Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,967
- 166,364
Mbunge wa Mwibara, Mh. Kangi Lugola ametaka mkuu wa Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya bwana Christopher Shekiondo awajibishwe kwa kushindwa kuwakamata vigogo wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya.
Amemlaumu mkuu huyo wa Tume hiyo kwa kushindwa kuwakamata wahusika licha ya kukiri wahusika kufahamika kwa kisingizio cha ugumu wa kazi hiyo.
Mbali na kutaka mkuu wa Tume hiyo kuwajibishwa,pia ametaka mabosi wake nao wawajibishwe kwani wameshindwa kumchukulia hatua.
Swali langu ni je Kikwete nae atawajibishwa na.nani kwani alidai kuwajua wahusika wa hiyo biashara na mpaka leo hajachukua hatua yeyote!
Mh. Kangi Lugola amezishutumu taasisi na idara za serilali kuhusika na biashara hiyo.Amezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Jeshi la polisi nchini,idara ya usalama wa taifa pamoja na idara ya uhamiaji.
CHANZO: TBC 1