Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,281
Waziri Lugola kupita vituo vya polisi kukagua bodaboda zinazoshikiliwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuanzia Juni 15 mwaka huu ataanza ziara katika vituo mbalimbali vya polisi kukagua utekelezaji wa agizo lake kuhusu jeshi hilo kuzishikilia bodaboda.
Mei 20 mwaka huu akiwa Bungeni Lugola alitoa maagizo kwa polisi akitaka pikipiki zinazokamatwa na kuwekwa vituoni ni zile zilizohusika katika uhalifu, zilizoibiwa na zisizo na wenyewe badala ya kuziweka kituoni bodaboba zenye makosa ya kofia ngumu au kupakia abiria zaidi ya watatu
Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Mwibara (CCM) ametoa kauli jana na kuahidi kupita hadi vituo vya polisi kuangalia utekelezaji wa agizo lake.
“Nitapita kila kituo kwa nyakati tofauti kuangalia utekelezaji wa agizo hili. Hawatajua siku, saa wala dakika watashtukia nimeibukia kwenye kituo chao, nataka suala hili liishe ili tuondoe malalamiko ya muda mrefu ya vijana hawa kuhusu bodaboda zao.”
Aliongezea kuwa:“Nawaambia nikikuta kituo chako kuna bodaboda umezikamata tofauti na makosa niliyoanisha ile kauli ya ‘ama zao, ama zangu’ niliyoisema Bungeni itatimia siku hiyo,” alisema Lugola