Kaniacha kisa kumwambia abadili dini

Kaniacha kisa kumwambia abadili dini

Hizi dini zinataka kututenganisha na vipenzi vyetu hata mimi ni muhusika wa hili janga ila nimeona wacha iwe itakavo kuwa
 
Mpenzi ni wako siyo wa mama yako au ndugu zako suala la mapenzi ni ya wawili ukiwa mwanaume katika suala la mapenzi upaswi kumsikiliza mtu yoyote au mbwa yoyote umezaliwa peke yako utakufa peke yako utazikwa peke yako..
 
Habari naombeni ushauri!!nimekuwa kwenye mahusiano na binti almost miaka minne japo ni dini tofauti yeye muislamu,mimi mkristo!!Tumefanya vitu vingi sana pamoja na kushirikiana katika mengi tu tangu tukiwa chuo mpaka baada ya kumaliza!in short anajua kila kitu kuhusu mimi nami pia hakuna nisichojua kuhusu yeye!!

Ukweli tumependana sana,mwanzoni tuliona suala la dini halitakuwa tatizo sana binti alijitahid sana kujifunza mambo yanayohusu dini yangu mpaka kuingia kanisani mda mwengine lakini alikuja kubadilika ghafla baada ya kwao kujua na kumgombeza sana kwanin anafanya mambo yaliyo kinyume na dini yake hivyo sikuendelea tena kumuhimiza kujifunza dini yangu.Aliacha kwenda kanisan na kuacha kabisa kufwatilia dini yangu!
Tuliendelea kuwa kwenye mahusiano pasipo kuingiza tena suala la dini!

Lakini lilikuwa ni suala linalomuumiza kila mtu hasa future yetu na watoto wetu ni ipi!na je vp wazazi watakubaliana nasi! Kusema ukweli wazazi na ndugu zangu wasingekubali kabisa hili suala!!nilimficha binti mwanzon na kumtia moyo tu kuwa wazazi wataelewa na kunikubalia kumuoa hivyo hivyo nilifanya hivi ili nisimpoteze na kumkatisha tamaa.

Siku zikazidi kwenda binti akawa hana amani kwani alikuwa anaitaka sana ndoa akaamua kwenda kuwaambia wazazi wake kuhusu mimi na walikubali!ila ukija upande wangu ni suala gumu sana wazazi na ndugu kuelewa!

Ikabidi tu nimueleze wazi kuwa upande wangu hawakubali wanataka abadili dini kwanza japo nilijua ni jambo gumu kwake na hukukubaliana nalo.Mwisho nikamuambia basi itabidi tufunge ndoa ya bomani akakubaliana nayo!wakati namueleza yote hayo wazazi wangu sijawaambia lolote na wala hawajui kuhusu mahusiano yangu na binti.

Siku zikawazinazidi kwenda huku nasita kufanya lolote sababu najua wazazi na ndugu zangu watanipinga.Binti akawa hana amani kwani marafiki zake wanaolewa yeye na mimi tumekwama.Ilifika kipindi binti akawa ananinunia kabisaa wala hajisikii kuongea na mie wala hataki kukutana kimwili sababu ya mawazo ya ndoa.

Nilimuelewa hali alonayo na kumuonea sana huruma kwani watu kibao wa dini yake wanaenda kwao kutaka kumuoa lakini anawakataa sababu yangu hilo lilikuwa linaniumiza kwani mda unazidi kwenda na hamna nachofanya!!

Sikuwa na jinsi ikabid niongee na mama yangu nimueleze kila kitu kuhusu mimi na binti mama alikataa kabisa na kuniambia hilo haliwezekani na hata binti akibadili dini bado litakuwa suala gumu kwani mwisho wa siku atarudi tu dini yake ya mwanzo!!

Nikambembeleza sana mama na kumueleza tulipotoka mbali na binti na jinsi tunavyopendana lakini mama aliishia kuniambia tu tafuta wa dini yako!
Ikabidi tu nimueleze binti ukweli kuwa home wamekataa kabisaa hata ndoa ya bomani hivyo nikamshauri abadili dini ili hili suala liwe jepesi kwetu na hasa future ya watoto wetu waje wapate malezi mazuri!!Binti alikataa kabisa na kuanza kunilaumu nimempotezea mda wake bure na kwanin sikumueleza mapema!alinishukuru na kuniambia maisha mema asanteni sana!!

Yaani kiukweli binti ananichukia sana mimi mpaka ndugu zangu!!Moyo unaniuma kwani nampenda sana na wala sio nia yangu kumpotezea mda au kutokumuoa ila changamoto kubwa ni dini!kila mmoja wetu hataki kubadili kumfwata mwenzake!!

Nimekwama sielewi nifanye nini?wazazi na ndugu zangu wananipinga na hawakubaliani na hili!huku binti nae kanikasirikia hataki hata kunisikia na namba zangu kafuta na kuniblock!hahitaji kuongea lolote na mie kashafanya maamuzi ya kuniacha anasema haikuwa fungu lake mimi kumuoa!!

Naumia sana hasa mda wote tulokuwa pamoja na upendo wangu kwake!Anaona mie nimempotezea mda na simpendi kwani nimekuwa upande wa wazazi na ndugu zangu pia ni selfish nataka abadili yeye tu dini na sio mimi!!

pole kwa miaka minne iliyopita, una mawazo gani kuhusu miaka 10,20,30, 40 au zaidi ijayo?
 
Hamna kitu kinachoniboa kama dini hasa pale inaposababisha maafa kama haya...
 
Kumshinikiza mtu abadili dini ni kosa kubwa. Hivi mtu anabadilishaje imani aliokua nayo. It's very hard. Anaweza kukubali ili muwe pamoja lakini deep down kitakua kinamtafuna ndani kwa ndani mwisho hayo mapenzi yatabadilika kua resentment. Kubali kila mtu abaki na dini yake au tafuta mwenye dini inayofanana lkn usilazimishe kumbadilisha mtu
 
Na mimi nilipata kademu kazuri kakiarabu ila dini ndio ilizingua mimi najua kabisa home hawawezi kukubali kubadili dini na mimi siwezi kubadili dini wala dhehebu ilo nilishajiwekea kabisa kama nadhiri yangu ikabidi nimwache tu demu maana na yeye walikataa nisibadili dini mpaka leo sijabadili

Na demu nilishamwacha kabisa
Mwache tu Mkuu
Hakuna jinsi sasa kama wote mmeshindana ndio hivyo

Hakikisha ukitaka kudate na demu mwingine basi awe wadini yenu Mkuu
Hii itasaidia wewe kupata mke kabisa
 
Ila mkuu kama ww ulikua unaona kubadili dini ni jambo lahisi si ubadili wewe!!!! Yaan we unataka abadili mwenzio kwakua ww kwenu hawataki..uo ni ubinafsi....kama kweli unampenda ungemwambia msepe mbali na familia zenu wote..otherwise acha malalamishi
 
Kumwambia mtu abadili dini ni kosa ambalo niliapa kutokuja kulifanya iwe kwa mwanamke au kwa mtoto wangu na hata watoto zangu nimewambia wasije kujalibu kosa hili

Kama unaona huwez kuishi na mtu wa imani tofaut bhas ni vyema uwe unawauliza mapema ili ujue kama ni wa imani unayotaka!

katika vijana wangu kadhaa nilionao wapo watatu ambao mama zao ni Muslims,sikuwah kuwambia mama zao maswala ya kubadili na hata watoto wangu wawili walipofika umri flani waliamua kufata dini za mama zao na nililidhia kwa moyo mmoja maana daima naamini kuishi na mwanamke dini tofaut haikuondolei hadhi ya yako ya kuwa mume na pia kuwa na mtoto dini tofaut na ww haikuondolei hadhi yako ya kuwa baba yake
Pawaga
Mlifunga ndoa na huyo mazaz mwenzako??
 
Na mimi nilipata kademu kazuri kakiarabu ila dini ndio ilizingua mimi najua kabisa home hawawezi kukubali kubadili dini na mimi siwezi kubadili dini wala dhehebu ilo nilishajiwekea kabisa kama nadhiri yangu ikabidi nimwache tu demu maana na yeye walikataa nisibadili dini mpaka leo sijabadili

Na demu nilishamwacha kabisa
Mwache tu Mkuu
Hakuna jinsi sasa kama wote mmeshindana ndio hivyo

Hakikisha ukitaka kudate na demu mwingine basi awe wadini yenu Mkuu
Hii itasaidia wewe kupata mke kabisa
Hata Mimi hivyo hivyo dah ikabidi nikapotezee kalishanitajia mpaka mahali kwao
 
Kwanini usibadili wewe dini au mkaenda bomani dini inakuzuia nini wewe kuwa nae tatzo watu tunapenda sana kumchorea mipaka mwanamke
 
Kitu cha kwanza kabisa wewe huna maamuzi yako binafsi. Yaan huwezi kuamua kitu bora kwako unaamliwa na familia yako.
Binti amekubali ndoa ya bomani kwanini msifunge hio ambayo haina kikwazo kwa pande yoyote!?. Nina uhakika kabisa kama mngeshikilia uamuzi wenu wa kufunga ndoa ya bomani basi msingefikia huku mlipo.
Na kwa upande wako ungeambiwa kubadili dini uwe muislam ungekubali?
Jiulize kwanza wewe ndio ujue yeye ana uzito gani kwenye hayo mabadiliko yako.
 
Haha umeamuje mkuu?
Mkuu Mimi ni mengi sana yanayo nitatiza likiwepo na ukabila sio dini peke yake ila nimefikia uamuzi nikaona huyu ambae sio dini yangu wala kabila langu ni bora zaidi kwahiyo hakuna jinsi nikuowana tu nakufikia malengo
 
Back
Top Bottom