Kanisa Katoliki Congo kusema linamfahamu mshindi wa Uchaguzi Mkuu, limepata wapi nguvu hii?

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,414
36,572
Habari waungwana,

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, katika mchakato mzima wa uchaguzi wa Congo, Kanisa Katoliki limekuwa na ushawishi mkubwa sana hasa baadhi ya matamko juu ya Serikali na uchaguzi kwa ujumla

Tamko la hivi karibuni ni kuishinikiza tume ya taifa ya uchaguzi imtangaze mshindi sababu wao tayari wanamfahamu mshindi. Katibu mkuu wa baraza la Maaskofu anatoka mbele ya wanahabari na kusema data zao za waangalizi zaidi ya elf 40 nchi nzima zinaonyesha tayari kunamshindi.

Msimamo wa tume ya uchaguzi ni kwamba matokeo ya awali yatatangazwa Jumapili na Jan 15 matokeo yote kwa ujumla huku Rais atakayeshinda kuapishwa siku tatu baadaye.

Binafsi najiuliza kwanini Kanisa Katoliki Congo lina nguvu kiasi hicho? Je linanufaika na rasilimali za Congo? Linatumika na Mabepari? Limemsimamisha mgombea wake kisiri? Congo hakuna madhehebu mengine au Dini zingine kama Waislamu?

Nawasilisha kwa mjadala
Ndumbula Ndema
===========

HABARI KAMILI:
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco) limesema kuwa linafahamu jina la mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 nchini DRC na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika hali ya "ukweli na haki ".

IMG_20190105_111159.jpg

Baraza hilo limesema lina sampoli ya wawakilishi iliyochapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawauhusu kujuwa jina la rais aliechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya elfu 23 kati ya vituo elfu 70 vilivyowekwa na Ceni.

Donatien Nshole, msemaji wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC amesema sio jukumu lao kutangaza matokeo wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliechaguliwa na wananchi.

Ni muhimu kusisitiza kuwa kasoro zilizojitokeza haziwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa chaguo la wananchi wa DRC walioonyesha wazi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30," msemaji wa Cenco ameongeza."

Cenco imeitaka Tume ya Uchaguzi (CENI) kama taasisi inayounga mkono demokrasia kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa heshima ya ukweli na haki," amesema Padri Nshole.

Msemaji wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco) amekuwa anawasilisha ripoti ya awali ya ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi wa Tume ya Haki na Amani ya Cenco, ambayo inasema kuwa ilikuwa na waangalizi 40,000 wakati wa uchaguzi wa siku ya Jumapili.

Uchaguzi Mkuu wa Jumapili utapelekea kumpata mrithi wa Rais Joseph Kabila, ambaye hakuruhusiwa kuwania muhula wa tatu kulingana na Katiba.

Siku ya Jumanne CENI ilisema kuwa itatangaza matokeo ya awali siku ya Jumapili Januari 6, 2019. Siku ay Alhamisi CENI ilisema kuwa kuna uwezekano zoezi hilo liahirishwe.

Raia nchini DRC bado wanasubiri kutangazwa matokeoa ya uchaguzi huo.

hali ya wasiwasi bado inaendelea, huku huduma ya intaneti ikiendelea kufungwa na mitambo ya radio ya kimataifa RFI ikizimwa.

Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi CENI imesema kuwa tayari imehesabu asilimia 20 tu ya kura zilizopigwa.
 
Hata mimi nimeshangaa kusikia hilo kupitia DW inakuaje wanaingilia mchakato ambao hauwahusu kama kanisa hawaoni wanaweza kuleta ghasia ikiwa tume ya uchaguzi itamtangaza yule aliyetofauti na jina walilonalo kama wakimtaja na wao mtu wao?

Lakini pia kuna dini na madhehebu tofauti tofauti huko Congo endapo mgombea wanaedai ameshinda akishinda kweli haitaonekana yupo kwa maslahi ya wakatoliki na hata yeye kuwa loyal kwao kwa kuamini ndiyo waliyomuweka na hivyo kuleta mpasuko wa kiimani na kidini ambao ndiyo hatari zaidi

Nadhani katika hili kanisa katoliki limekosea kuja na hoja hiyo hadharani
 
Unaulizia nguvu...?? Nguvu wanayo tena kubwa...

Wasomi wengi ni Wao..

Wana Vyuo vinavyozalisha Idadi kubwa ya Wakatoliki wasomi ambao ndio wanejazana huko Serikalilini...

Idadi yao ni kubwa huko Congo....

Hivyo Serikali ni wao....Tume ya Uchaguzi utawakuta huko....Mashuleni ni wao....Mahospitalini ni wao....Kila kona....
NB
Wekeza kwenye Elimu na Afya utaitawala dunia ...hakuna uchawi
 
Nguvu ya RC NI kubwa kuliko serikali yoyote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
We Chukulia Mfano mdogo..

Shule zote bora zinazotoa wanafunzi bora ni Za Catholic....maana yake Universties Feeder kubwa ni Wakatoliki......hivyo Wasomi wengi ni Wakatoliki.......Hivyo Huko Serikalini na Sekta Binafsi wanejaa Wakatoliki......Hivyo lazima wawe na nguvu....kila kona wapo.

Tazama Vyuo vyao Vikuu...Hapa Tz hata Serikali bado haijaweza Kuwa na Idadi ya Vyuo ilivyonavyo Kanisa Katoliki....Maana yake Wasomi wengi ni Wakatoliki....Utashindana nao wapi...??

Huko Dodoma Jesuits wataporomosha State of Art University.....

Hapo ndipo palipo na nguvu ya Kanisa...

NB
Wekeza kwenye Elimu Uitawale Dunia...

Leo Dunia inatumia Kalenda Ya Wakatoliki
Leo Hii Dunia inatumia Biblia iliyoyengenezwa na Wakatoilki..
Kila Kona na Pembe ya nchi ni wao.....

" Endeneni ulimwenguni kote (Katolicos) mkawafanye wote kuwa wanafunzi wangu."
 
Sio kwamba hawajui, wanajua ila hawataki kuukubali huu ukweli. Haujalishi Catholicism faith inafata misingi ya Mungu au la, but hata mifumo yote ya usalama na uendeshaji was serikali duniani una baraka za Vatican. Ukimess up na vatcan jiandae kuitwa gaidi, dictator and titles alike mpka utie hadab

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Chukulia Mfano mdogo..

Shule zote bora zinazotoa wanafunzi bora ni Za Catholic....maana yake Universties Feeder kubwa ni Wakatoliki......hivyo Wasomi wengi ni Wakatoliki.......Hivyo Huko Serikalini na Sekta Binafsi wanejaa Wakatoliki......Hivyo lazima wawe na nguvu....kila kona wapo.

Tazama Vyuo vyao Vikuu...Hapa Tz hata Serikali bado haijaweza Kuwa na Idadi ya Vyuo ilivyonavyo Kanisa Katoliki....Maana yake Wasomi wengi ni Wakatoliki....Utashindana nao wapi...??

Huko Dodoma Jesuits wataporomosha State of Art University.....

Hapo ndipo palipo na nguvu ya Kanisa...

NB
Wekeza kwenye Elimu Uitawale Dunia...

Leo Dunia inatumia Kalenda Ya Wakatoliki
Leo Hii Dunia inatumia Biblia iliyoyengenezwa na Wakatoilki..
Kila Kona na Pembe ya nchi ni wao.....

" Endeneni ulimwenguni kote (Katolicos) mkawafanye wote kuwa wanafunzi wangu."
We tulia, unadhani shule za Wakatoliki wanasoma Wakatoliki tuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio linanguvu Bali linahurumiwa tu
Habari waungwana,

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu,katika mchakato mzima wa uchaguzi wa Congo, Kanisa Katoriki limekuwa na ushawishi mkubwa sana hasa baadhi ya matamko juu ya Serikali na uchaguzi kwa ujumla,tamko la hivi karibuni ni kuishinikiza tume ya taifa ya ucuchaguzi imtangaze mshindi cos wao tayari wanamfahamu mshindi,katibu mkuu wa baraza la makanisa anatoka mbele ya wanahabari na kusema data zao za waangalizi zaidi ya elf 40 nchi nzima zinaonyesha tayari kunamshindi.

Msimamo wa tume ya uchaguzi ni kwamba matokeo ya awali yatatangazwa Jumapili na Jan 15 matokeo yote kwa ujumla huku Rais atakayeshinda kuapishwa siku tatu baadaye.

Binafsi najiuliza kwanini Kanisa Katoriki Congo lina nguvu kiasi hicho? Je linanufaika na rasilimali za Congo? Linatumika na Mabepari? Limemsimamisha mgombea wake kisiri? Congo hakuna madhehebu mengine au Dini zingine kama Waislamu?

Nawasilisha kwa mjadala
Ndumbula Ndema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Chukulia Mfano mdogo..

Shule zote bora zinazotoa wanafunzi bora ni Za Catholic....maana yake Universties Feeder kubwa ni Wakatoliki......hivyo Wasomi wengi ni Wakatoliki.......Hivyo Huko Serikalini na Sekta Binafsi wanejaa Wakatoliki......Hivyo lazima wawe na nguvu....kila kona wapo.

Tazama Vyuo vyao Vikuu...Hapa Tz hata Serikali bado haijaweza Kuwa na Idadi ya Vyuo ilivyonavyo Kanisa Katoliki....Maana yake Wasomi wengi ni Wakatoliki....Utashindana nao wapi...??

Huko Dodoma Jesuits wataporomosha State of Art University.....

Hapo ndipo palipo na nguvu ya Kanisa...

NB
Wekeza kwenye Elimu Uitawale Dunia...

Leo Dunia inatumia Kalenda Ya Wakatoliki
Leo Hii Dunia inatumia Biblia iliyoyengenezwa na Wakatoilki..
Kila Kona na Pembe ya nchi ni wao.....

" Endeneni ulimwenguni kote (Katolicos) mkawafanye wote kuwa wanafunzi wangu."
Yeah though kwenye institutions za Catholics hawabagui nani asome pale labda tu kwenye zile za seminary. Ila kiukweli wana nguvu kubwa sana kwenye nchi nyingi duniani.
 
Back
Top Bottom