Kanisa Anglikana laiasa Kamati Kuu ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa Anglikana laiasa Kamati Kuu ya CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Kanisa Anglikana laiasa Kamati Kuu ya CCM

  Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma; Tarehe: 18th April 2011 @ 22:40 Imesomwa na watu: 80; Jumla ya maoni: 0
  KANISA la Anglikana mkoani Kigoma limewataka wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioteuliwa katika mabadiliko ya hivi karibuni kutumia nafasi zao kumshauri vizuri Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ili maisha bora kwa Watanzania yapatikane.

  Mchungaji Kiongozi wa Ushariki wa Mwanga, Daniel Bugemwa alisema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza katika kituo cha wazee cha Silabu, na cha watoto waishio mazingira magumu cha Mwocachi.


  Alisema kuwa sehemu ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ndiyo viongozi waandamizi wa serikali na wanayo nafasi ya kuleta mabadiliko mbalimbali katika nchi kwa kupitia kikao hicho.


  Mchungaji huyo alisema kuwa jambo la kwanza ambalo wajumbe hao wanapaswa kuzingatia ni kwa serikali kuweka mazingira mazuri katika kuboresha uchumi na kuleta unafuu wa maisha kwa Watanzania.


  Alisema kuwa ubinafsi wa baadhi ya viongozi na uchu wa kujilimbikizia mali ndiyo ulioifanya nchi kufikia ilipo.


  Alisema Watanzania wamechoshwa na mtindo wa baadhi ya viongozi kutumia rasilimali ya nchi kwa manufaa yao.


  “Kelele zinazopigwa kila siku na Watanzania kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na

  serikali kuhusu ufisadi ni ishara kwamba watu hao wamechoka na vitendo vinavyofanywa na watu hao, ni wakati sasa wa kamati kuu ya CCM kuhakikisha kwamba gamba lililovuliwa halitarudia tena,” alisisitiza Mchungaji Bugemwa.

  Akizungumzia upendo, alisema kuwa Watanzania wote bila kujali dini, kabila wala umaeneo, wanayo nafasi ya kuwasaidia wenzao wenye shida mahala popote na hasa wakati huu ambao waumini wa Kikristo wanaelekea kusherehekea Pasaka.


  Mchungaji huyo kwa niaba ya waumini wa kanisa lake alikabidhi vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 1.8 zikiwemo nguo, sabuni na vyakula mbalimbali ikiwa maalumu kwa ajili ya kuwafanya watu hao washerehekee vizuri Pasaka.


  Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Kilahumba International Christian, Kilahumba Kivumo ambaye taasisi yake imekuwa ikiwasaidia wazee hao wa kituo cha Silabu, alisema kuwa pamoja na taasisi yake kutoa msaada mara kwa mara kwa watu hao, bado mahitaji ya wazee hao ni makubwa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  PHP:
  "Kelele zinazopigwa kila siku na Watanzania kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na   
  serikali kuhusu ufisadi ni ishara kwamba watu hao wamechoka na  vitendo  vinavyofanywa na watu hao, ni wakati sasa wa kamati kuu ya CCM   kuhakikisha kwamba gamba lililovuliwa halitarudia tena," 
  alisisitiza   Mchungaji Bugemwa.   
  you can say that again and again....................................
   
Loading...