Kangi Lugola kujiunga CHADEMA?

Kangi Lugola kujiunga CHADEMA?

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
9,557
Reaction score
24,180
Salam Wakuu.

Kwenye MAWIO la leo, page 2 kwenye story ya UKAWA WAMFUKUZA ZITTO kuna habari ndani ya hii story kuwa Mh Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara leo anatarajia kujiunga na Chadema pale Mwanza. Yeyote mwenye uhakika wa hii taarifa atumwagie tafadhali.
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.
 
kinachonikwaza ni kwamba wanaojiunga au kutajwa kujiunga ni wale ambao wamepima upepo na kuona either hawakubaliki na chama au wapiga kura. yaani makapi hakuna pure grain hata mmoja. feel sad to cdm
 
huu ndo wakati mzuri wa ccm kuiteka chadema nzimanzima.
tuma makada 150 wahamie chadema na watapewa nafasi ya kugombea ubunge na wakipita wanakuwa wamo kwa maslahi ya ccm.

inaitwa infiltration
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.

Mutungirehi na MWIBARA wapi na wapi..
Ukitaka uwe great thinker uijue siasa na history.

JIMBO LILIKUWA LA MUTAMWEGA KIPINDI NIPO DARASA LA PILI PALE SHULE YA MSINGI BARAA
 
Kwani tarehe za kura za maoni ya watia nia ubunge cdm hazijapita? Au anakwenda cdm kuwa mwanachama wa kawaida?
 
Nasikia wapigaji wote wanahama CCM baada ya bosi wao kupigwa chini
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.
Pitia vizuri kumbukumbu zako,Mwibara ilikuwa chini ya TLP kwa Mhe. Mutamwega Mugahywa.
Mutungirehi alikuwa mbunge wa TLP pia jimbo la Kyerwa mkoani Kagera,siku nyingine kama huna uhakika uliza utaelezwa bila tatizo kuepuka kupotosha,tupo hapa kuelimishana,wewe unajua hiki na mimi najua kile basi tuelimishane.
 
huu ndo wakati mzuri wa ccm kuiteka chadema nzimanzima.
tuma makada 150 wahamie chadema na watapewa nafasi ya kugombea ubunge na wakipita wanakuwa wamo kwa maslahi ya ccm.

inaitwa infiltration
Sizitaki mbichi hizi.
 
Ccm ilikuwa ikiakilisha wananchi na wabunge wasiozidi kumi. Ester bulaya, kangi lugora, James lembeli, luhaga mpina, , deo filikunjombeo, ole sendeka, Kingwangala, nk. Wakiondoka hao ccm linabki kabila moja tu (mafisadi)
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.

wewe utasutwa bure we nsujure. nani kakwambia mtungirehi ni wa kibara. mtungirehi ni wa kyerwa. mtamwega mgahywa ndiye alikuws wa kibara kwa tlp. mtungirehi yuko chadema tayari na tunafikuri ndiye mpeperusha chadema kyerwa
 
kinachonikwaza ni kwamba wanaojiunga au kutajwa kujiunga ni wale ambao wamepima upepo na kuona either hawakubaliki na chama au wapiga kura. yaani makapi hakuna pure grain hata mmoja. feel sad to cdm
Una uhakika na ulichoandika lakini...??
Esther Bulaya hakubaliki Bunda..?? na James Lembeli hakubaliki Kahama..??
Usitumie za kuambiwa tu, changanya na zako japo unazo kidogo.
 
huu ndo wakati mzuri wa ccm kuiteka chadema nzimanzima.
tuma makada 150 wahamie chadema na watapewa nafasi ya kugombea ubunge na wakipita wanakuwa wamo kwa maslahi ya ccm.

inaitwa infiltration

sasa ndio umeandika nini?
 
Una uhakika na ulichoandika lakini...??
Esther Bulaya hakubaliki Bunda..?? na James Lembeli hakubaliki Kahama..??
Usitumie za kuambiwa tu, changanya na zako japo unazo kidogo.

Haya wanakubalika waambieni wakafanye mkutano bunda na Kahama, watu wajenge chama wao warukie tu ka chura kisimani.
 
Back
Top Bottom