Kanisa katoliki ndio limetufikisha hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa katoliki ndio limetufikisha hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Taifa_Kwanza, Feb 8, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika Uchaguzi uliomuingiza Mkwere Madarakani Mwaka 2005, Kanisa katoriki lilijiingiza kwenye Siasa za uchaguzi Miguu yote miwili na kuwalazimisha Watanzania Wamchague Kikwete kwa sababu ni Chaguo la MUNGU. ni kutokana na nguvu ya UONGO huu ndio maana Kikwete aliingia madarakani kwa ushindi ambao yeye, chama chake na kanisa katoriki waliuita wa kishindo.

  Yes, Kanisa katoriki limetufikisha hapa kama taifa, Kanisa Katoriki lilijua toka Mwanzo kwamba Kikwete sio chaguo la Mungu hasa Mungu ambaye habari zake zimeandikwa kwenye Biblia, kwamba yeye ndio THE AUTHOR wa habari zilizo andikwa mle, Mungu aliyeiandika Biblia ni Mungu wa Amani na Upendo, ni Mungu wa Haki, ni Mungu wa Utaratibu sio mafarakano na sintofahamu kama tunazofanyiwa leo na Kikwete.

  Kama Mungu alishiriki katika uchaguzi wa Mwaka 2005, angeweka mtu ambaye hata kama leo angekuwa na viwango vya utendaji kama wa kikwete, basi watanzania wangekuwa na huzuni "kwamba Mbona kiongozi wetu amebadirika", Watanzania wangemlilia Mungu alimrudishe kiongozi wao katika mstari,na Mungu angetumia fursa ya Uchaguzi uliopita kumpiga chini.Ushahidi wa Mahusiano ya Mungu na Viongozi uko namna hii kama ilivyoandikwa kwenye Biblia.

  Katika Uchaguzi wa Mwaka 2005 na hata wa Mwaka 2010, Kikwete alitumia pesa za wizi katika Uchaguzi,
  Aliiba Pesa BOT, Mwaka huu vivyo hivyo, mara zote mbili ametumia Uganga, Uchawi na Ushirikina katika Kampeni zake, Haya yote kanisa katoriki liliyajua toka Mwanzo, Kikwete alianza Majungu toka mwaka 1995 ambayo leo yanakisumbua chama cha mapinduzi utafikiri ni chama kinda,uovu ulitapakaa katika harakati zake zote za Urais. Haya Yote kanisa katoriki liliyajua.Je Mungu anaweza kuwa na ushirika na mtu kama huyu?

  Kanisa katoriki halijawahi kuwaomba msamaha watanzania mpaka leo,halijawahi kubadilisha kauli yake mpaka leo, liko kimya kabisa, kipindi cha Kampeni za mwaka 2010 baadhi ya wananchi walihoji, Wapi mvuto wa Kimungu wa Mkwere? Kanisa halikutoa maelekezo. Bila Kanisa katoriki Kikwete asingeingia Madakani mwaka 2005, na wengi tulijua kwa haki ama kwa hila angeendelea kuwa madarani kwa miaka mitano zaidi.

  Hapa tulipofika Kanisa Katoriki linahusika Moja kwa moja. KWA NINI KANISA KATORIKI LILITUDANGANYA?
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Ndo maana tumelitosa 2010 lilipotutaka tumchague Padri Slaa
   
 3. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Rubbish..!!
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi sikumbuki kama kanisa katoliki kama taasisi liliwahi kuwasihi watanzania kumchagua mtu fulani; ninachojua kanisa katoliki wakati wote limekuwa likiwahasa watanzania kumchagua mtu aliye muadirifu. Hili la kumwita Kikwete chaguo la Mungu alilitamka askofu Method Kilani wakati huo akiwa askofu msaidizi wa jimbo la DSM. Kauli hiyo ilikuwa inawakilisha mawazo yake mwenyewe kama raia yeyote.
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  crap
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmh, so so! kuna hoja ndani lakini IMEPINDA
   
 7. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata lugha haujui vizuri, linaitwa kanisa katoliki, na siyo katoriki. Nakuomba uache uzushi na uzandiki. Kuwa mkweli.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,403
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe unayejiita taifa kwanza ............Hao kanisa katoliki wangekuambia ukate kichwa chako ungefanya hivyo..........???
   
 9. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona Slaa alipokuwa Sisiem ukatoliki wake au upadre wake haukuonekana? Ni kweli upadre unaonekana unachangaywa na siasa au 'umetumwa' na kanisa ukiwa nje ya ssm. Kuna mbunge namjua alikuwa padri na sasa ni mbunge wa ssm na sijawahi kusikia akituhumiwa katumwa na kanisa.
  :clap2:
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho wewe.
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hata kama walikuwa right by that time, who knows? Sauli au Daudi alikuwa ni chaguo la Mungu ingawa baadaye alikuja kukengeuka, hivyo mabadiriko ya mtu si sababu ya kukataa uhalisia wa zamani uliokuwepo.
  Tuna Shetani, kwani Mungu alimuumba Shetani akiwa kama shetani? kama alijua kuwa atakuja kuwa Shetani nadhani asingemuumba, ila alikengeuka mwenyewe baada ya kuona utukufu na mamlaka aliyokuwa nayo vikamlewesha na kujivuna mwisho akaanguka.
  Mungu aliumba malaika.
   
 12. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  mmh! Hapa ninaweza nikafungwa au nikalaanika nitarud bidae
   
 13. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,403
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  Sote tunafahamu kuwa Dk. Slaa kwa muda wa miaka kumi na mitano amekuwa ni mbunge wa Jimbo la Karatu na ni jambo linalojulikana kuwa aliingia katika siasa akitoka kuwa padri wa Kanisa Katoliki akiwa ameshika nafasi mbalimbali kuanzia jimboni kwake hadi makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki pale Kurasini.
  Alipotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM kule Karatu, CCM ilimuengua kwa kumpendekeza mtu mwingine na Dk. Slaa akaamua kuhamia CHADEMA wakati huo kikiwa bado ni chama kichanga kabisa. Kuingia kwake CHADEMA kulidhaniwa kutakuwa ni mwisho wake kisiasa na wananchi wa Karatu baada ya uchaguzi mmoja tu wangemtema na kurudisha CCM. Miaka kumi na tano imepita na Dk. Slaa amekuwa ni mbunge wa Karatu huku chama chake kikishika na Halmashauri ya Karatu mojawapo ya halmashauri chache ambazo zimeshikiliwa na upinzani.
  Katika kipindi chote hicho cha miaka kumi na mitano suala la kuwa Dk. Slaa alikuwa ni padre halijawahi kuwa jambo la kuwakwaza watu. Aliposimama kuwanyoshea vidole mafisadi bungeni alimtaja miongoni mwao mtu ambaye alikuwa ni Mkristu, Gavana David Balali.
  Suala la kuwa aliwahi kuwa Padri halikuwa suala kubwa. Na aliposimama pale Mwembe Yanga alitaja majina ya watu mbalimbali kuwatuhumu vitendo vya ufisadi. Hakukuwa na mtu yeyote aliyesimama na kusema ‘imekuwaje mbunge aliyewahi kuwa padri kufanya jambo hili"?
  Ukweli ulibakia ni kuwa Watanzania hawakujali dini ya Dk. Slaa wala hali yake ya upadre. Watanzania walitamani na hatimaye walipata mwanasiasa mwenye ujasiri wa kuita embe embe, chungwa chungwa, na kitunguu kitunguu! Hadi pale chama chake kilipompendekeza kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania. Hapo ndipo tulipoona wabaguzi wa kidini wakianza kujitokeza na kufanya suala la upadri wa Dk. Slaa kuwa hoja.

  source: Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?
   
 14. c

  chumakipate Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ilikua kauli ya Methodius Kilaini siyo kauli ya kanisa.Na hata kama Kilaini asingetamka maneno hayo je, moyo wa Kikwete ungebadilika?Hiyo ni tabia yake hata kama waliosema wangekuwa malaika sembuse masheikh?
   
 15. n

  nyantella JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ndiyo kanisa gani hilo?
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wewe kiswahili inaonekana ulipata F+
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Sio mkurya huyo!
   
 18. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani wana JF, hapa ni mahala pa kujufunza na hoja zote zina umuhimu kwa namna moja au nyingine. Wakatoliki wanaamini kuwa, sauti ya watu ni sauti ya Mungu au kwa kilatini "VOX POPULI VOX DEI". Hilo lilitamkwa na Askofu mmoja ambaye aliwahi kuzomewa kanisani na wakatoliki waliokuwa wamekuja kanisani {na walivaa kanga za ccm} baada ya kuwauliza, hivi kweli mmeamua kuuza utu wenu kwa shs elfu 2???? Walimzomea akakatisha mahubiri akaendelea na sala zingine.

  Baada ya uchaguzi mwandishi mmoja mfukunyuku au mwenye kumbukumbu na mfuatiliaji alimwendea Askofu yule yule akitaka maoni yake kuwa JK Ameshinda kwa asilimia 84%. Alijibu kuwa "sauti ya watu ni sauti ya Mungu, na kama unajua logic, then, chaguo la watu {84} ni chaguo la Mungu. Hapo ni mambo ya imani, unaruhusiwa kuwa na imani nyingine.

  Swali hilo hilo aliulizwa Kofi Annan alipokuwa kibosile wa UN, Mzee, Mwanachama wako mmoja tanzania ameshinda kwa kishindo asilimia 84, ni nini maoni yako, alijibu kifupi, "Atawalipa nini watu hao kwani inaelekea watu wana matumaini naye makubwa sana. Asilimia hizo ni nyingi sana. Atakuwa na kazi kubwa ya kulipa matarajio. Yanayotokea ni ushahidi wa majibu yote mawili.
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mbona watu wanapenda kupotosha Habari sijuhi ni kwa makusudi ama ni kwa kutafuta sifa
  Kanisa KAtoliki Tanzania halijawahi kutamka JK kuwa ni Chaguo la Mungu, Kama hiyo kauli ilitolewa na Viongozi wa kikatoliki basi ilikuwa ni misimamo na maoni yao labda kiimani ama ni kwa utashi wao binafsi,
  Hivyo Haikuwa kauli rasmi ya Kanisa Katoliki, kitu kilicho rasmi ni kama ule Waraka wa Kuwaelimisha watu kuhusu Mambo ya uchaguzi
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  No wonder
   
Loading...