Kaniomba nizae naye!!

Kaniomba nizae naye!!

lewiathan

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
211
Reaction score
290
Baada ya kutembelea mji mmoja nilibahatika kukutana na Binti mwenye maisha/Biashara zake.

Baada ya muda tulianza mahusiano lakini nilimuambia ukweli kuwa nina mke na ni Baba wa mtoto mmoja.

Tuli-date mara mbii tu kwa miezi miwili tofauti nilienda mwaka jana mwezi 9 ndio mwezi ambao mahusiano yalianza na nikaenda mwezi wa 10 baada ya hapo sijaenda tena maana nilichokifuata nilikamilisha.

Cha ajabu mwezi huu yaani Jana saa 2:45pm kanpigia simu ananiomba tuzae mimi nikamwambia ukweli siwezi kutunza nyumba mbili I mean kulisha huku na huku, akasema kuhusu hilo nisijali atahudumia kila kitu labda akiugua tu ndo naweza lazimika kuchangia napo kwa 25% tu. Nimemuomba asubiro nilifkirie.

WanaJF naomba mawazo yenu nikubali?

Je, wife akojua Japo yupo mbali ila hii dunia hamna siri ya watu wawili.


Nb: Ndoa yangu ni moja kat ya Ndoa zenye furaha Dunian
 
Mzalishe tu japo iwe kwa mandishi hayo ayasemayo itasaidia sana mbeleni.
 
Mungu katuleta duniani TUZALIANE ww ni nan kupingana na mungu?
 
Mkuu usiseme ingkuwa na naamn ni moja kat familia zenye furaha.
Iltokea tu nikvutiwa naye kwa 7bu nilkuwa mbal na mke wangu
ingekua na furaha usingeanza mahusiano.tubu acha dhambi za kizembe/hasara
 
Siwz kua na wame wawil hcho ktu haiwz tokea
Usikubali, kauli za kusema nitalea mwenyewe zimewaponza wengi na ikitokea ukafariki ataisumbua sana familia yako. Kama upo tayari kuzaa nae na ukibari kumuoa kabisaaaaa ifahamike ni mke wa pili. Nimemaliza
 
Nimesoma hadi mwisho wewe tunaweza kushauri uanchane nae kumbe kimoyomoyo nyuma ya pazia unamendea roho inakuuma
Soma tena huo uzi nina Familia boss kaomba ktu kikubwa sana nahtaj ushaur
 
Itakuwa ana mimba tayari...si uliuza mechi hizo mara mbili ulivyolala nae?
 
Hahahaaa Kuchepuka hakuwz kukwamisha furaha ya Ndoa
[/QUOTE
Basi ni furaha feki, au wewe ndio mwenye furaha, au mkeo. je naye anachepuka? ama ni wewe tu
? je anajua kuwa unachepuka ? na bado ana furaha?
 
ujanani nilikutana na jambo kama hili Kyela wakati tukifanya magendo ya power namba moja na sukari pori kwa pori na akina X ambaye kwasasa ni mbunge wa jimbo flani ndani ya mbeya na ni maarufu kwa biashara ya vipodozi,sasa pale nilikutana na dada ambaye kiukweli naweza sema ni moja kati ya wanawake waliowahi kunipenda sana aisee ndipo akaniomba nizae nae mtoto ili hata siku nikiondoka awe ana mtu wa kumfanya anikumbuke na alikuwa anajiweza kifedha na alisema kuhusu malezi atalea mwenyewe mwanzo nilikataa ila baadae niliingia mkenge nikakubali,mamvo yalienda sawa akabahatika kujifungua mtoto wa kiume na hapa ndipo kero zikaanza aisee yan nilikuwa mhuni asiye na mke lakini kichwa kilikuwa kinawaka moto sasa wewe mwenye ndoa itakuaje kama mambo yakija kupinduka,ilifikia kipindi kero zikazidi hadi nikabadili hata route ya biashara nkaanza kuingia malawi kupitia mto flani upo pale pemba karibia na tunduma,nilikuwa nimepanga pale Migombani ila alipeleleza mpaka akapajua na kwa kero zake ilibidi nihame pale wakat palikuwa ni muhimu sana strategically kwa shughuli zangu maana ni karibu na Mpaka wa Nakonde na pia palikuwa karibu sana na tazara/reli pia kuhama migombani kuninighalimu sana sana maana kipindi magendo yalipokuwa magumu(kuna kipindi dolia ya askar wa kuzuia magendo ilikuwa kali sana) nilikuwa nafanya biashara ya viatu ambavyo nilikuwa nachukua pale mwanjerwa au sido kisha napeleka Zambia Ndola na nilikuwa sometimes napata faida ambayo kuna muda nilitaka hata niachane na magendo,hii biashara ilibidi niiue kwa kero za yule bibie nikaludi iringa

Na mbaya zaidi niliwah kumwambia kijiji nachotokea(ndani ya iringa)aisee kuna siku sina hili wala lile nilimkuta nyumbani kwa mzee wangu kaleta mtoto....ni hadithi ndefu sana ila nilisusiwa mtoto ambaye kwa sasa ni mtu mzima sasa

Kataa hiyo kitu kwa faida yako,familia yako na hiyo ndoa yako yenye fulaha ndgu yangu
 
Back
Top Bottom