua ni Wakatoliki wa Tanzania.
  kichwa chako cha thread kilipaswa kuwa hivi

  Kanisa Katoliki Philipines latoa waraka kuhusu Mafisadi
   
 3. P

  Paschal Matubi Member

  #3
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25


  Hakuna Kanisa Katoliki Tanzania, Philipines, Italy au Germany.

  Kanisa Katoliki ni Kanisa Katoliki tu.

  Katekism ya kanisa Catholic inasema hivi:

  The Church is One, Holy, Catholic, and Apostolic
  ambayo kwa kiswahili inatafsiriwa hivi:
  Kanisa ni moja takatifu, Katoliki la kitumeeee.

  Vilevile lengo ni kuwakumbusha wale wapiga debe waliodhani nyaraka hizi ni jambo geni kwamba linafanyika nchi zote liliko kanisa Katoliki na huko hutawasikia wanapiga kelele zozote kwani hawana ugeni na nyaraka hizo.
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni ubishi ambao sio wa lazima, mbona Pengo anaitwa askofu wa Jimbo kuu la Katoliki Dar es Salaam? Kuna ubaya gani kuonyesha sehemu?Ushauri uliotolewa ni halali na ulichotakiwa kufanya ni kusema nashukuru.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  mimi wala sijazungumzia umoja wa kanisa Katolic, pamoja na kelele zote lakini nadhani hujuhi chochote kuhusu Ukatoliki, HICHO KICHWA CHA HABARI KIMEKUWA KAMA CHA GAZETI LA UDAKU, MAANA MTU ANAKUWA NA SHAUKU YA KUSOMA AKIJUA NI HABARI FULANI LAKINI MWISHOWE ANAKUTA NI KITU TOFAUTI
   
 6. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii nayo imekaaje? yaleyale.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280

  yaah nadhani hajuhi kuwa hipo tofauti ya Tanzania na Philipines, huwezi kusema Pengo ni Cardinal wa Manila,
   
 8. P

  Paschal Matubi Member

  #8
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Katika Kanisa Katoliki hakuna Kadinali wa D'Salaam, Manila, Toronto, Washington au Kampala. Makadinali wote ni wa kanisa Katoliki na wote wana Parokia zao kule Roma zinaitwa Titular Church.

  Polycarp Pengo ni Kadinali wa Kanisa Katoliki na si kadinali wa D'Salaam au Tanzania.Labda kama unataka kusema kwamba Pengo ni mzaliwa wa Tanzania amavyo unaweza kusema Papa Benedict XVI ni mzaliwa wa Ujerumani.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hapa Mkuu umechemsha..Kubali kwamba umekosea na umeandika kwa lengo maalumu..Ni kweli kabisa kanisa katoliki ni moja tena takatifu la mitume ila ni muhimu kutofutisha habari za Tz na nchi nyingine..Hata mimi nilifikiri hapa kwetu nikashangaa mbona sina habari.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwa hili best sina swali manake uko well versed. Thanx!
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Mar 21, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  Halafu wangekuwa Katoliki Tanzania so what?

  epukeni issue za dini dini nchini mwetu ala!
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Waberoya tayari kashaibuka bado Tumaini.lazima aje ajibu hili....Wanawaogopa wakristo kama sijui nini vile,sijui wamewafanya nini....
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  NAOMBA KUKUULIZA ACCORDING TO WARAKA WA PAPA ULIOMTOA KILAINI DAR, ulimtaja Kilaini kuwa ni nani kwa sasa?
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ..and what exactly is your problem??
   
 15. P

  Paschal Matubi Member

  #15
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Kilaini hajawahi kuwa Kadinali na hata akiwa akiteuliwa sasa hivi kuwa Kadinali huwezi kusema ni Kadinali wa Bukoba au Tanzania.
  Waraka kama unavyouita ni taarifa ya uhamisho toka Vatican kwamba Kilaini sasa anakuwa askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba.

  Kumbuka wewe umeleta mada ya kuuliza ukadinali wa eneo. Pengo ni askofu mkuu wa D'salaam na hyo ninaikubali nusu na nusu nitakueleza kwenye aya ifiatayo.

  Ni kweli askofu kama Pengo (Dar), Tmanywa (Bukoba) tunasema ni maaskofu wa majimbo hayo. Lakini kimsingi na kiusahihi wote hawa ni maaskofu wa Kanisa Katoliki isipokuwa tu wao wamekabidhiwa jukumu la kuongoza majimbo waliyo nayo.

  Kama hukubaliani na mimi basi turejee Sheria za kanisa kuhusu maaskofu hawa zinasemaje.

  Sheria za Kanisa au Canon Law zinapatikana dukani pale St. Joseph Dar tena kwa bei nafuu. Ukinunu utaona Can. 376 inasema hivi:
  Bishops to whom the care of a given diocese is entrusted are called diocesan Bishops; the others are called titular Bishops.

  Kwa hiyo utaona kwamba huyu ni askofu wa Kanisa Katoliki lakini yeye jukumu lke amekabidhiwa jimbo la waumini.

  Na Methodius Kilaini ukitaka kumuita kiusahihi utamuita askofu wa Strumniza yaani Titular Bishop of Strumniza na si askofu wa Bukoba kwa sababu Bukoba amekabidhiwa askofu Timanywa.

  Mjadala wa Kilaini tuliujadili vya kutosha hapa jamvini tukasema yeye ni wale ambao kifungu hiki kinawakewa kama askofu wa Kanisa Katoliki ambaye hakukabihdiwa jimbo kama jukumu lakini kakabidhiwa usaidizi kama wengine walivyokabidhiwa majukumu mengine huko Vatican, na kama askofu Novatus Rugambwa mtanzania wa kwanza kukabidhiwa ubalozi wa Papa huo Angola wiki iliyopita.

  Huwezi kumuita Rugambwa askofu wa Angola kwa sababu anafanya kazi huko.

  Karibu tena kwa hoja nyingine.
   
 16. P

  Paschal Matubi Member

  #16
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Ni kweli kwamba nina lengo maalumu. Na lengo langu ni kuwaletea kilichoandikwa na gazeti la TUMAINI LETU bila kubadilisha nukta kwani nahisi wengi humu si wasomaji wa gazeti hilo.

  Nadhani TUMAINI LETU wanaweza kuulizwa wana lengo gani kuandika vile maana heading nime-copy and paste.

  Namba za simu za TUMAINI LETU ni 075-4305514 ambao pia ni wamiliki wa Redio na TV Tumaini.
   
 17. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Heading haikuwa sahihi hata kidogo kwa mujibu wa contents zake.
  Ukweli ubaki kuwa ukweli unapokosolewa
  JF twajifunza mengi, apologies huwa ni za muhimu unapokuwa umewarusha kimanga wa membaz
   
 18. P

  Paschal Matubi Member

  #18
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25

  OK. Ninakubali kukosolewa na ninajisahisha kwa kuweka maneno sahihi yaliyotumika kwenye gazeti la TUMAINI LETU.

  Waliosoma gazeti hilo wataona nilitakiwe niweka heading kama ilivyo gazetini kwani heading inasema KANISA LATOA WARAKA KUHUSU MAFISADI.

  Mimi niliongeza neno KATOLIKI kwani nigeishia na mimi kusema neno kanisa wachangiaji wasingejua ni kanisa gani maana hata protestants nao ni kanisa.
  %
   
 19. M

  Mdanganywa JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 542
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Umewaweza waliokuwa wanang'ang'ania uombe apology ya heading kana kwamba wewe ndiye editor wa hilo gazeti.


  Mimi nimelisoma na wenzangu wawili na hakuna kati yateu aliyeona tatizo kwenye habari hiyo hadi kufikia kuomba gazeti liwaombe radhi wasomaji.


  Afterall wasomaji wakuu wa gazeti hilo ni wakatoliki sasa kama linakukera acha kulisoma nunua MWANANCHI, TANZANIA DAIMA, MTANZANIA na mengine kama hayo.
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280

  maana kuna thread zinaanzishwaga humu na heading kama KWA WANAWAKE TU, KWA WANAUME TU, KWA WANYAKYUSA TU NK,

  NADHANI KWA MAELEZO YAKO HAPO KWENYE NYEKUNDU NI BORA MNGETUANDIKIA KWA WAKATOLIKI TU, WALA KUSINGEKUWA NA HAYA MANENO
   
Loading...