Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Hili sasa naona linako elekea sio kuzuri kwani limevaa sura ya kisiasa zaidi kuliko ukweli wenyewe wa kucheza na IMANI YA WAKRISTO WA KIKATOLOKI. Kwanini muhusika aliye cheza na imani za wenzie asiombe msamaha kikaeleweka????
Huyo aliyesema hayo ni muisilamu, hawezi kuzuiwa kutamka hayo kwani hiyo si imani yake, na ndio maana halazimishwi kuomba msamaha. Ila kanisa linawachukulia hatua wale wamumini wake tu waliokuwa wakimsapoti alipokuwa anaongea kashfa hizo. hapo inabidi ieleweke kwamba kama wangelikuwa waumini wa hata Ukristu katika dhehebu jingine mbali na katolik, jimbo lisingeweza kuwazuia. Cha msingi ni hao waliopewa ban waombe msamaha kama walivyoelekezwa, tatizo lao ni ukaidi.
 
Huyu mwandishi achukuliwe hatua za kisheria,kwa kuchochea mfarakano wa kidini nchini.Hii ni hatari sana.Sidhani kama ana maadili ya uandishi wa habari.
 
Kabla hujafa hujaumbika na ukikikataa ya Mussa utayapata haya!
Tulizoelea kuyasikia haya kule Pemba kati ya CCM na CUF lakini hili la Kanisa kuwatenga waumini kweli tumekwenda mbali.

Mbona tuliyoyazoea kule sasa tuna yaona hapa?

Si bora hao wakatoliki waliowatenga waumini wao wanaokubaliana na mtu aliyeukufuru ukristo kuliko DINI nyingine zinazotoa hukumu ya kifo kwa aliyekufuru! Unamkumbuka mwandishi wa AYA ZA SHETANI? hadi leo hawezi kutembea mtaani!
 
Huyu mwandishi achukuliwe hatua za kisheria,kwa kuchochea mfarakano wa kidini nchini.Hii ni hatari sana.Sidhani kama ana maadili ya uandishi wa habari.

Atachukuliwa hatua na nani wakati haohao wanaotakiwa kuwachulia hatua is like wanapenda/wanachochea/wanashabikia udini??????????? Na sababu ni ili tu chama kimoja kionekane kina mwelekeo wa dini fulani. Lengo lao kukiharibu bila kujali madhara mengine!!!!!!!!!!!!!!!

Zitakapotokea fujo somewhere na watu wakauana nadhani itakuwa furaha ya hawa wachochezi wa udini maana ndo lengo lao.Vita vya kidini ni vibaya sana - usicheze na imani za watu.. Hawa wanasiasa wanaudhi sana kuingiza dini katika siasa just because Dr. Slaa alishawahi kuwa Padri.. Huu ni uzandiki, wehu, uuaji, na uchafu mwingine usioweza kutamkika. Sh**zi zao.
 
Habari leo imenifanya nichukie magazeti karibu yoote. What a trash....
Trash!!? which one ... Kanisa katoliki kuendekeza udini katika mambo ya demokrasia ama magazeti kuripori udini wa viongozi hao wa katoliki???.

Cha msingi ni kuukubali ukweli huo na kutafuta jinsi ya kuziba ufa huo wenye harufu mbaya kwa msakabali na umoja wa taifa hili.
 
Si bora hao wakatoliki waliowatenga waumini wao wanaokubaliana na mtu aliyeukufuru ukristo kuliko DINI nyingine zinazotoa hukumu ya kifo kwa aliyekufuru! Unamkumbuka mwandishi wa AYA ZA SHETANI? hadi leo hawezi kutembea mtaani!

Dini gani hizo mkuu?
 
 
Source: HabariLeo, Majira ?....haya ni ya Serikari ya CCM au majira lilikuwa linamilikiwa na mbunge wa zamani wa CCM aliyefariki?...... HIYO ni propaganda TUUUUUUUUU
 
Huu ndio udini ambao benjamini mkapa ( rais mstaafu ) alizungumzia pale jangwani sasa chadema mnataka uthibitisho gani kuwa chadema ni chama cha katoliki, kkkt inabidi nasi kutafute chama.
Hii sio nchi ya katoliki.
Nawashauli waumini mliotengwa kanisa sio hilo tu kuna sabato anglikana na mengine mengi nendeni huko.
Hawa viongozi wa katoliki wako kichama zaidi sio kiroho.
Narani kitendo hiki
 
Huyo muislam amewashika makalio wakatoliki-yeye na vibaraka wake wote wenye njaa hawatakiwi kugusa eneo lolote la kanisa katoliki kwa kuwa walishaitusi imani! Wangekuwa wao damu ingemwagika.....! Wakatoliki naona imani yao inawapa upole na amani!
 

Mambo ya CDM yanaingiaje hapa, angetukanwa mtume ungeongeaje!...
 
.

Kwa mtu yeyote aliyekuwa akifuatilia kampeni za vyama vyote vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, kila mgombea bila kujali anatoka chama gani, pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa wananchi kumchagua mbunge, diwani na rais kutoka chama chake ili kuwezesha utawala bora...dhana ya mafiga matatu na wengine walikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano kuwa chungu huinjikwa kwenye mafiga matatu na si mawili wala moja...
 
kwa jinsi habari hii inavyopishana na ukweli uliopo, hatuitaji ushahidi ku-conclude kua muandishi wa habari hii pamoja na msimamizi wa gazeti vichwa vyao vimejaa makamasi badala ya ubongo.na kama wanaubongo basi lazima umechanganyika na mafuta ya taa.....kila mtu/watu hujenga heshima kwa namna wanavyosimamia msimamo/misimamo yao.kwa vile walianza wao kukashfu utatu mtakatifu then msilegeze kamba mpaka heshima ijengeke.
 
Huyu mwandishi achukuliwe hatua za kisheria,kwa kuchochea mfarakano wa kidini nchini.Hii ni hatari sana.Sidhani kama ana maadili ya uandishi wa habari.

hakuna uchochezi wowote hapo. it is a fact of what is happening in Sumbawanga. Mjinga peke yake ndiye anayeona kuwa ni uchochezi. Situation ya sumbawanga ni tete kwa sababu ya ujinga, uwezo mdogo wa kiuongozi wa watendaji wa ccm kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa pengine na taifa. Pinda ndiye mchafuzi wa hayo yote yanayotokea sumbawanga.

nasisitiza mjinga yeyote ndiye anayesema ni habari za kichochezi. na niswa na kukana kuwa 1+1=2. mwandishi ametoa taarifa kuonyesha mpasuko mkubwa wa kijamii ulioko sumbawanga unavyopaswa kushughulikiwa haraka. sidhani kama huo ni uchochezi

Mbunge wa sasa wa sumbawanga hapendwi hata na wana ccm wenzake kutokana na matendo yake machafu aliyoyafanya. Unataka kujifanya kuwa wewe ni m-ccm kuliko mzindakaya ambaye alikunjana mashati na pinda?
 

Mkuu, kukashifu imani ya mtu hadharani ni kosa! Tatizo ni kuwa huyo aliyefanya hilo kosa yuko nje ya mikono ya watendewa...ila supporters wake ambao mwanzo ilidhaniwa ni wanajumuia ndy haswaa watoke wakajiunge naye....wabadili dini tu! Nipo pamoja nawe mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…