MONTESQUIEU
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 847
- 80
Rafiki yangu kaniomba nimsindikize benki achukue pesa akanunue kiwanja kaenda kaunta kachukua pesa kanituma nikamnunulie maji akidai ananisubiri hapo ndani ya benki kwani kuna receipt anaingojea.
Narudi simkuti nampigia cm hapokei, baada kama ya robo saa ananipigia cm eti alishaondoka nimfuate huko anakonunua kiwanja.
Hapa nikaanza jiuliza huyu kaomba lift yangu huko tena kaenda nanani?
Na kwanini anitoroke?
Jamani wana JF huyu anamaana gani?
Kwani ni mmeo huyo?
mmh mashtaka mengne jaman
asi kakupunguzia muda na mafuta umeokoa..
rud hm /kwako endelea na mambo ako..au unha hisa kwenye icho kiwanja?
Rafiki yangu tu
Wa kike wa kiume?
Wa kike mpendwa!
Ah,mpotezee tu huyo labda aliona utakwapua mzigo nn! Sasa kwann akukimbia na acpokee hata cm!
Ninachojiuliza ni kwann akukimbie kulikuwa na haja gani ya kukuomba umcndikize kama alikua hakutaki
Nimefanya utaratibu huo nisharudi kwa ofisi. kwanza kanitoa job nikaomba ruhusa ya uongo!
mwaya binafsi nimeshangaa!
Mwaya binafsi nimeshangaa!
basi alitaka kukurusha roho uone anavyo droo mipene
kama ni kumrusha roho si angempelekea hati ya kiwanja tu kuliko kumtoa mwenzie kazini jamani
Aliogopa usije ukamkaba ndo maana akaamua kukutoloka
dar huyo kiboko, sasa alikushirikisha ya nini? urafiki mwingine bwana?
pole sana ndugu
Ukweli ni kwamba kuna jambo ambalo lilimpita kichwani na akagundua kuwa hakuamini hata kidogo kuongozana nawe kwenda kununua hicho kiwanja na hakuwa na njia nyingine ya kukwambia zaidi ya kufanya alichofanya.
Ipo siku anaweza kukwambia kama ni muwazi kwako ila isikuumize sana kichwa