Kaniblock kwa kumkumbusha deni ninalomdai

Darren2019

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
1,111
Reaction score
2,412
Habari zenu waungwana, ni matumaini yangu kwamba mwaendelea vema.

Binafsi sikuwahi kuamini kama urafiki unaweza kuuliwa na vitu vidogo kama kukopeshana, japo nilikuwa nasikia tu tangu nakuwa kauli kama, "usimkopeshe rafiki wa karibu au ndugu" badala yake uwasaidie tu au ukikopesha basi usiwe na bajeti kwa hiyo pesa.

Unajua kujizuia kumsaidia mtu nako si rahisi sana, kwahitaji roho ngumu kidogo. Siku moja nikapokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana, tumesoma pamoja miaka 6 ya sekondari, ana shida mpenzi wake ana matatizo ya kiafya na hana namna nyingne zaidi yangu, niokoe maisha ya mpenzi wake.

Ukweli sikuwa na pesa kiasi alichotaka ila kulikuwa na pesa za Mzee wangu nahifadhi baada ya kuuza kiwanja chake. Nikamueleza ukweli hali halisi ilivyo akanihakikishia nisiwe na wasiwasi within a month ingerudi.

Kumbuka pesa ninayopanga kumtumia ni ya Mzee wa watu aliyouza kaardhi kake ili ajenge kanyumba kijijini pale.

Baada ya kurudi home nkampa mke wangu full mkanda ulivyo na nia yangu. Mke akasita na hakutaka nifanye hivyo ila mimi nikalazimisha tena kwa mbwembwe, yule rafiki yangu wewe, tumetoka mbali! Unataka kututenganisha?

Basi nikazama NMB nikatuma pesa bhana.
Miezi ikaenda kimya. Mzee anataka pesa yake aanze ujenzi, ikabidi nireplace lile deni. Mwaka kimya, mawasiliano yakaanza kupungua, mwaka wa pili, wa tatu, huwa simdai ila kwanini urafiki ufe?

Namtafuta tu mimi mara moja moja. Mwaka wa 4 huu, juzi nikatext Messenger maana na namba zake nilipoteza ila huwa namuona mitandaoni. Badala ya kureply leo ndo nagundua kumbe ameniblock!

SIHITAJI MARAFIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachopitia wewe ndio ninachopitia sahivi. Ila nimewatumia meseji leo wadeni wote nimewaambia ikifika 2020 pesa wakae nayo tu. Wengine majirani na wengi coworkers na marafiki.

Aisee kufanya biashara ya kukopeshana na marafiki ni upuuzi.
 
Mmenikumbusha mbali. Mimi pia rafiki yangu mkubwa tena mfanyakazi mwenzangu. Tulikuwa marafiki sana na siri zake zangu na yeye pia. Sasa alijua nina vipesa kiasi nilitoka kuchukua mkopo. Akakuta mtu anauza pikipiki 1.5m .Akaitamani na muuzaji alitaka apewe 1m kwanza nyingine mnunuzi anamalizia baadaye.
Jamaa akaja kwangu anataka nipe 1m akachukue mashine. Nilisita sana kiukweli nikajua urafiki ndio unayoyoma hivyo kwani naelewa sana japo alidai atachukua mkopo karibuni anirudishie. Halafu sikuona sababu ya msingi ya kununua piki piki. Yeye alidai ya kwendea kazini wakati kazini kwake akishuka kwenye daladala anabakiza kama mwendo wa dk 30 kufika kwa kutembea. Nilipiga chenga siku 2 hivi kisha nitasalimu amri nikampa.
Akachukua ile pikipiki Alichukua mkopo akanipa 500k inabaki 500k. Kisha akajiingiza kwenye majukumu mengine. Alihamisha mtu toka baa akampangishia akawa mke wa pili. Alianza kunisumbua kila wakati mara nipe 50k mara 70k nk. Mshahara ukitoka ananipa lakini haiishi wiki tena anataka 100k na kuendelea . Yaani full usumbufu. Kisha akakata mawasiliano wakati namadai 700k Nikimtumia msg hajibu nilipiga hapokei. Nikapiga kimya mwaka. Kisha nikaona huu ujinga nikampa mkanda boss alishangaa sana maana jamaa anaaminika sana. Nikamwomba atumie nafasi yake kumshawishi anilipe maana mikopo alikuwa anachukua lakini kulipa deni hapana. Boss alimwita akakiri na kuahidi kulipa kiasi baada ya miezi 3 nikawa mpole. Muda ukafika akalipa 400k.
Nilipofuatilia kwa boss zingine lini akawasiliana na jamaa yangu. Jibu lake sasa.Du!
Anadai hela gani zingine mimi deni nimelipa hatudaiani tena.
Hilo jibu halikuninyima usingizi kwa sababu hata kabla sijaenda kwa boss nilishajindaa kwa lolote maana hela tulipeana bila ushahidi wowote. Tokea hapo sina rafiki hadi sasa ni mahusiano ya kiasi tu bila mafungamano ya karibu.
 
Habari zenu waungwana, ni matumaini yangu kwamba mwaendelea vema.

Binafsi sikuwahi kuamini kama urafiki unaweza kuuliwa na vitu vidogo kama kukopeshana, japo nilikuwa nasikia tu tangu nakuwa kauli kama, "usimkopeshe rafiki wa karibu au ndugu" badala yake uwasaidie tu au ukikopesha basi usiwe na bajeti kwa hiyo pesa.

Unajua kujizuia kumsaidia mtu nako si rahisi sana, kwahitaji roho ngumu kidogo. Siku moja nikapokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana, tumesoma pamoja miaka 6 ya sekondari, ana shida mpenzi wake ana matatizo ya kiafya na hana namna nyingne zaidi yangu, niokoe maisha ya mpenzi wake.

Ukweli sikuwa na pesa kiasi alichotaka ila kulikuwa na pesa za Mzee wangu nahifadhi baada ya kuuza kiwanja chake. Nikamueleza ukweli hali halisi ilivyo akanihakikishia nisiwe na wasiwasi within a month ingerudi.

Kumbuka pesa ninayopanga kumtumia ni ya Mzee wa watu aliyouza kaardhi kake ili ajenge kanyumba kijijini pale.

Baada ya kurudi home nkampa mke wangu full mkanda ulivyo na nia yangu. Mke akasita na hakutaka nifanye hivyo ila mimi nikalazimisha tena kwa mbwembwe, yule rafiki yangu wewe, tumetoka mbali! Unataka kututenganisha?

Basi nikazama NMB nikatuma pesa bhana.
Miezi ikaenda kimya. Mzee anataka pesa yake aanze ujenzi, ikabidi nireplace lile deni. Mwaka kimya, mawasiliano yakaanza kupungua, mwaka wa pili, wa tatu, huwa simdai ila kwanini urafiki ufe?

Namtafuta tu mimi mara moja moja. Mwaka wa 4 huu, juzi nikatext Messenger maana na namba zake nilipoteza ila huwa namuona mitandaoni. Badala ya kureply leo ndo nagundua kumbe ameniblock!

SIHITAJI MARAFIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa ya ww na mzee wako inakuaje kuomba ushaur kwa mkeo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe wahenga tupo wengi humu aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi mwenyewe kuna mtu namdai tangu mwezi wa 5 mwishoni mwaka huu mpaka December hii hajanipa na kila nikimkumbusha analeta kiswahili kisichoeleweka mana ngoja nisubiri niuze TV na vingine nitakurejeshea, mara subiri nikipata mpeano wangu, mara oooh ila me nakua mpoole.

Na huyo jamaa ni rafiki yangu na nilisoma nae shule ya msingi japo kwa sasa hata sms zangu kujibu hataki. Kuna siku alinitext kuwa namba yake ya zaman anaacha kutumia kwa sasa anatumia ingine, hapo hapo likanijia wazo kuwa huyu jamaa hataki kutumia namba yake kisa madeni.

Ila messenger huwa namuona sana na namtext ila wapi viswahili vyake havina maana. Nimeamua kumpotezea tu ila nikipata time namkumbusha mara moja moja sio mbaya na hapa huwa najiuliza nimekosea nini mpaka anizungushe kiasi hiki.

Kwa sasa nadhan nimejifunza kitu, sitokubali kukopesha tena kwa marafiki zangu aisee bora nionekana mchoyo tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbula nilimkopesha rafiki yangu wa karibu wakati tupo mwaka wa mwisho chuo. Ni mshikaji ambaye kwao siyo mambo mabaya na anahudhuria sana kwenye nyumba ya ibada. Aliniambia kuwa angenilipa ndani ya mwezi mmoja.

Lol, kilichotokea sasa uliisha mwaka na miezi kadhaa hajanilipa hela yangu. Siyo kama hana hela, Ila alikuwa anajali tu mambo yake.

Kuna siku nikamtext whatsapp kumdai akasema hana labda nisubiri mshahara ukitoka atanipa. Ikakata kama miezi mitatu hivi yupo kimya.

Nikaona huu ni utoto, Nikafuta namba zake nikampiga block. From there naonaga kukopesha washkaji ni usenge tu. Mtu kama ana shida bure utoe msaada au umnyime ila siyo kumkopesha.

Akipita hapa akaiona hii screenshot atajijua mwenyewe...
20191229_181803.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu waungwana, ni matumaini yangu kwamba mwaendelea vema.

Binafsi sikuwahi kuamini kama urafiki unaweza kuuliwa na vitu vidogo kama kukopeshana, japo nilikuwa nasikia tu tangu nakuwa kauli kama, "usimkopeshe rafiki wa karibu au ndugu" badala yake uwasaidie tu au ukikopesha basi usiwe na bajeti kwa hiyo pesa.

Unajua kujizuia kumsaidia mtu nako si rahisi sana, kwahitaji roho ngumu kidogo. Siku moja nikapokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana, tumesoma pamoja miaka 6 ya sekondari, ana shida mpenzi wake ana matatizo ya kiafya na hana namna nyingne zaidi yangu, niokoe maisha ya mpenzi wake.

Ukweli sikuwa na pesa kiasi alichotaka ila kulikuwa na pesa za Mzee wangu nahifadhi baada ya kuuza kiwanja chake. Nikamueleza ukweli hali halisi ilivyo akanihakikishia nisiwe na wasiwasi within a month ingerudi.

Kumbuka pesa ninayopanga kumtumia ni ya Mzee wa watu aliyouza kaardhi kake ili ajenge kanyumba kijijini pale.

Baada ya kurudi home nkampa mke wangu full mkanda ulivyo na nia yangu. Mke akasita na hakutaka nifanye hivyo ila mimi nikalazimisha tena kwa mbwembwe, yule rafiki yangu wewe, tumetoka mbali! Unataka kututenganisha?

Basi nikazama NMB nikatuma pesa bhana.
Miezi ikaenda kimya. Mzee anataka pesa yake aanze ujenzi, ikabidi nireplace lile deni. Mwaka kimya, mawasiliano yakaanza kupungua, mwaka wa pili, wa tatu, huwa simdai ila kwanini urafiki ufe?

Namtafuta tu mimi mara moja moja. Mwaka wa 4 huu, juzi nikatext Messenger maana na namba zake nilipoteza ila huwa namuona mitandaoni. Badala ya kureply leo ndo nagundua kumbe ameniblock!

SIHITAJI MARAFIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
SASA UMEKUA MKUBWA KIJANA WANGU SAFI
 
Mkuu umesahau kuwa
"Tanzania Ni miongoni mwa Nchi za kiafrika ambazo ukimukopesha pesa rafiki ako una mupoteza yeye na pesa yako vyote kwa wakati mmoja".

Ilinitokea kwa rafiki angu tuliesoma nae mpaka Leo Sina rafiki wa kivile zaidi ya ushikaji tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M kuna mshikaji wangu wa karibu alienda kwenye mishe zake kijijini kaishiwa pesa akanicheki mm nikawa sijabeba hela mfukoni nikamwambia subiri nikirud mjini jion nitakutumia basi kila mda msg anaulizia km nimerud bahat mbaya nilichelewa kurudi nishashindwa kumtumia usiku huo kesho nikaingia job anapiga simu mda mwingi na msg kibao nikatoka job saa nane nikapitiliza m pesa nikamtumia
Duuh hata asante hamna nikamwandikia msg hajajibu na delivery report imekuja nikamtumia msg kwa namba nyingine akajibu nikaumia sana nikasema hyo hela sitakaa niidai na assume nimeipoteza maisha yakaendelea baada ya wiki akaja kuniandikia msg "inakuwaje man" nikakausha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom