Kanisa Katoliki lagoma kuzika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kim jong ii, Dec 14, 2010.

 1. k

  kim jong ii Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

  Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

  Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

  Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

  Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly.

  Baada ya waombolezaji kufika na majeneza ya miili hiyo mbele ya milango ya kanisa wakiwa tayari kuingia ndani, yalisomwa matangazo yaliyodai kuwa ibada ya kuombea marehemu haiwezi kufanyika hadi waumini waliotengwa (wanaCCM), watawanyike na wasionekane nje wala katika maeneo ya karibu na kanisa hilo.

  Miongoni mwa waumini hao waliohudhuria, lakini wametengwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hypolitus Matete, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fraten Kiwango, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini aliyefahamika kwa jina moja la Tumombe na Diwani wa CCM Viti Maalumu Kata ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

  Hali hiyo iliibua dhahama na kusababisha vurugu ya makundi mawili kati ya waliyotengwa na wanaounga mkono maamuzi hayo ambayo yalitiliwa nguvu na Paroko wa Parokia ya Kristu Mfalme, Pambo Mlongwa aliyefika maeneo hayo na kuwashinikiza mapadri waliokuwepo pale kuendelea na msimamo huo huo na kuwafanya waumini kuwataka waliokataliwa waondoke ili ibada ifanyike.

  Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini, John Mzurikwao aliwataka waumini hao kwa kuwa wametengwa, watii maamuzi hayo na kuwasihi kuondoka hapo ili utaratibu wa ibada ya mazishi uendelee.

  Viongozi hao baadhi walikubali na kurejea msibani, lakini baadhi ya waliotengwa walitoka nje ya uzio na kusubiri miili ya marehemu ili waungane na wenzao ili kwenda mazikoni. Ibada ya mazishi iliendelea.

  Francis Chale ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na gazeti hili, alikiri si kutengwa tu, bali alivuliwa ukatoliki wake, akituhumiwa kumshabikia Hilaly ambaye ni Muislamu, aliyetuhumiwa na kanisa hilo kwa kuukufuru utatu mtakatifu katika moja ya mikutano yake ya kampeni alipojifananisha na Yesu Kristo kwa kuelezea dhana nzima ya mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani.

  “Kitendo hiki kimetusikitisha sana, tulidhani kwamba tumezuiwa tu kuhudhuria ibada za misa takatifu kumbe hata ibada za mazishi. Sasa kama hali ndio hiyo na kanisa linajitambulisha kwamba ni wakala wa Chadema, basi na sisi tuliotengwa tunajipanga tupandishe bendera ya Chadema kwa kila Parokia iliyopo katika jimbo hili,” alidai Chale.

  Hivi karibuni, Parokia kadhaa za Jimbo Katoliki limewasimamisha waumini wake kwa madai ya kuisaliti imani yao kwa kutotii imani ya kanisa ambayo yaliwataka wasishabikie mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

  Katika msuguano huo wa kiimani, tayari kanisa hilo limewasimamisha na kuwatenga makatekista kwa madai wamelisaliti kanisa kwa kuwahamasisha waumini wao kumshabikia mgombea wa CCM.

  Hata hivyo, kutokana na mchakato huo, kanisa hilo linajiandaa kutangaza orodha ya mapadri waliolisaliti hadharani ili nao waadhibiwe kama walivyoadhibiwa waumini hao.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  nimesoma aya ya kwanza.

  kabla sijaendelea, naomba source
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 15,868
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapa.................... Kwa sababu kuna mtu humpendi basi kila baya litokealo ni lake..............
   
 4. k

  kim jong ii Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source ni habari leo
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  source gazeti la majira la leooooooooooooo
   
 6. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  sisomagi habari za magazeti ya udaku.

  basi sitaendelea kusoma.

  samahani sana mkuu
   
 8. SUNGUSIA

  SUNGUSIA JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili sasa naona linako elekea sio kuzuri kwani limevaa sura ya kisiasa zaidi kuliko ukweli wenyewe wa kucheza na IMANI YA WAKRISTO WA KIKATOLOKI. Kwanini muhusika aliye cheza na imani za wenzie asiombe msamaha kikaeleweka????
   
 9. L

  Leornado JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Habari leo imenifanya nichukie magazeti karibu yoote. What a trash....
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  waandishi na viongozi wasipokuwa makini wataliingiza taifa kwenye balaa , hapo wametengwa kwa kumsapoti mtu anayeukashifu ukristu bila kujali chama chake hata leo mgombea wa chadema akiukashifu ukristu atatengwa vilevile .
  magombea wa
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kabla hujafa hujaumbika na ukikikataa ya Mussa utayapata haya!
  Tulizoelea kuyasikia haya kule Pemba kati ya CCM na CUF lakini hili la Kanisa kuwatenga waumini kweli tumekwenda mbali.

  Mbona tuliyoyazoea kule sasa tuna yaona hapa?
   
 12. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 4,935
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ni sawa kabisa HAIWEZEKANI HUYO MBUNGE WA SISIEM KUJILINGANISHA NA YESU, KUMLINGANISHA JK NA MUNGU BABA na KUWALINGANISHA MADIWANI na ROHO MTAKATIFU. Walaaniwe na watengwe milele
   
 13. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 358
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sweden fujo ilitokea na waislam waliandamana na dunia yote ya kiislam pale mchora katuni,alipomchora Mtume Muhamad, Miss World ya mwaka 2002 Nigeria ilihamishiwa London,pale mwandishi mmoja alipotoa mfano kwamba mtume angekuwepo angeoa miss mmoja. Facebook Pakistan ilikuwa blocked pale walipochora katuni ya mtume. HUYU MBUNGE WA SUMBAWANGA AMEKASHIFU UTATU MTAKATIFU. AMBAYO NDIO NGUZO NA MSINGI MKUU WA IMANI TAKATIFU KWA KANISA KATOLIKI .DAH KWELI WAKATOLIKI Ni WAPOLE. WANGEKUWA NDUGU ZETU .MOTO UNGEWAKA.
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,394
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hii habari ilivyoandikwa chumvi imezidi. Kila dhehebu lina imani inayosimamia na muumini endapo atatenda kinyume na kile anachoamini lazima kanisa lichukue hatua. Imani Katoliki haimtengi muumini wake kwa sababu ya kumshabikia mgombea wa cheo cha siasa asiye mkatoliki, mwandishi aeleze sababu za hao waumini kuondolewa ukatoliki kwani lazima anafahamu ukweli ila anajaribu kuupotosha. Nachelea kujadili zaidi kwani mijadala ya Imani za watu hazina nafasi hapa JF
   
 15. D

  Derimto JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na akaindelea kujipa kazi ya kuwaza zaidi lazima umkute muhimbili kichwa kimepasuka kwa msongo wa mawazo.
  Ni utoto tu akikua ataacha.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ukisoma habari hii kwa makini unaweza kujiuliza mara moja tu kuwa nia ya mwandishi ni kuonyesha kwamba kanisa katoriki halikumtaka Hilary kwa sababu ni mwislamu kuwa mbunge wa sumbawanga lakini pia kanisa halikumtaka mgombea wa CCM lilimtaka wa Chadema.

  ukizama ndani zaidi, unabaini ukweli kwamba mtafaruku ulianza wakati wa kampeni ambapo taarifa ya mwandishi inadai Hilary ambaye ni mwislamu aliukufuru utatu mtakatifu wakati wa kampeni alipojifananisha na Yesu kristo kwa kueleza dhana ya mafiga matatu yaani kuchagua Rais, mbunge na diwani wa CCM.

  Mpaka hapo unabaini kwamba, tatizo hapo sio CCM wala Uislamu wa mbunge bali kauli zake wakati wa kampeni kuhusu utatu mtakatifu. Mimi nafikiri kwamba baada ya kauli hiyo ya kufuru kanisa katoriki parokia ya sumbawanga liliweka msimamo wa kutomuunga mkono mtu aliyekashifu utatu mtakatifu au ukristo kwa ujumla sio kwa uCCM wake au Uislamu wake bali kwa kauli zake. Msimamo huu wa kanisa ukageuka kuwa imani ya parokia hiyo na wale waliosaliti imani hiyo wakaadhibiwa kwa kumuunga mkono aliyekufuru utatu mtakatifu jambo ambalo katika dini zote linaweza kutokea kuwapa adhabu wanaokufuru dini.

  Nashauri kwamba, badala ya mwandishi kulikuza suala hili na kulipa sura au picha ya kanisa kupinga mwislamu kuwa mbunge au mgombea wa CCM angetusaidia kumuulliza mgombea, na waathirika wa kadhia hii kama ni kweli walikashifu/ walikufuruku utatu mtakatifu na pengine hawakutaka kukili kosa hilo mapema kwa kuomba radhi ili yaishe.

  kama huu ungekuwa ndio msimamo wa kanisa katoriki nchi nzima dhidi ya Uislamu au CCM migogoro kama hii ingesikika mahali pengine nchini na sio sumbawanga pekee kwani kuna wakatoriki wengi tu walikipigia kura chama cha CCM lakini bado ni wakatoriki na hakuna aliyewahoji kwa hilo... nini kimejiri huko sumbawanga? Tuambiwe ukweli.

  Je waliotengwa walikwenda kufanya nini kwenye ibada ya mazishi kama sio uchokozi uliwahi kuona lini kafri akaruhusiwa kuingia msikitini? hawa wametengwa na kuondolewa ukatoriki wao na mvutano ndio kwanza unaanza hakuna suluhu ni nini kiliwatuma huko? walipoambiwa waondoke kupisha ibada ya mazishi wangekuwa waungwana kutoka nje kwa amani ili padri afanya kazi yake.
   
 17. papason

  papason JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,169
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 280
  Safii sanaaa kanisa katoliki parokia ya familia takatifuu jimbo la sumbawanga, kwa taarifa yenu huu ni wakati muafaka kabisaa wa siasa za chukii na kulipizina visasi sisi tulisha jiandaa kwa hiloo
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwandishi ana ajenda ya siri ambayo inaweza kuhatarisha mahusiano ya jamii kama hatazama ndani zaidi kutafuta kiini cha mvutano huo. Uandishi wa namna hii hautaigawa CCM na parokia hiyo tu au Hilary mwislamu na parokia hiyo tu bali waislamu na wakristo kwa upande mmoja ama walio ndani na nje ya Jf au wanaccm na watu wa vyama vingine vya siasa.

  Mwandishi ameandika katika makala yake kwamba, kiini cha mgogoro ni mgombea wa CCM kuukufuru utatu mtakatifu wakati wa kampeni lakini anakwepa kuzama ndani ya kiini hicho cha tatizo analazimisha tunaosoma habari hiyo tuamini kwamba kiini ni tofauti za dini au vyama vya siasa.

  Dhamira ya mwandishi ni kuona wasomaji tunachangaia mada hii kwa misingi ya dini au misingi ya itikadi za vyama kwa jambo ambalo linaweza kuwa halipo au linakuzwa bila kuchukua tahadhali ya kuikoa jamii na mgawanyiko wa makala yake. kuwachonganisha waislamu na wakiristo wa sumbawanga hakuwezi kuishia sumbawanga tu kunaweza kusambaa nchi nzima na kisha kutuweka njia panda tunaoitakia mema nchi hii.
   
 19. J

  J Lee Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandiko ktk bblia yana sema kama mtu akifa azikwe ila haikuamriwa azikwe na kanisa so sio lazima kuzikwa na kanisa hata wanafamilia wa marehemu wanaweza zika pia kanisa lisiyumbishe watu
   
 20. d

  dotto JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Ni kosa lao na kufananisha ujinga wao na Utatu Mtakatifu. Diwani, Mbunge na RAis wote wanaotokana na michakato ya Rushwa kufananishwa na Utatu Mtakatifu ni kukufuru kwa makusudi. Adhabu hiyo ni ndogo.
   
Loading...