Tausi Mzalendo
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 1,470
- 722
Asante NN, unadhani misemo hiyo ina maana gani?
"Shanuo baya pale linapokuchoma" - huu ni ujumbe na kijembe kwamba kitu ni chema hadi pale kitakapokudhuru
Nakumbuka moja niliwahi kusoma zamani "Umeyataka Mwenyewe"..
Sasa hadi leo sijui ujumbe huo ulikuwa unamhusu nani, kwanini na kwa vipi. Nilitaka hata kuuliza "imekuwaje"? Kwa kweli kanga nyingine huacha maswali bila kujibu wala kujaribu kujibu.
TM umepotea saaaaaaana assante kwa hii ya kuunga mkono ile. Ngoja tusubiri Khangaologists waje kutupa elimu hapa.
Raha ya raha ni kupata raha zaidi
Wachome wachomeke
Nakubaliana na tafsiri uliyoitoa.Ule msemo mwingine wa "wachome wachomeke" - Hii ni rusha roho hakika!Tafsiri ni jinsi wewe msomaji utakavyotafsiri. Hiyo ya raha ya raha nu kupata raha zaidi nadhani inamaanisha ukiamua kula raha basi kula kikwelikweli na usisaze kitu.
Wewe umeitafsiri vipi kwani?
Asante NN, unadhani misemo hiyo ina maana gani?
"Shanuo baya pale linapokuchoma" - huu ni ujumbe na kijembe kwamba kitu ni chema hadi pale kitakapokudhuru
duh.. hii ya kweli au umejitungia tu mbele ya safari.. inabidi nikushtukie hapa kwa kweli.
Nakubaliana na tafsiri uliyoitoa.Ule msemo mwingine wa "wachome wachomeke" - Hii ni rusha roho hakika!
Hehehehee Mwanakijiji bana. Kwani hizo zingine hazitungwi? Na kwa nini unishtukie? Ni kwamba huamini au?
Hapo zamani na inawezekana bado yanaendelea ni kwamba jirani wakigombana basi mmoja hwenda kutafuta kanga yenye ujumbe maalumu wa kumfumba jirani yake. Jioni mwenyewe huzivaa zile kanga na kukaa kibarazani nje, na huhakikisha kwamba ule ujumbe jirani anausoma.
Jirani naye akitaka kujibu mapigo basi na yeye hutafuta kanga yenye msemo wa kujibu na yeye hufanya vile vile. Basi inakuwa malumbano tu kwa misemo ya kanga.
Kanga niliyovaa leo imeandikwa 'hata na wewe nawe' nilipewa kama ujumbe kwamba nilisahau kumwalika mtu kwenye arusi basi nikaletewa zawadi hiyo. Baadae ilibidi niombe radhi.
Ndo maanake! Khanga na rusha roho ni pete na kidole.