GE2025 Kangi Lugola: Kati ya Wagombe 17 wa Urais, 6 wamenambia wanagombea kwa sababu Samia katoa magari kwa Wagombea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kangi Lugola amepanda jukwaani kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mara waliojitokeza kumpokea Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi Agosti 30, 2025 mara baada ya kuwasili mkoani Mara.

Kangi amesema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza wake watashinda mapema sana siku ya Uchaguzi Oktoba 29, 2025 kabla hata ya saa 5 asubuhi

Amesema "Kati ya wagombea 17 tunaoshindana nao, miongoni mwao kuna Wagombea 6 ni marafiki zangu. Walikuwa wananiambia wao hawatagombea, ila waliposikia Samia katoa magari kwa Wagombea wakaamua kuchukua fomu za kugombea. Nikawapigia simu, 'mbona sasa mmenidanganya?', wakasema 'hapana sisi uchaguzi wetu ni magari tumeshatiki ila Oktoba 29, ni Mama Samia na amepita"

Kwa hiyo kumbe hayo magari yametolewa na CCM na siyo tume?

Hakika hii ndio kiini macho. Hii itakuwa historia ya pekee.

Lakini mwisho wake waja, it's just a matter of time.
 
Vyama vingi tulivikubali huku shingo ikiwa imelemewa na uzito wa chama kimoja kichwani!
 
Back
Top Bottom