Kaniacha bila sababu, moyo unaniuma

mkuu fuata ushauri uliopewa na mimi naongezea kuwa bora pengo kuliko jino bovu...achana nae na kamwe usije kulamba matapishi yako kwa maana najua tu kuna mtu kamshikia akili na ninaamini atarudi mrudiane...acha kabisa kama uwezo unakuruhusu tafuta binti aliyetulia uoe.
 
pole sana kijana Tafuta pesa kwanza kwa bidii,
mapenzi utapata, muache aende akikutana na vijana wa mujini atakukumbuka😀😀
 
""Nikaenda kwa mama yake akasema nimvumilie kwa kuwa bado hajakuwa kiakili nikavumilia nikampa onyo akajirekebisha wiki mbili tu baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza anataka asikilizwe yeye tu nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana, kiburi nje nje.""

[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
Huyo mzazi wake anamtetea mwanae anasema mwanae hajakua kiakili but mi nasema mwanae amekuwa kivitendoo, ndo mana anasema hivyoo, but usijaribu kwa mzazi wake Fanya uchunguzi hata kwa Rafiki zake, usijekuta ashapewa maneno tiale
 
Huyo bado hajajua thamani yako kwake, muache ndo atajifunza
 
Nitausema ukweli utakuuma kijana mwenzangu/Mdogo wangu ni hivii elewa Huyo binti anajihusisha kimapenzi na mwanaume mwingine ,binti anampenda jamaa ila jamaa hampendi binti hizo turn around unazoziona ni pale anapozinguliwa na jamaa ,inabidi aje kupoza kwako believe me atarudi kuja kuomba msamaha tena kwako.
Nini cha kufanya sasa kama gentleman jikite kwenye vitu vya msingi katika maisha yako haswa masuala ya kiuchumi let her go, usikumbatie kaa la moto hata ukilazimisha hatokufaa maishani kwako , atakusumbua ukilazimisha kumuoa huwezi kuendelea kuishikilia kamba inayovutwa na gari/ng'ombe kisa tu kung'ang'ania kuiweka kwenye uelekeo unataka wakati kamba inakuumiza mikono yako.
 
kifupi wewe una mbembeleza mtafutie time kwanza na wewe akipiga usipoke mda mwingine mpe adhabu kama mwezi hivi then utaona wewe una muogopa kumpoteza una onyesha mi wangu alikuwa hivyo ni simple saizi kimya kajielewa
hiyo kitu ngumu sana kupractice kwa mtu anayempenda kama huyo mshikaji mtafanya awe anaangalia WhatsApp kila dk kuona kama demu yuko online au offline na akimuona roho inauma sana. Kupenda kubaya sana huyo jamaa sasa hivi ni kama anaumwa ila ndio hivyo hamna namna. Tatizo la demu wake ni kwamba ana jamaa mwingine na pia umri wake ni mdogo hivyo hajielewi
 
Mkuu wanawake wengi huwa wanajisahau sana wanapopendwa tena wakiwa na uhakika wa kutoachwa. Huwa wanadharau na kiburi sana si anajua huwezi kumuacha. Tena kibaya umeshaonesha udhaifu, hata akikuudhi unamsamehe.
Hapo lazima akusumbue tu. Mkuu kwa usalama wa afya yako usije kuthubutu kumuoa huyu mwanamke. Utajuta
 
HV kama hali hiyo inakutokea kwa MTU umeshamlipia mahari; unatakiwa ufanyeje
 
Hawa wanawake wa miaka 21 wengi wana matatizo sana. Wanachangamoto sana. Ukitaka kuoa angalia mwanamke mweny umri angalau 24 hiv
Hatari sana halafu huyu mwanamke baada ya miaka kadhaa atasema wanaume walaghai na hawana mapenzi ya dhati.
Wanawake wapo wa aina 2
1. Wife material
2. Sex material
inategemea unakutana na nani
 
Unachotakiwa kufanya ni kushukuru kwamba hamkufikia hatua ya kufunga pingu za maisha ukajua tabia zake.
 
Bora alivyokuambia ukweli kuliko aendelee kukupotezea muda.
Hata hivo vituko anafanya ili umuache lakini kwakuwa unampenda unavumilia na muda mwingine yawezekana anakuonea huruma ndo mana anakuomba msamaha.
Anakwambia hajisikii kuwa na wewe lakini kunasababu zinazomfanya awe hivo ila tu hataki au hawezi kukwambia kwakua utajisikia vibaya sana.
Muache afanye anavyotaka na wewe kuwa bizzy na shughyli zako wala usimtafute.
Akili zikimrudia atakutafuta wakati huo keshachelewa na wewe umemove on.
 
[QUOTi11, post: 17991085, member: 201241"]Unachotakiwa kufanya ni kushukuru kwamba hamkufikia hatua ya kufunga pingu za maisha ukajua tabia zake.[/QUOTE]
Mkuu sasa mtu huyo anavunjaje uchumba; na mahari ashalipa
 
kuacha au kuachwa ni jambo la kawaida sana katika huo umri wenu, take it easy bado unasafar ndefu ya kujionea mengi zaid ya hayo mdogo wangu
 
kukosa sababu na yenyewe ni sababu pia. Chapa lapa mdogo wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…